Lugha zifuatazo hazifundishwi darasani na mwanadamu yeyote

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,125
22,615
Salaam, shalom,

INTRODUCTION.

Lugha ni chombo na mawasiliano, ni nyenzo ambayo hutumika kama kiunganishi kati ya mtu mmoja na mwingine au kundi moja na jingine.

Lugha hizo zaweza kuwa Rasmi au zisizo Rasmi, pia lugha zaweza kuwa zinazotamkika zingine zaweza kuwa za Ishara.

Dunia ilipoumbwa, tulikuwa na lugha Moja tu, lakini baada ya uasi pale katika ujenzi wa Mnara wa Babeli, lugha zilichafuliwa na watu walisambaratika kwenda sehemu mbalimbali.

Lugha hizi unaweza jifunza mwenyewe Kwa kukaa na wahusika au ukafundishwa darasani.

AINA KUU ZA LUGHA.

1. LUGHA ZA WANADAMU.
Lugha hizi, nimejaribu Kwa uchache kuziainisha hapo juu


2. LUGHA ZA MALAIKA/ LUGHA ZA MBINGUNI.(1 Korinthians 13:1-2), (Matendo 2:1....).
Hapa kwenye aina hizo za lugha, ndipo penye mada. Lugha hizi hutumika kumsaidia mtu aliye duniani kuwasiliana na Mbingu Kwa haraka na Kwa Siri bila ukinzani na uchakachuzi wa adui.

3. LUGHA ZA WANYAMA,NDEGE,WADUDU, MITI, ARDHI NK NK.


Lugha hizi pia Zina upana wake kulingana na uelewa na Maarifa.

4,5,6....


LUGHA AMBAZO HAZIFUNDISHWI NA WANADAMU.(1Korinthians 14-15).(Matendo ya mitume 2:1...), (1 Corinthians 13:1-2), (1 Corinthians 12:1-12)

Hizi nimeziainisha kipengele namba 2 hapo juu. Yaani, LUGHA ZA MALAIKA/ LUGHA ZA MBINGUNI.

Lugha hizi za Malaika, Mbinguni, zimegawanyika katika makundi matatu. Lugha zote hizi hazifundishwi na wanadamu.

1. LUGHA ZA UNABII, PROPHECY. (1 Corinthians 13:1-2), (Acts 2), (1 Corinthians 12:1-12).


Lugha hii ni kipawa pia, mtu aliyejazwa Roho mtakatifu na kunena Kwa lugha, hutabiri Kwa kuongea Kwa lugha za Mbinguni/Malaika akileta ujumbe wa Mungu, pia hupewa uwezo wa KUTABIRI Kwa lugha za WANADAMU Kwa uwezo wa Roho mtakatifu. Pia lugha hii haifundishwi na wanadamu, Si sahihi kukariri na kuigiza kunene Ili uonekane nawe una upako.

2. LUGHA ZA WANADAMU BILA KUFUNDISHWA.

Lugha hii pia ni kipawa, mtu wa Mungu,mtanzania muhubiri Kwa Mfano, amekwenda kuhubiri Ufaransa na hajui lugha ya kifaransa, ghafula akiwa jukwaani akihubiri Kwa kutumia mkarimani, anaweza kujazwa Roho mtakatifu akajikuta akihubiri Kwa kifaransa na wafaransa wakaelewa, na akimaliza kuhubiri, inakata. Kipawa hiki ni zawadi atoayo Roho MTAKATIFU kulingana na mazingira. Lugha aina hii haihitaji mfasiri,maana Roho huileta Kwa lugha za WANADAMU kabisa.

3. LUGHA YA MAOMBI/ KUNENA KWA LUGHA. (Acts 2:1...)

Hiki ni kipawa mtu aliyeokoka hupewa baada ya kuomba, au kupokea automatically baada ya kuokoka na kujazwa Roho mtakatifu. Kamwe haifundishiki na wanadamu.

Lugha hii ni lugha ya maombi, ni Siri kati ya mtu akiongozwa na Roho mtakatifu kuongea na Mungu direct. Ni Siri Ili kuwapiga chenga mapepo wasijue unaomba nini au unatumia silaha Gani katika maombi. Pia lugha hii ni zawadi atoayo Roho mtakatifu, haifundishwi na wanadamu, kamwe usikariri.

Lugha hii haihitaji mfasiri. Na hunenwa sirini kati ya mtu na Mungu.

NB: Ukipita katika makanisa, maarufu kama, makanisa ya kilokole, wakiwa katika maombi, unaweza sikia wakiomba Kwa lugha za WANADAMU kama kawaida, lakini hufika Mahali, Wana switch na kuanza kuomba Kwa kutamka Kwa lugha isofahamika na hadhira Ile, na Kuna wakati, hawawizi hata kujizuia Ili kurudi kunena Kwa lugha za WANADAMU, Hadi Roho mwenyewe aamue mtu kurudi katika lugha ya kawaida.
Lugha hii kamwe usijaribu kuifundisha Kwa mwingine, lugha hii hupatikana Kwa njia ya kupewa zawadi au kipawa.

Lugha hizi hazifundishwi, hazifundishwi, hazikaririwi, hazidurufiwi.

HITIMISHO.
Ni muhimu Kwa wote waliookoka kuomba Kwa bidii Ili kupokea zawadi na kipawa hiki, ni muhimu sana.

Kuna wakati wa kuomba Kwa mwili, na kunena Kwa Roho, yaani Roho ndani Yako na Roho mtakatifu ndani Yako anakuconnect na Mbingu Ili kupeleka sifa, haja na shukrani katika KITI Cha enzi.

ANGALIZO: Kamwe usiigize kunena Kwa lugha Kwa kukariri Jirani Yako anachonena, sababu ni Siri na ni kosa. Mwombe Mungu kupitia Yesu Kristo Ili upewe kipawa hicho Bure.

Kunena Kwa lugha ni hatua ya juu zaidi ya kiroho, hivyo ukitamani kufikia hatua hiyo, lazima uishi maisha ya utakatifu na udumu katika maombi na kusoma neno muda wote na kulitafakari.

Mungu wa Mbinguni awabariki.

Amen
 
Tamani sana kunena Kwa lugha. Omba Kwa bidii, utapokea karama hiyo.

Aombaye na anenaye Kwa lugha, anena na kuomba Kwa Roho, hivyo hachoki kama aombaye KIMWILI.
 
Back
Top Bottom