Uchambuzi huru: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya Aprili 22, 2021

Ndugu mwandishi unataka kuniaminisha hao mabeberu ndio wanatuchelewesha sisi kama taifa kuendelea yan kushirikiana na mabeberu ndio chanzo cha kukosa maendeleo
 
Sioni kosa kwa huo mtazamo wa Rais, hiyo dhana ya kila Rais kuja na mtazamo wake imeasisiwa na watangulizi wake, hivyo naye sio wa kwanza, japo hii tabia kwa namna fulani inachangia kuturudisha nyuma kitaifa, binafsi ningependa pawe na kitu kama succession plan kwa hawa viongozi wetu, anapomalizia mmoja ndipo aanzie mwingine.

Kuhusu kuvutia wawekezaji yupo sawa, hawa watu tunawahitaji na dollar zao watasaidia kwa namna kupunguza tatizo la ajira nchini, na kuongeza mzunguko wa pesa kwa watanzania kama anavyojinasibisha Rais, japo anatakiwa kuwa na tahadhari ahakikishe analinda maslahi yetu kama taifa.

Mfano. Alipozungumzia uchimbwaji wa madini ya Hellium yaliyopo kwenye mbuga fulani akasema Simba hawayali yale, sawa hawayali, lakini awe makini kwenye mikataba serikali yake itakayoingia na wawekezaji coz record za mikataba na wawekezaji kwa viongozi wa awamu zilizopita ni mbovu.

Mwisho kabisa unajinasibu kwa ujamaa kwa kusema wewe unaamini maendeleo ya mwafrika yataletwa na mwafrika mwenyewe, hiyo dhana kiukweli kwangu imepitwa na wakati, huu ujamaa wa mwafrika utaleta maendeleo gani bila kuwa na teknolojia, capital, na skilled man power inayohitajika? hapa unanikumbusha ile kauli ya Nyerere aliposema madini yaachwe ardhini yatachimbwa na mtanzania akiwa tayari.

Sasa kuliko kuendelea kusubiri huo utayari kwa serikali hii ya CCM ambayo imekuwa ikipigana na maadui watatu (ujinga, umaskini, maradhi) toka tupate uhuru zaidi ya miaka sitini sasa, huo utayari wa kuchimba wenyewe tutaupata lini? naona bora tuwape wazungu wachimbe, lakini tuhakikishe tunapata faida badala ya kuwaachia wazungu waondoke na faida huku viongozi wetu wakipata 10% na sisi kuachiwa mashimo.
 
Wewe kwanza tengeneza internet yako, halafu tengeneza maandishi yako, uache internet ya mabeberu na herufi za mabeberu.

Halafu tuite huko kwenye internet yako ambayo haijatumia teknolojia ya mabeberu tujadili hoja zako za kijima.

Hapo angalau nitakuona uko serious.

Lakini maadam bado unatumia internet ya mabeberu na herufi zao, mimi nakuona mnafiki tu ukiwakataa mabeberu kwa misingi uliyoiandika hapa.

Ama mnafiki, ama mjinga.

Inawezekana kabisa mnafiki mjinga.
Mkuu Kiranga ni tatizo la uelewa tu. Tumueleweshe taratibu huenda akaelewa na kesho akawa mjumbe wa positive change. Tumuelimishe mkuu Mkandara maana huwezi jua, pengine ana dhamira njema tu lakini hana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya uchumi wa kisasa
 
Wewe ni miongoni mwa watu wenye upeo wa chini sana! Itakuchukua miongo mingi sana kujua anachoongea Mama Samia !

Wanyonge unaowazungumzia Rais Magufuli aliwapigania je ni pamoja na Paulo Makonda akiyekuwa akipora fedha za watu huku akitembelea Range Rover na Lamborghini?!

Rais Magufuli aliwahi kumkemea Paulo Makonda kuhusu tabia zake hizo?
Ndugu hujitambui na wala huijui Dunia tuliyonayo sasa.

Rais Magufuli alikuwa na nia nzuri ya kujenga Taifa Ila alikuwa na mawazo primitive sana ( mawazo ya kizamani) na hakuwa na "exposure" kubwa kuhusu Dunia inavyo operate!

Mama Samia inaonekana anayo "exposure" na anajua Dunia inavyo operate tunasubiri usimamizi wake.
Kama atakuwa na usimamizi mzuri atamfunika Rais Magufuli asubuhi sana!
Rais Magufuli alikuwa anajenga Nchi kwa jasho na damu la Watanzania!

Watu walikuwa wameshachoka sana,mlibaki wewe na akina Makonda mnafurahia matunda ya Nchi hii!
 
Ujamaa ni mfumo usiyo halisia na hauendani na utashi wa mwanadamu, mataifa yote yaliyo kuwa na huo mfumo yamefeli na hatimaye yameangukia kwenye ubepari, China ni rafiki zetu lakini wao wamekuja na mikataba ya kibepari, sasa sijui huo ujamaa umekuwa ujamaa mambo leo!
Mama Samia atatumia ilani ileile ya CCM lakini style ya utawala ndiyo itabadilika.
 
Kuna mifumo ya kizamani dunia ilipokuwa ni kama inaanza na kila mtu alikuwa hana kitu, was the big struggle....kwa sasa dunia imeendelea sana kwenye mambo mengi na vitu vingi hupatikana kwa urahisi..

Tunapozungumzia uwekezaji tunazungumzia watu wenye mitaji kuanzia ya hela, akili na teknolojia...watu hawa wako mbele miaka mingi kwa kila kitu....kuwaalika na kuchangamana nao maana yake tunachangamsha uchumi wetu na watu wetu wanapata mitaji, akili, maarifa, teknolojia nk vitu hivi vikifika kwa watu wetu nao watapata uwezo wa kuwekeza hapa na kwingineko....China tunayoiona imekua kwa uwekezaji kutoka ulaya na kujifunza maarifa kutoka ulaya..
 
Ujamaa ni fikra za kimasikini karne hii, Ujamaa inawezekana zilikuwa fikra nzuri zama za zamani..Kwa sasa kuwaza ujamaa wakati ubepari umetamalaki duniani kote ni kuutafuta umasikini tu na kuwafanya watu wako primitive..
 
Umejitahidi kuchambua japo Uchambuzi wako ni wa Masikini Jeuri, wa kua na Mawazo Makubwa bila ya Uwezo wa Kutenda.

Mama Samiah anataka tufanye tunachoweza kufanya sasa wakati tunaendelea kujenga Uwezo wa kufanya hayo unayoyaelezea.

Tunahitaji Uwekezaji wa Ndani na pia tunahitaji Uwekezaji kutoka nje ili kuendelea kujenga Uwezo wa kujenga Uchumi wa Kujitegemea.
Amekuambia haya yalishafeli kwenye tawala zilizopita. Ndo maana tukaja na approach mpya lakini sasa tunarudi tulipotoka.
 
Kuwalinganisha Wawekezaji na Mabeberu ni hoja Muflisi

China unayoiona kuwa ni nchi ya Kikomunisti bila kufungua uchumi wake na kuvutia uwekezaji leo hii ingeendelea kuwa hohehahe.

Cha msingi uzungumzie uwekezaji wenye Tija na kuhakikisha tunanufaika na uwekezaji huo

Hata huyo Magufuli unayemsema, aliunda wizara ya Uwekezaji na aksiaeka chini ya Ofisi ya Rais akiamini kuwa kwa kufanya hivyo atasaidia kuondoa vikwazo vya uwekezaji nchini.

Halafu mada yako inaturudisha kwenye mijadala ya Kiitikadi ya twende na Ujamaa au Ubepari.
Ujamaa ulishamshinda Nyerere unataka turudi hukohuko kwenye kufeli?
Na huyo Magufuli wako hakuwa mjamaa, alikuwa ni authoritarian tu
 
Mkuu, huo Ujamaa wa Mwafrika unavutia sana kinadharia. LAKINI kiuhalisia (practically) hautekelezeki. Mwalimu aligundua hilo mwanzoni mwa 1980s akaamua kuachia madaraka kwa AHM 1985 akiridhia afuate mwelekeo mpya kunusuru Taifa. Yeye binafsi alichelea kugeuka “Jiwe”!

Tatizo kubwa ni kuwa huo ujamaa ukishindwa na kuanza kutoa athari hasi, viongozi huzidisha propaganda na utawala wa kiimla huku wakizima uwazi na kutumia muda na rasilimali nyingi kupambana na mawazo mbadala (dissent). Ndio maana leo hii tunaongea kuhusu kurejesha muafaka wa kitaifa.
 
Unamkataaje beberu na huku maisha yako yote yanamtegemea beberu.
Kama siyo beberu ungetype hapa wewe?
Hiyo keyboard unafikiri imeokotwa mpitimbi?
Hotuba yake umeisikiliza kwa kuwezeshwa na beberu.
Kesho huwezi enda kazini bila ya uwezeshwaji na beberu.
Hata ulipolala usiku huu mkono wa beberu umegusa.

Tunachotakiwa kukifanya ni namna ya kumbenefit huyu beberu kabla hajatushtukia kuwa tunamnyonya eyeye- hapo ndipo penye uzalendo wa ukweli.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom