Uchambuzi huru: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya Aprili 22, 2021

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Kwa rehma zake Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu sote tutaumaliza Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan salama salimin na hakika yeye ndiye mwenye kurehemu riziki zetu kubwa na ndogo na hapana mwingine apaswaye kuabudiwa. Tumuombe sote atuepushe na kila lisokuwa na kheri kwetu. Ameen.

Nina hakika siku ya leo tutasikia SIFA kemkem za mafuta ya tin na zaitun zitamiminika kupamba na kusifia hotuba ya rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassan kwa sababu imewagusa watu wote katika mazingira tofauti katika mwelekeo mpya wa dira ya Awamu hii ya sita ikitekeleza kauli mbiu ya KAZI IENDELEE.

Mimi binafsi, niseme ukweli wangu kutoka moyoni ya kuwa sii mshabiki wa rais Mama Samia Suluhu Hassan toka hotuba yake ya kwanza alipo apishwa kama rais wa Awamu ya sita. Huu ndio ukweli wangu! Na sababu zangu ni ndogo kabisa, nilimsoma toka mwanzo mwelekeo na Dira yake Kitaifa, dira ambayo Kiitikadi, mimi sii muumini wake na hupingana na nadharia zinazofungamana zaidi na UBEPARI badala ya UJAMAA wa Mwafrika.

Hivyo unaponisoma hapa ni muhimu Uzingatie kuwa mimi ni muumini wa UJAMAA wa Mwafrika na naamini Maendeleo ya Tanzania yataletwa na WATANZANIA wenyewe badala ya WAWEKEZAJI kutoka nje. Imani ya kwamba maendeleo yetu yanahitaji kuweka masharti rahisi ili kuvutia Wawekezaji ni sawa na fikra za.Kitumwa za Mababu zetu walokubali kupewa na wakoloni Shanga na vilemba ili tupendeze huku wagenu wakiondoka na madini mali ghafi na nyara zetu za Kitaifa.

Niseme wazi kwamba binafsi yangu naiona tofauti kubwa sana baina ya Hayati rais wa awamu ya Tani John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na kwamba hawa sii kitu kimoja hata kidogo. Tofauti zinazotokana na ahadi za mabadiriko makubwa ya SERA na SHERIA ambazo Chama cha Mapinduzi na Hayati Magufuli walizitumia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi wa mwaka 2020. Niseme kwa nini nasema hivi?

Haina Shqka kabisa, Hayati Magufuli alikuwa rais anayepigania maslahi ya Wananchi Wanyonge kwa maana ya Watanzania Maskini dhidi ya Wawekezaji Mabeberu tofauti kabisa na Dira na Mwelekeo wa Mama Samia anayetazama zaidi viwashwishi kwa maslahi ya WAWEKEZAJI pamoja na dhana ya UKUONGEZA UZALISHAJI wa Mazao kwa WINGI zaidi (Quantity) badala ya fikra za Magufuli kudhamiria Kuanzisha viwanda vya ndani ili Kuongeza thamani ya Mazao yetu ya Asili yalokuwa BORA zaidi (Quality).

Nimalizie tu kwa kusema, rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan awe makini sana na dhana hizi, kwani hatukuanza jana wala juzi. Tulifuata mrengo ule toka wakati wa Rais Ally Hassan Mwinyi, akaja Mh. Benjamin Mkapa na Mwishowe mstaafu Jakaya Kikwete, na kote huko nyuma tulifanya makosa mengi sana kwa dhana ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Biashara. Matokeo yake tukaunda Matabaka ya Walionacho na wasiona nacho baina ya Wainanchi wenyewe. Ndipo Ufisadi na rushwa viliposhamiri kwani hapana alotaka kubakia katika kundi la wasionacho (Maskini)

Maoni ya rais kuhusu matumizi ya mbinu za kisasa katika Kilimo, kuna hatari kubwa ya nchi yetu kurudi kutawaliwa tena Kiuchumi kutokana na ujio wa mbegu za maabara ambazo zitaondoa kabisa rutuba ya Ardhi yetu, ubora wa mbegu zetu (Organic) na kubwa zaidi kumikilisha Mashirika ya nje nguzo za Uchumi wetu Kitaifa.

Maasalaam,
- Ramadhan Kareem
 

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
454
1,000
Umejitahidi kuchambua japo Uchambuzi wako ni wa Masikini Jeuri, wa kua na Mawazo Makubwa bila ya Uwezo wa Kutenda.

Mama Samiah anataka tufanye tunachoweza kufanya sasa wakati tunaendelea kujenga Uwezo wa kufanya hayo unayoyaelezea.

Tunahitaji Uwekezaji wa Ndani na pia tunahitaji Uwekezaji kutoka nje ili kuendelea kujenga Uwezo wa kujenga Uchumi wa Kujitegemea.
 

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
928
1,000
Hata akikutana anataka wajadili jinsi ya kufanya siasa zenye tija kwa nchi.

Maana yake baada ya kukutana hatutarajii kuwaona akina Lisu wakiponda Atcl, Sgr, bwawa la Nyerere kuwa ni miradi ya hovyo badala yake wataanza kusema hiyo ni miradi ya watanzania.


Kwa akili zao wanahisi mama ataenda kuwaruhusu kufanya maandamano kila siku.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,511
2,000
Wewe kwanza tengeneza internet yako, halafu tengeneza maandishi yako, uache internet ya mabeberu na herufi za mabeberu.

Halafu tuite huko kwenye internet yako ambayo haijatumia teknolojia ya mabeberu tujadili hoja zako za kijima.

Hapo angalau nitakuona uko serious.

Lakini maadam bado unatumia internet ya mabeberu na herufi zao, mimi nakuona mnafiki tu ukiwakataa mabeberu kwa misingi uliyoiandika hapa.

Ama mnafiki, ama mjinga.

Inawezekana kabisa mnafiki mjinga.
 

hans_mbawa

Member
Oct 8, 2016
66
125
I like this one though you missed some points.

Kila mtawala huja na vipaumbele vyake, so It doesnt matter ana ideology kinachoangaliwa ni suala zima la maendeleo yatafikaje na kwa wakati gani!!!!!

Lakini pia serikali ni wananchi, unaposikiliza kero zao na kuzitafutia majibu, kwa mwanasiasa huu ni mtaji. Nadhani Mama Samia anatafuta njia fulani zitakazofanya aimbwe kwenye midomo ya watu ilihali anakamilisha ilani za chama chake.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Mkuu Mkandara habari za siku nyingi?

Binafsi nimefurahi sana kuona wajenga hoja wazuri kama wewe wanaanza kurudi kwenye mijadala. Hii peke yake ni hatua nzuri inayoashiria kuwa tumepiga tena hatua na kurudi kwenye awamu ya hoja kwa hoja na si hoja kwa ngumi.

Kuhusu hotuba, kwa upande wangu nilitegemea kusikia niliyoyasikia na zaidi kidogo. Hata hivyo yaliyosemwa yamesemwa vizuri na ambayo nilitaraji yatasemwa zaidi na hayakusema naamini ipo siku yatasemwa. Kila kitu ni hatua.

Kuhusu approach za uwekezaji, mama yupo sahihi sana. Unapozungumzia habari za ujamaa na ubepari, inawezakana huelewi vyema implications ya dhana hizo katika ulimwengu wa sasa.

Suala hili la uwekezaji na nadharia za ujamaa na ubepari kama ulivyoliweka ni mjadala unaohitaji utulivu na ulivyouweka, umeuweka kijuu juu mno kiasi kwamba ni rahisi amma kutoeleweka vyema au kupotosha mambo kadhaa. Nikitulia nitarudi tujadiliane jambo hili kwa kina.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,736
2,000
Mkuu wewe ni yule Rufufu Mkandara mchambua mikanda ya video? Yaani hapa ndio umechambua hotuba ya Rais Samia? Haki ya nani Kanda ya Ziwa inatapatapa!! Uliposikia anasema kuongeza uzalishaji wewe ukenda kwenye GMO? Mbona mama alikuwa wazi kabisa kwamba wataiongezea uwezo (mtaji) ASA ili izalishe mbegu za kutosha kuliko kutegemea mbegu za kutoka nje! ASA haizalishi GMO mkuu! Naona mnahaha!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom