Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA inatarajia kukutana kesho jumamosi Januari26.2008 chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Kamati kuu itafanyika jijini Dar es Salaam ambapo pamoja mambo mengine itajadili na kupitisha jina la mgombea ubunge jimbo la Kiteto kupitia CHADEMA.

Imetolewa na;

Erasto K. Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
0713 47 47 07
Januari 25, 2008
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,776
2,000
Wasifanye makosa yale ya awali kuharakisha kuteua wa kwao. Kwa vile sasa kuna ushirikiano wa vile vyama vinne,basi wakae pamoja wapange nini cha kufanya ili CCM iangukie pua huko Kiteto.
 
Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA inatarajia kukutana kesho jumamosi Januari26.2008 chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Kamati kuu itafanyika jijini Dar es Salaam ambapo pamoja mambo mengine itajadili na kupitisha jina la mgombea ubunge jimbo la Kiteto kupitia CHADEMA.

Imetolewa na;

Erasto K. Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
0713 47 47 07
Januari 25, 2008

Kazi unaiweza mkuu....
 
NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
560
195
Kazi ipo!!!!!!!!!!
CCM leo kuteua mgombea ubunge Kiteto
na Tamali VulluKAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inakutana leo kwa mkutano wa siku moja ambao pia utateua jina la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Kiteto.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho jana ilisema kuwa mkutano huo maalumu utafanyika chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi, John Chligati, alisema kuwa agenda kubwa itakayoshughulikiwa katika mkutano huo ni kujadili na kufanya maamuzi kuhusu mapendekezo ya Wana CCM walioomba kugombea nafasi ya ubunge kupitia chama hicho.

Wanachama waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Paulo Lemunyo, AIi Juma Lugendo, Benedict Ngarama Ole Nangoro, Dann Meng'orick Mollel, Meshark Ole Lutikise na Luteni Lepilal Ole Moleiment.

Chiligati alisema katika kura za maoni zilizopigwa jana, Nangoro aliongoza kwa kupata kura 384, akifuatiwa na Mollel (193), Lugendo (105), Lemunyo (97), Lutikise (50) na Moleiment (37). Jumla ya kura zilizopigwa ni 869 na kura tatu ziliharibika.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Februari 24 mwaka huu.

NEC ilitangaza kuwa siku ya uteuzi ni Junuari 29 na kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 30 hadi Februari 23 mwaka huu.

Jimbo la Kiteto lipo wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Benedict Losurutia, kichotokea Desemba 16 mwaka jana.
 
Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Luteni Lepilal Ole Moleiment

Huyu bado yupo tu? Lazima atachukua nafasi ya mgombea wa CCM.
 
Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,408
2,000
Out of topic, samahani.

ngomanzito.... avatar yako kiboko ndugu wewe!! lol
 
Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,776
1,195
Wasifanye makosa yale ya awali kuharakisha kuteua wa kwao. Kwa vile sasa kuna ushirikiano wa vile vyama vinne,basi wakae pamoja wapange nini cha kufanya ili CCM iangukie pua huko Kiteto.

Nakuabaliana nawewe, hapa wasifanye kosa la jinai..
Ndo pa kushikamana haswa kuwangoa mafisadi!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
Hivi tunaijua Kiteto vipi? Nani ana habari za kiteto ambazo zinaweza kuwa issue kwenye uchaguzi huu?
 
Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,137
1,500
Sasa inabidi wagombea kama wanataka misaada yetu tulio mbali waingie kwenye hii Tech waweke CV na sera zao na kujinadi through web na watuombe michango tutawachangia kama wana make sense.
 
Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,137
1,500
Hivi tunaijua Kiteto vipi? Nani ana habari za kiteto ambazo zinaweza kuwa issue kwenye uchaguzi huu?

nakuaminia mkuu najua utaweka mtu live kutuletea mambo moja kwa moja kutoka jikoni,najua ni will tuu ya kufanya hivyo maana technology ipo tayari tena cheap sana
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,614
2,000
Mzee Mh Mwanakijiji.
Salaam!Ni wazi kwamba u mzima wa afya.
Sasa mimi huwa nakuja kuchangia kwenye thread zako..mimi nimeposti ya kwangu kuhusu kushinikiza serikali yetu iwajibike.Naelewa kwamba ulibadili msimamo wako mara baada ya kumhoji Mama MeghjiHowever mchango wako bado unahitajika kwenye mada hii muhimu kupita kiasi kwenye historia ya nchi yetu hii changa tunayoujaribu kuijenga huku wengine wakiisambaratisha.Au hauoni umuhimu?Tafadhali changia mawazo na usisahau slogan yako ninayoipenda ya "hoja hujibiwa kwa hoja"
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
hey.. yamekuwa haya? haya ngoja niangalie.. basi tatizo siwezi kusoma thread zote na kuchangia zote hata kama ninapenda ila kwa vile umeniambia ni muhimu mno basi ngoja niangalie... Ila ungeni PM tu ingetosha.
 
Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
873
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA inatarajia kukutana kesho jumamosi Januari26.2008 chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Kamati kuu itafanyika jijini Dar es Salaam ambapo pamoja mambo mengine itajadili na kupitisha jina la mgombea ubunge jimbo la Kiteto kupitia CHADEMA.

Imetolewa na;

Erasto K. Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
0713 47 47 07
Januari 25, 2008

Pengine linaweza kuwa ni swala la mchango wa mawazo tu, na hakuna mahali popote sasa hivi palipo na mchango mahsusi zaidi kuliko palivyo JF.

Ni kwa msingi huo basi, wapinzani ambao wanajulikana kuwa ni washiriki wakubwa katika ukumbi huu wangechukua nafasi ya kuwashirikisha wenzao hapa JF walio na tamaa ya kuuona upinzani nao unaongeza nguvu bungeni kwa kupata ushindi katika kinyang'anyiro hiki. Si lazima watoe siri za mbinu zao zote kama wanazo ili zisinyakuliwe na wana ccm wanaopitia hapa; lakini nina hakika wakiweza kupenyeza baadhi ya mambo mhimu wanayohitaji yatendeke katika uchaguzi huu ili yajadiliwe, wanaweza wakapata mchango mhimu sana kutoka hapa. Hata mchango wa hali na mali inawezekana pia wapo wanaJF wanaoweza wakajitolea.

Jameni, leteni mada za mipangilio yenu ya kupata ushindi Kiteto tuijadili hapa kungali mapema.

Mimi nipo tayari kujitolea gharama za kudurufu? (kopi) za makala muhimu zinazopitia humu JF ili zisambazwe kwa wananchi na wapiga kura wa Kiteto. Wanchi wanatakiwa wayajue yanayofanywa na watawala wetu kwa mapana na marefu sasa, wasibaki kusikia Kasi, nguvu na ....Mpya zisizotupeleka popote. Tumechoka.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,668
0
Habari za ground zero ni kwamba Kiteto, ni po-CCM kwa hiyo CCM itashinda kwa kishindo, lakini CCM haiwezi kushinda Biharamulo, kwa hiyo strategically, upinazni wanahitaji kuwa makini na ku-invest Biharamulo ili wasiishie kukosa majimbo yote matatu, maana Tyson ambaye anasadikiwa kuwa in line kuwa the next PM, hawezi kukubali kuiachia Mwibara, maana CCM walimrubuni kwa shughuli kama hizi,

Upinzani wanahitaji kuwa makini kwenye hizi chaguzi tatu, na kukubali ukweli inapobidi maana ndio hasa maana ya national politics anyways.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,587

(1) Nadhani hauko serious kuhusu the next PM.

(2) Sidhani kama atasaidia kuirudisha Mwibara kwa CCM; uhusiano wake na wajitta/wakerewe umekuwa wa kuyumba yumba sana tangu alipomaliza Ubunge wa Mwibara mwaka 1975. Kama CCM wanaitaka Mwibara ni afadhali wamtumie sana Mzee Msekwa pale kuliko hawa longolongo wengine.
 
Mr EWA

JF-Expert Member
Mar 15, 2007
332
225
Nafikiri cha maana hapa ni ushindani kuteuwa mtu makini kutoka chama chochote na kuendeleza mshikamano na si kila chama kutaka mtu wao.
 
Chiluba

Member
Nov 8, 2007
51
70
Hivi tunaijua Kiteto vipi? Nani ana habari za kiteto ambazo zinaweza kuwa issue kwenye uchaguzi huu?

Kwa kifupi issue kubwa kiteto ni miundombinu.Kiteto ipo ktk mkoa mpya wa Manyara,lakini hadi sasa hakuna mawasiliano ya barabara ya moja kwa moja kati ya Kiteto na Makao makuu ya mkoa yaani Babati..lazima upitie Arusha au Kondoa Dodoma! Usafiri wa basi kiteto- Arusha upo mara mbili au tatu tu kwa wiki..Ni rahisi kwa mwananchi wa kiteto kwenda Dodoma au Dar es salaam kuliko kwenda makao makuu ya mkoa wake!

Kutokana na hili huduma nyingi muhimu kiteto wanazipata kutokea arusha au Dodoma..ahadi ya barabara ya moja kwa moja kiteto-babati huwa inatolewa kipindi cha uchaguzi tuuu..

Jambo lingine Kiteto ni migogoro ya ardhi,kuna mashamba makubwa ambayo yamevamiwa kunyemela na wenye pesa zao toka dar na Dodoma kwa ajili ya kilimo...mwaka jana kulitoke vurugu hadi polisi walipigwa na gari lao kuharibiwa sana na wananchi ktk eneo hilo lenye mgogoro.

inasemekana kuna kigogo anataka kuwahamisha wananchi ktk eneo hilo kwa visingizio vingi,lakini inasemakana wanataka kuanzisha ranch kubwa ktk eneo hilo.

KWA UELEWA WANGU HIZO NDIO ISSUES KUBWA...
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom