Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Naona niwapatie majina ya kata pamoja na idadi ya waliojiandikisha kupiga kura kama ifuatavyo;

1.Bwagamoyo 3276,
2.Dongo 6717.
3.Dosidosi 2715.
4.Engusero 7791.
5.Kibaya 3092.
6.Kijungu 3233.
7.Lengatei 3283.
8.Makame 2490.
9.Matui 10677.
10.Ndendo 1587.
11.Njoro 4687.
12.Olboloti 2828.
13.Partimbo 10077.
14.Songambele 5794.
15.Sunya 6311.
 
Kuhusu Kiteto,ni kuwa vyama vilivyoko kwenye ushirikiano wa vyama vimekubaliana kumsimamisha mgombea wa CHADEMA ambaye ni ndugu Victor Kimesera.

na leo CHADEMA wametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uteuzi huo wa Kimesera n.k.

Kwa wanaomfahamu Kimesera, je mnaweza kutusidia kujua ni mwanasiasa wa aina gani?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA imefanya kikao chake Januari 26, 2008 chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Kikao hicho maalumu cha Kamati kuu kilifanyika katika Hoteli ya Markham jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na ajenda nyingine kilijadili na kumpitisha Victor Parkimaro Kimesera kuwa mgombea ubunge jimbo la Kiteto kupitia CHADEMA. Kimesera ndiye aliyekuwa mgombea pekee aliyependekezwa na Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Kiteto kilichoketi Kibaya Januari 20, mwaka 2008.

Kimesera amewahi kuwa mgombea katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kupata asilimia 42 ya kura zote wakati huo. Kimesera mwenye shahada ya falsafa amewahi kuwa mtendaji mkuu wa taasisi na makampuni mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Kimesera amewahi pia kuwa Katibu Mtendaji na Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA katika nyakati mbalimbali. Kwa sasa Kimesera ni Mkurugenzi wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Taifa. Kadhalika Kamati kuu imepitisha Mkakati/Mpango wa Kampeni ya uchaguzi katika Jimbo la Kiteto.

Aidha Kamati Kuu imepitisha pia Mwongozo kuhusu utekelezaji wa maadili, itifaki na kanuni za chama juu ya uendeshaji wa kampeni za uchaguzi ndani ya chama; kutokana na kanuni za chama vifungu vya 10.1, 10.2 na 10.3. Lengo la mwongozo huo ni kufafanua mambo yanayoruhusiwa na mambo yasiyoruhusiwa kufanywa na wagombea na viongozi wakati wa kampeni za uchaguzi wa ndani ya chama ili kuhakikisha chaguzi za ndani ya chama zinakuwa huru, zenye uwazi na haki.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Habari na Uenezi inapenda kuchukua fursa hii kuutaarifu umma wa watanzania kwamba tayari CHADEMA imekwishaanza kujipanga kushinda uchaguzi katika jimbo la Kiteto.

Timu ya Awali ya Kampeni inaondoka hivi karibuni kwenda kukamilisha maandalizi ya awali ikijumuisha Dr Ben Kapwani -Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa; Joseph Fuime-Mwenyekiti wa Mkoa wa Ruvuma; Afisa Mwandamizi wa Sera na Utafiti- Danda Juju Martin, Mheshimiwa Halima Mdee- Mbunge wa Viti maalum na Wakili wa kujitegemea; Jafari Kasisiko- Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma na Chiku Abwao- Mjumbe wa Kamati Kuu.

Aidha Kampeni za CHADEMA zitazinduliwa rasmi Februari Mosi na Dr Wilbroad Slaa(Mb)- Katibu Mkuu. Kadhalika viongozi wengine watakaoshiriki kampeni hizo ni pamoja na Chacha Wangwe(Mb)-Makamu Mwenyekiti na Zitto Kabwe(Mb)- Naibu Katibu Mkuu; wakurugenzi, madiwani na viongozi mbalimbali wa chama wilayani Kiteto. Pamoja na viongozi wa CHADEMA, Kampeni hizo pia zitahusisha viongozi wa vyama vilivyoko kwenye ushirikiano vya CUF, TLP na NCCR Mageuzi ambavyo kwa pamoja vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja. Viongozi wengine wa kitaifa watakaoshiriki kampeni hizo watatangazwa katika hatua za baadaye.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi inapenda kusisitiza kuwa CHADEMA imejizatiti kushinda jimbo la Kiteto kutokana kuwa na timu mahiri na mgombea anayekubalika katika jimbo hilo. Aidha CHADEMA imedhamiria kukuabiliana na vitendo vya hujuma wakati wa uchaguzi huo na itahadharisha kwamba mbinu yoyote ya kupenyeza fedha za ufisadi kwa lengo la kuwaghilibu wapiga kura katika jimbo hilo zitazimwa kwa nguvu ya umma. Kurugenzi ya Habari na Uenezi inapenda kukumbusha kuwa kwa mwelekeo Wabunge waliowengi wa CCM na hali ya ufisadi uliopo nchini, wananchi hawapaswi kwa sababu yoyote ile kuwaongezea mbunge CCM. Hii ni fursa pekee kwa wananchi kuongeza mbunge mwingine wa upinzani bungeni kwa lengo la kutoa fikra mbadala zenye kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa demokrasia na maendeleo ya nchi yetu.

Aidha Kurugenzi ya Habari na Uenezi ingependa kutumia fursa hii pia kutangaza kwamba uchaguzi wa ndani ya chama unaanza Februari Mosi, 2008 kama ilivyotangazwa kwa kuanzia na Uchaguzi katika ngazi ya Msingi ambao utafanyika kwa miezi miwili mpaka tarehe 31 Mwezi Machi 2008. Kwa lengo la kufanikisha uchaguzi huu, Kurugenzi inasambaza rasmi “Maelekezo ya Taratibu za Uendeshaji wa Uchaguzi Ndani ya Chama Ngazi ya Msingi na Tawi”( Nakala za Nyaraka hii inasambazwa pia kwa waandishi wa habari kama sehemu ya taarifa hii). Kurugenzi ya Habari na Uenezi inahimiza umma wa watanzania hususani wanaCHADEMA na wapenzi wa CHADEMA kushiriki kwenye mchakato huu kwa lengo la kujenga oganizesheni ya chama mbadala kuanzia ngazi ya chini kabisa. Pamoja na uchaguzi wa Viongozi wengine wa chama katika ngazi hizo, mabalozi wa CHADEMA ambao ni wawakilishi wa chama katika nyumba kumi watachaguliwa. Mchakato huu utahusisha pia uundaji wa Mabaraza ya chama katika ngazi hizo. Mabaraza hayo ni Baraza la Wazee, Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) na Baraza la Wanawake wa CHADEMA(BAWACHA).

Imetolewa 28 Januari 2008 na;


Erasto K. Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
0713 47 47 07
 
Mpaka Kielewee:
Umefanya kazi nzuri.
Mgombea sasa amepatikana, na kwa vile tayari anao uzoefu wa kugombea nafasi hiyo, atakuwa anajua ni wapi palipokuwa na ugumu safari iliyopita. Kwa hiyo inawezekana amejiandaa vizuri kukabiliana na vikwazo vilivyomzuia asiwe mbunge safari iliyopita. Kazi mhimu ni kutafuta njia za kuwafikia wananchi mapema ili kujua shida zao kubwa, pamoja na kuwataarifu mienendo ya kiutawala inayoendeshwa na serikali iliyopo madarakani wakati huu na jinsi inavyohusikana na kukosekana kwa maendeleo Kiteto.

Mgombea na chama chake wajaribu kutupenyezea ni sehemu zipi wanapohitaji msaada wa hali na mali ili ushindi uweze kupatikana.

Hata kupiga kelele tu ni msaada. Hata mtu wa JF aliye na ndugu yake Kiteto akimshawishi au akimuelimisha 'one-on-one' maovu yanayotendeka leo ili kura hiyo moja ipatikane ni msaada vile vile, wengine watatoa misaada ya kupatikana kwa vipeperushi na maandiko maalum ili wananchi wapate kujisomea, n.k.

Mhusika mkuu ni mgombea mwenyewe na jinsi anavyotaka kuendesha kampeni yake.
 
Naona niwapatie majina ya kata pamoja na idadi ya waliojiandikisha kupiga kura kama ifuatavyo;

1.Bwagamoyo 3276,
2.Dongo 6717.
3.Dosidosi 2715.
4.Engusero 7791.
5.Kibaya 3092.
6.Kijungu 3233.
7.Lengatei 3283.
8.Makame 2490.
9.Matui 10677.
10.Ndendo 1587.
11.Njoro 4687.
12.Olboloti 2828.
13.Partimbo 10077.
14.Songambele 5794.
15.Sunya 6311.

Asante sana ndugu yangu hii itatusaidia kujua kama watafanya kale ka-mchezo ka kina Kivuitu na KEC...
 
CHADEMA mafanikio mema huko Kiteto.

Ila ningelikuwa mimi kiongozi wa CHADEMA hilo jina lingetangazwa na mkutano
wa hao viongozi wa vyama vinne kwa pamoja na hata ratiba nzima ingejenga kwenye huo umoja zaidi.

Lakini akili ni nywele kila mtu ana zake, huenda wameona hiyo njia ndio inafaa, japo mimi naona kama wanakosea.
 
Tatizo la Chadema ni pupa, jazba na papara. I hope and wish wataangukia pua....
 
Kama Mungu angekuwa anasikia dua kama hizi, wengi wetu humu nadhani tungekuwa ahera madukani!
 
Wanajibaraguza tu hawana chao, wanajua kabisa hawawezi kushinda. Sasa hivi wanapanga mikakati ya kuiba uchaguzi huo, lakini tutakula nao sahani moja kuhakikisha hawafanikiwi na ujambazi wao.
 
mpaka kieleweke Re: Uchaguzi wa Kiteto:

Naona niwapatie majina ya kata pamoja na idadi ya waliojiandikisha kupiga kura kama ifuatavyo;

1.Bwagamoyo 3276,
2.Dongo 6717.
3.Dosidosi 2715.
4.Engusero 7791.
5.Kibaya 3092.
6.Kijungu 3233.
7.Lengatei 3283.
8.Makame 2490.
9.Matui 10677.
10.Ndendo 1587.
11.Njoro 4687.
12.Olboloti 2828.
13.Partimbo 10077.
14.Songambele 5794.
15.Sunya 6311.


Masatu,

Tatizo la Chadema ni pupa, jazba na papara. I hope and wish wataangukia pua....

Loh! Masikini ya Mungu! Yaaani kwenye uongo ukweli hujitenga, kweli akili ni nywele!


Mkuu Kieleweke,

Salute! Endelea kutuletea habari muhimu za huko ground zero na tunashukuru kwa hizi dataz na ubarikiwe!
 
........... naona ngoja sasa nibookmark thread hii; ina mavituz kweli kweli.
 
Kuna mambo muhimu yanazidi kuja.. na wengine mkipata nafasi google na play with your search engine, and tell us something about Kiteto, something we do not know yet.
 
CCM waanze kampeni zao kwanza. Kwa taarifa ya Dr. Slaa kutoka Karatu, vyama vya upinzani vikiongozwa na Dk. Slaa watakuwa Kiteto tarehe 9 na 10 Februari. Hapo kitaeleweka!

Wambugani
 
ukweli usiojificha upinzani wanaaangukia sehemu zote tatu.

Tanzania bado upinzani unatuchezea shere.

hapo watajitia kujua na mengi mengine na mtaona
 
Kwa wapenda maendeleo au mabadiliko ya siasa na kisheria bongo, baada ya yaliyofanyika Kenya tunaombea uchaguzi wa haki na huru, otherwise sidhani kama kuna anything tofauti kinaweza kutokea, unless upinzani wakishinda symbolically ni a big plus,

Lakin cha msingi tunachoombea huko ni amani, na respect kwa sheria zetu.
 
ukweli usiojificha upinzani wanaaangukia sehemu zote tatu.

Tanzania bado upinzani unatuchezea shere.

hapo watajitia kujua na mengi mengine na mtaona

Mtu wa Pwani,

Huoni kwamba sasa upinzani kunaanza kuwa na mabadiliko? Hayatoshi lakini
angalau wengine tunaanza kuona mambo ambayo yanafurahisha roho zetu. Cha kuombea ni watu kama akina Dr. Slaa na Zitto waongezeke sana.

Pia ni kuombea upinzani wakae chini na kuangalia hasa ni kwanini wanashindwa? System iliyopo ya CCM kutumia pesa na vyombo vya dola haitabadilika, lazima wajifunze kushindana kwenye mazingira hayo hayo magumu.

Nakubaliana na wewe kwamba bado kuna safari ndefu lakini pia muhimu ni kwamba sasa japo gari limeondoka kwahiyo litafika ili mradi halidondoki huko njiani.

Ninaamini wanaweza kushinda majimbo mawili kati ya hayo matatu.

Uwingi wa wabunge wa CCM bungeni ni balaa kwa taifa. Ni kuombea 2010 hiyo tofauti iwe ndogo sana.
 
CCM waanze kampeni zao kwanza. Kwa taarifa ya Dr. Slaa kutoka Karatu, vyama vya upinzani vikiongozwa na Dk. Slaa watakuwa Kiteto tarehe 9 na 10 Februari. Hapo kitaeleweka!

Wambugani[/QUOTE

SITAKI KUWAKATISHA TAMAA BALI NDIO UKWELI HAKUNA NAMNA CHADEMA ITASHINDA UCHAGUZI KULE,INGAWA WANA MGOMBEA AMBAE NAMUHESHIMU SANA KAMA BABA YANGU HASA NIKIKUMBUKA ENZI ZILE NIKICHEZA NA NASERIAN KIMESERA ,MTOTO WAKE MTAA WA MKADINI OBEY.HUYU MZEE WANGU HAUZIKI KULE NA AMEGOMBEA KILA UCHAGUZI BILA KUKOSA TANGU VYAMA VINGI VIANZE,LABDA APEWE KURA ZA HURUMA
 
Cha kuombea ni watu kama akina Dr. Slaa na Zitto waongezeke sana.

Mkuu heshima mbele, hapa wa kumuongezea ni Freeman, Lisu bado sijampitisha kama ni pure, so far ninawaaminia the big three Zitto, Dr. Slaaa, na Freeman, wasichoke maana taifa letu liko njia panda! Na huko upinzani kuna kondooo wengi waliovaa ngozi tu, kwa hiyo tuna kaaazi kweli kweli!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom