Uchaguzi una kushinda na kushindwa...

Uchaguzi una kushinda na kushindwa...

attachment.php


Hodi hodi naingia jamvini, malenga mnipokee
Ujumbe wangu kumpelekea, meneja uchaguzi CCM
Umfikie aliko, akiomboleza chama chake kushindwa uchaguzi
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Uchaguzi ndivyo ulivyo, kuna mshindi na mshindwa
CCM mlijiamini, tena mno kupita kiasi
Badala ya kutangaza sera, mkawatumia wajeshi
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Mkawatisha wananchi, kwa mitutu na mabomu
Hofu kuu ilitanda, Jiji la Arusha likazizima
Wakazi wakakimbizwa, vijana kukamatwa
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Ikawadia siku ya uchaguzi, wakapiga wachache mno
Ukweli ukabainika, wengi waliopiga ni wana-CCM
Wana-CCM hao wakaamua, CHADEMA kuichagua
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Kumbe mlipowapiga CHADEMA, wana-CCM nao walichoka
Ahadi kedekede mlitoa, chache sana mlitimiza
Hali ikawa mbaya, vijana kukosa ajira
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Mkatangaza mikopo, kwa akinamama na vijana
Kumbe mliwaandaa, maswahiba zenu kuwapa
Wananchi wakabaini, mkenge kuingizwa
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Tamati najongea, malenga nahitimisha
Najua hamu bado mnayo, shairi hili kulisoma
Japokuwa vina halina, bado laitwa shairi
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Natumai mmejifunza, wananchi kutowadharau
Mabomu kutowapiga, bure bilashi kuwaua
Mnapovunja haki zao, mwawatakia nini
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo
 

Attachments

  • mwigulu akiomboleza.jpg
    mwigulu akiomboleza.jpg
    39.5 KB · Views: 883
Mwigulu umetumia pesa nyingi za ccm kuhonga matokeo yake mmeshindwa uchaguzi...poleni sana...chadema hongereni sana :majani7:
 
hivi huyo hapo pembeni ya mwigulu ni nani kwa upande wa kushoto?
 
Usiomboleze sana mwigulu kura ndiyo msema kweli, na mimi naongezea..machache kukueleza...achana na siasa za majitaka..unazidi kuiangamiza ccm...siasa si uadui, siasa ni mshikamano ili tuijenge nchi...Tanzania hatukuwa na ubaguzi, udini na ukabila...na wewe mwigulu..unatangaza ubaguzi , udini na ukabila.pia achana na rushwa, kwani ni adui wa haki.bila kusahau kubambika watu kesi za ugaidi na uongo.naweka kalamu chini..machache kwa leo yatosha.Usiomboleze sana mwigulu...uchaguzi ndivyo ulivyo!
 
aiseeeee babayangu mbona simuoni shonza na yule jamaa anayetembea na mwigulu aliemwagiwa tindikali nao wamekula mita ha ha ha ha ha
 
aiseeeee babayangu mbona simuoni shonza na yule jamaa anayetembea na mwigulu aliemwagiwa tindikali nao wamekula mita ha ha ha ha ha

Huogopi matusi..!?? jamaa anatukana hadi basi..
 
Huyu apunguze ukatili, atapata presure. Anahitaji counselling ya mchungaji wake.
 
hahahaha.nimecheka sana aise.kidogo ni spirt uji wa pilipili niliopewa na jirani yangu baba khalfan.
 
Ccm imefanya maisha kuwa magumu vijana kupata kazi nivigumu arusha imewahukumu
ccm ni wahujumu wananch kuwalaumu
usiomboleze sana mwigulu... uchaguzi ndivyo ulivyo!
 
Gharama kubwa sana hizi za chaguzi ndogo KATIBA MPYA haitatusaidia? Kuna shule za msingi nyingi tu kwenye Jiji hili la Arusha watoto wanakaa chini sakafu isiyo hata simenti lakini uliza gharama walizotumia wafuatao:
-Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
-CCM;
-CHADEMA;
-Wagombea wenyewe.
Tutagharamia SIASA kwa mtindo huu hadi lini? Tumeanza uchaguzi huu tangu mwaka 2010 hadi leo tunaendelea kuchaguana!
Afrika tunawekeza kwenye siasa wnzetu wa dunia nyingine wanawekeza kwenye elimu mkuu .
 
Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandsaae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mambo yote yamekwenda sawa).


kumbe unalijua hilo leo saa nyingine unakuwa na akili timamu,kwa hiyo wakati mwingine huwa unajitoa akili au ndio ukiwa CCM hata akili za ziada huondoka nazo?
 
Safi sana Bwana Nape kwa Kuongea vizuri. Lakini napenda nikushauri. Tafadhali mwambieni Mwigulu kuwa aache kutuharibia chama chetu cha CCM. He is too much obsessed now with CHADEMA. CDM sasa hivi imepata umaarufu kwa sababu ya vituko na hila za Mwigulu dhidi ya CDM. Afanye siasa za kisomi kama anavyotamba kwamba yeye ni msomi. Ni kweli tulikuwa naye mlimani mimi nikiwa sayansi na yeye akiwa political science. Anajenga chuki dhidi ya wananchi. Tanzania bado hatujafika hatua ya kutishiana na vikundi vya mgambo kama ambavyo ccm na cdm wameanza. Mungu ibariki nchi yetu, Mungu ibariki CDM na CCM.
wewe futa hapo pekundu, hawa wanafaa kulaniwa milele
 
Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mambo yote yamekwenda sawa).

Natamani kauli hii mngekua mnatoa baada ya uchaguzi mkuu (kama mambo yote yamekwenda sawa)
Sasa hv ni rahisi kusema hvyo kwa sababu huu ulikua uchaguzi mdogo wa udiwani. Nakusibiri '15 uje na hii kauli baada ya uchaguzi (kama uchaguzi utakuwa huru na haki kweli na kama hakutakuwa na wizi wa kura na fujo za kubambika)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Na wale mliowaua Arusha kwa bomu yatawatokea puani muda si mrefu utapelekwa apolo kama baba yako mwandosya

Tujitahidi kuheshimiana hata kama tunatofautiana ktk itikadi zetu za kisiasa.
 
Back
Top Bottom