Uchambuzi: Kuna Div 1 ya Darasani vs Div 1 ya Mtaani (akili halisi)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
UCHAMBUZI: KUNA DIV 1 YA DARASANI Vs DIV 1 YA MTAANI (AKILI HALISI).

Anaandika Robert Heriel.

Matokeo yametoka, nawapongeza waliofaulu vizuri, lakini pia Kwa waliofeli nawapa moyo kuwa wasikate tamaa kwani mtanange bado haujaisha, ndio Kwanza vita ndio imeanza.

Kwa tuliomaliza nyuma kidogo tuliamini kufaulu Kidato cha nne au cha sita ndio kufaulu maisha lakini wengi wetu Leo hii tumegundua kuwa hatukuwa sahihi.

Kufaulu darasani ni sehemu kiduchu sana Kama tone la maji kwenye bahari ya mafanikio katika maisha yetu.

Kuna Divisheni 1 ya Darasani lakini pia ipo Division 1 ya mtaani ambayo Mimi nimeiita AKILI HALISI.

Mtu akiniuliza ni Div 1 ipi kali na yaheshima kati ya hizo mbili nitamjibu Div 1 Kali na yaheshima ni hiyo ya mtaani.

Hakuna kazi rahisi Kama kupata Div 1 ya DARASANI. Hakuna kazi rahisi kama kufaulu Darasani. Ingawaje kunachosha na kunahitaji uvumilivu kutokana na baadhi ya waalimu kuwa wasumbufu mbali na changamoto zingine za kimazingara.

Mimi ni moja ya binadamu niliyepata Divisheni 1 ya Darasani, tena nikitokea shule za kata za wakati huo ambazo zilikuwa na changamoto lukuki hasa uhaba WA waalimu, uhaba wa vifaa vya kujifunza na kufundisha, uhaba wa karibu kila kitu. Hivyo najua nikisemacho.

Division 1 ya Darasani ni rahisi Sana kuliko Jambo lolote ndio maana kuna wakati nashangaa wanaojivunia kuzipata Kama vile Kina Mwijaku.

Embu tuone utofauti wa Div 1 ya Darasani Vs Mtaani

1. Div 1 ya darasani unajifunza na kukariri mambo yasiyobadilika, yaliyopita. Kwa mfano ukijifunza Laws za Physics, au fomula zake ukazielewa vyema ndizo hizo hizo zitakazltoka kwenye mitihani, au ukijifunza Historia labda ya mambo ya kale au vita ukizi-master ndizo hizo hizo zitakazotoka kwenye mtihani, hapo muhimu ni kukumbuka na kujifunza Basiii!

Div 1 ya darasani inahusu mambo yaliyopita, yaliyowahi kutokea. Hivyo ni uwezo wako tuu kujifunza na kuyakariri na kuyaelewa. Kiufupi Div 1 ya darasani inatabirika.

Yaani mtu anaweza akawa na uhakika atafaulu kutokana na alivyojipanga

Lakini Div 1 ya mtaani unajifunza kila siku na kamwe huwezi kukariri. Siku ya Leo huja na mambo yake na kesho hujui nini kitajiri. Div 1 ya mtaani kuipata ni ngumu Sana Kwa sababu inahusu mambo yajayo ambayo huyajui.

Div 1 ya Mtaani haitabiriki na ni ngumu kuipata Kwa sababu inahitaji macho ya kiroho zaidi tofauti na Div 1 ya darasani ambayo inahitaji Macho ya kimwili na akili yenye kumbukumbu.

2. Div 1 ya Darasani uwanja wake wa vita ni kitabuni na kwenye karatasi lakini Div 1 ya mtaani uwanja wake wa vita ni popote pale.

Hii ni kusema aliyepata Div 1 ya darasani ni Kama vile aliyemaliza Mafunzo ya mwanamgambo tuu. Wakati aliyepata Div 1 ya mtaani ni Komando ambaye uwanja wake wa vita ni mpana. Anaweza pigana popote pale akashinda mapema tuu.
Iwe ni mjini au vijijini, iwe ni baharini au nchi kavu, iwe kwenye njaa au penye chakula komando ana-survive.

Usishangae wenye Div 1 wengi wao nje ya Mfumo wa elimu na kuajiriwa hawana jipya, na huanza kulalama na kupiga mayowe, usiwalaumu ni Wanamgambo ambao wako limited, uwanja wao wa vita ni kwenye karatasi tu.

3. Mitihani ya wanaopata Div 1 za darasani inatangazwa mapema Kabisa na tarehe zake zinafahamika. Hivyo humfanya mtu ajiandae mapema kadiri ya awezavyo. Kama mtu akijitambua ni kilaza basi hupaswa kufanya mazoezi ya mara Kwa mara, kusoma kila mara ili kuibusti akili yake. Na hatimaye ataipata tuu hiyo Div 1.
Lakini mitihani ya Div 1 za mitaani hazina tarehe mahususi, yaani ni siku yoyote Ile unapigwa na kitu chenye ncha Kali.

Kwanza hakuna wa kukutangazia kuwa mwezi ujao utafilisika au utaachwa na Mkeo/mumeo au utaibiwa Mali zote, au utafungwa jela, au mafuriko yatagharikisha mazao yako yaani mtihani wowote kitaani unaweza kuupata saa na wakati yoyote. Iwe mchana, Asubuhi au usiku, uwe umelala au upo macho.

4. Div 1 ya darasani ukijiandaa umejiandaa, lazima ufaulu. Lakini Div 1 ya mtaani unaweza ukajiandaa na ukashindwa vilevile alafu Wale ambao hawajajiandaa wakashinda.

Mambo ya kuzingatia ili upate Div 1 ya Mtaani.

1. Mafunzo makali ya ukomando.
Lazima ujifunze kupambana katika Mazingira yoyote Yale. Majini na Nchi kavu, mistuni na jangwani, angani na ardhini. Penye Ajira na pasipo na AAjira. Penye njaa na palipo na chakula. Penye Giza na palipo na Nuru.

Jifunze kutumia silaha zote, tumia mwili panapo hitaji mwili, tumia akili panapohitaji akili, tumia hisia panapohitaji hisia, tumia roho panapohitaji roho.
Zote hizo ni silaha ambazo komando anapaswa Ajue kuzitumia Effectively. Usizubae zubae.

2. Jifunze kufungua Macho ya Kiroho.
Div 1 ya mtaani inahitaji uwe na macho ya kiroho. Uone mbele ukiwa nyuma, na uione nyuma ukiwa mbele. Kitu chochote kabla hujakifanya ukione mwisho wake, yaani ujue matokeo yake kabla hujakianza.

Kama kuna matatizo/mitihani IPO mbele yako inakuja basi uione kabla haijaja, fungua jicho lako la kiroho ili usiende Kama kipofu.

3. Uthubutu na ujasiri
Uthubutu na ujasiri unaletwa na hoja mbili zilizotangulia. Huwezi kuwa mthubutu na mjasiri Kama hujapata Mafunzo ya kikomandoo na hujafungua jicho la Rohoni.

Ukishakuwa na Mafunzo yakutosha ya ukomandoo kisha ukawa na macho ya rohoni basi utakuwa na uthubutu na ujasiri na nihaki yako kuwa hivyo.

Kuna watu wanawafundisha watu ujinga kuwa Maisha yanahitaji uthubutu na ujasiri bila kuwaambia mambo hayo ni mpaka wapate Mafunzo ya kikomando na jicho la rohoni lifunguke ndio ulete uthubutu na ujasiri wako.

Maisha ni vita, huwezi ends vitani na ujasiri a uthubutu Kama huna Mafunzo ya kutosha, utashindwa mchana kweupe na kupoteza maisha yako.

Jifunze ukomandoo kisha fungua jicho la rohoni kisha ujasiri utakuja automatically.

Kwa mfano unaenda kulima,
Ni lazima ujue ABC za zao unalolilima,
Ardhi utakayolimia, Tabia ya nchi na Hali ya hewa, Kisha utaangalia uchumi wako na soko la zao Hilo.

Mwisho kabisa utafungua macho ya rohoni yaangalie mbele kutatokea nini ili ukabiliane nacho.

Macho ya Rohoni yanafunguliwa Sehemu mbili;
1. Kwa kumuomba Sana Mungu. Kufunga, kujitakasa na kumuomba Mungu akuonyeshe ishara au yatakayotokea mbele ya kile unachoenda kukifanya, kisha akupe Kibali chakufanya au akuzuie.

2. Kwa kwenda wa Waganga, waganguzi, na walozi.

Usithubutu kufanya Jambo lolote pasipo kuwasiliana na falme za rohoni unazoziamini. Utaishia kulalamika tuu na kuanguka vibaya.

Unalima heka 10 unapata Gunia 10, hilo ni anguko kuu.

4. TUNZA AKIBA.
Ukomando ni pamoja na kuweka Akiba. Iwe Akiba ya silaha, mbinu na mikakati, au akiba ya mali zitakazotumika nyakati za Dharura, Ghafla na nyakati ukiwa hujiwezi.

Usitumie mbinu zote kana kwamba Leo ndio mwisho wako wa kuishi.

Div 1 ya darasani ili uipate kanuni yake ni moja tu. 1. Jifunze na kariri yote ya zamani na uwe na kumbukumbu.

Inatosha sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Huu Ni ujinga, Mfumo wa Elimu unapimwa Kwa Division 1 ya darasani!

Kaja Magu kuvuruga kila biashara, finally Wenye Elimu ndo walikuwa Na ahueni!

Mwanaume Ni: mpiga darasaani Na nje, Ila huwezi Shusha elimu ya darasaani ambayo Dunia inaitambua!
 
Msiwatishe Vijana Wana Wapambane Kwenye Majukumu Tuliowapatia Ya Kuitafuta Elimu Kwa Nguvu Na Akili Zao Zote.
 
Ngoja waje vipanga,mm na division five yangu naenjoy life.
Yes, nwisho wa siku lengo ni kuenjoy maisha tu..hayo mengine tunapita tu....

Mimi siku hizi hata sishtuki kusikia mtoto kapata 1.7 because, what i have seen in real life...ni struggle....
 
Piga, ua, alie nacho ataongezewa tu....

Weka malengo ya juu sana kwenye kila ufanyalo. Hata ukianguka hutaangukia chini sana.

“Basi lolote upatalo kulifanya lifanye kwa nguvu zako zote, na bidii zako zote, na maarifa yako yote.....”(Mhubiri 9:10)

Macho ya kiroho yapo kila mahali iwe darasani au mtaani.

Wengi wa wahitimu wazuri darasani ni wahitimu wazuri pia wa ‘school of hard knocks’.
 
Yes, nwisho wa siku lengo ni kuenjoy maisha tu..hayo mengine tunapita tu....

Mimi siku hizi hata sishtuki kusikia mtoto kapata 1.7 because, what i have seen in real life...ni struggle....
Wengi hawataki kuamini,najiuliza yale mamilion ya pesa wazee wangu waliyokuwa wananipa hv namm kweli nitakuja kuwapa wanangu kweny huu mfumo mbovu wa kielimu?

Bora mwanangu nimsomeshe kwa mitaala mingine kbs
 
Huu Ni ujinga, Mfumo wa Elimu unapimwa Kwa Division 1 ya darasani!

Kaja Magu kuvuruga kila biashara, finally Wenye Elimu ndo walikuwa Na ahueni!

Mwanaume Ni: mpiga darasaani Na nje, Ila huwezi Shusha elimu ya darasaani ambayo Dunia inaitambua!
Sizani km mtoa mada amebeza elimu ya Darasani. Nilichokiona mimi ameelezea sifa za elimu ya Darasani,na elimu ya mtaani. Na hajasema watu wasisome elimu ya Darasani.
 
Back
Top Bottom