kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,940
- 7,847
Mambo yote yalikwenda sawa bila shaka.... Nilidhani ungewapongeza cdm kwa ushindi mnono. Roho inauma lakini usijali sana. Japo mmepoteza nguvu na mali nyingi nyinyi hela mnazo kibao sijui mnapata wapi. Mmeweza kununua kila kitu ila mioyo ya watu. Mioyo ya watu haina thamani. Utawala mbaya (bad governance), mbinu na mikakati chafu kwenye siasa na uchaguzi itawatafuna hadi kwisha kwenu. Dhambi kubwa ya ccm (chama cha mwalimu nyerere) ni kula meza moja na mafisadi wa kibepari. Kwa sasa wamekiteka chama kilichokua cha wavuja jasho. Inafaa alama ya jembe na nyundo mfute kwenye bendera maana haina tena maana.Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mambo yote yamekwenda sawa).