Uchaguzi Umeisha! Sasa ni makali ya Mgao wa Umeme KULIKONI?

mimi nipo dar tena kwenye moyo wa darisalama na wala sijaona huo mgao na sishangai Tanzania Daima kuandika hizo habari maana nawajua wamiliki wake na huo utakuwa ni mwendelezo wa propaganda zao..........

Note*

Katizo la umeme kwa muda wa saa limoja au mawili mara moja kwa wiki au wiki mbili kwa baadhi ya sehemu huwezi kuita mgao wa umeme.
wewe unamatatizo upo dar ipi?? hata mgao wa umeme huoni?? niambie upo dar maeneo gani mkuu!
 
jamani more than 2 wks umeme tunakatiwa kuanzia saa 12 jioni mpk asubuhi cjui ni mgao kama kuna mwenye taarifa anisaidie
 
Ndugu hapa hakuna wakujb hilo. Labda ndo maisha bora kwa kila Mtz. Tunaburuzwa na hakuna wakututetea. Bora wangetoa taarifa kuwa kuna tatizo ili tujue tutakavyokabiliana nalo.
 
tutamkumbuka lowassa sana sababu hakutaka hii maneno itokee. i wish angekuwa pm hadi leo tusingekuwa na mgao wala bibi yake mgao.
 
Uchaguzi si umeshaisha? mtakoma kujipendekeza kuichagua sisemi hilo mnalo,na kwa taarifa yenu ni mgao kwa kwenda mbele mpaka mvua inyeshee,ila lowasa alikuwa na mipango mizuri sana ila wasidizi wake ndo waliomwekea kitumbua chake mchanga,leo hii hili tatizo tusingeliona
 
Na hii nn baada ya tu ya uchaguzi.........unajua kabla ya uchaguzi huwezi kuona uozo au upumbavu na uzembe kama huu.......kikwete anataka kutengeneza dili lingine kama lile la richmond si unajua kikwete,lowasa,rostamu....walikuwa na nia ya kulinyonya taifa kupitia richmond lakini waliandamwa kabla hawajatimiza malengo?....nasikia walikuwa na mipango kibao feki kwa ajili ya kuliangamiza taifa hili....sasa kikwete sijui saaizi anakuja na style gani ya kuliibia taifa....kaanza kwa kuwagawa watz kwa kuleta udini serikalini.......ole wake?! Tunamuona kwa macho yetu yote na tunamsikia sana
 
tutamkumbuka lowassa sana sababu hakutaka hii maneno itokee. i wish angekuwa pm hadi leo tusingekuwa na mgao wala bibi yake mgao.

wanamchukia lowasa ila mie naamini lowasa kabeba tuhuma za wenzake, na hata kama aliiba bado alifanya kazi inayo onekana, leo hii watu wa kahama na shinyanga wanamkumbuka sana lowasa kwakuwafanya waishi maisha ya raha wakipata maji safi na salama. hata umeme alifanya upatikane kwakutunza vyanzo vya mto ruhaha
 
tutamkumbuka lowassa sana sababu hakutaka hii maneno itokee. i wish angekuwa pm hadi leo tusingekuwa na mgao wala bibi yake mgao.

Mbinu za Lowassa hazikuwa sahihi kama mkakati wa muda mrefu. Zilikuwa za kutatua tatizo la umeme wa muda mfupi na zilikuwa za gharama sana, na kikubwa zaidi zilijaa ujanja mwingi wa kiulaji.
Mkakati wa kudumu wa tatizo la umeme TZ si kutafuta majenereta ya kutumia diesel au gas, ni kufua umeme toka mto rufiji kule stiglers gorge wenyewe wanapaita stigo. Palishapimwa na uwezo wake unajulikana. Panaweza kuzalisha umeme wa kuuza hata nchi zingine lakini ubinafsi wa viongozi ndio ulifanya ikajengwa mtera badala ya stigo. Umeme wa diesel na gas kwa eneo kubwa unapaswa kuwa ni wa dharura tu
 
Jamani najaribu kutafuta jibu lakini sipati tokea kumalizika kwa uchaguzi sasa hivi ni makali ya mgao wa umeme tena sasa hivi mgao huu wa ni wa kuanzia saa tisa za mchana hadi kunakucha kulikoni? Mbona wakati kampeni zikiendelea hadi uchaguzi kuisha na Raisi na wabunge tukawapata hali hii haikuwepo kulikoni? Halafu chakustaajibisha hata tahadhari hatupewi kua kutakua na mgao wa umeme maeneo fulani fulani TANESCO kulikoni? Jamani mbona hatuelewi tena kwenye miji mikubwa mojawapo jiji la Arusha sasa hivi ni siku ya pili! Au tunakomolewa kwakua wananchi wamechukua ridhaa ya kuwapa wapinzani Ubunge jimbo la Arusha? WAKULU kuna mwenye Idea yoyote kuhusu na wengine wenye machungu na mgao wa Umeme????:angry:
 
Mbona cku hizi umeme unakatika maeneo tofauti tofauti kwa muda mrefu aafu kila cku. Je ni mgao wa kisirisiri au ni hitilafu. Wenye nyeti zileteni
 
Hivi rais wetu (kikwete) ni mtu makini kweli? katika hotuba yake ya kuzindua bunge la 10 la jamuhuri ya muungano wa tanzania alituambia, moja kati ya mafanikio aliyopata katika awamu ya kwanza ya uongozi wake ni kuondoa tatizo la mgao wa umeme....hii ni aibu kubwa kwani sijui hizi takwimu zake na maneno yake yana uhalisia kiasi gani? Leo hiii dar kila mahali ukipita ni kero za makelele ya generators si mchana wala usiku....tatizo hili la mgao wa umeme tanzania mpaka lini?????????
 
Nilidokezewa kuwa CCM walichota pesa nyingi hivyo zile generators za mafuta pale Ubungo zimekata umeme. Hakuna pesa ya mafuta. Wanafanya load-shedding kwani matumizi yamezidi uzalishaji! Kila Unit 1 ya dizeli Tanasco wanapata hasara ya TShs 41. Huwa inafidiwa na overcharged Hydro and Gas power. Hydro zimechoka ile mbaya na unajua hatuna utamaduni wa maintenance! Gas hazijawa za kutosha - bado chache.
 
Upuuzi na ujinga tu wa Miafrika. Wewe fikiria hili tatizo la umeme lipo tokea enzi za ukoloni na kila mwaka hujitokeza na huleta usumbufu wa hali ya juu na hukera sana. Lakini mpaka leo hii katika karne ya 21 bado halija[atiwa ufumbuzi. Kama siyo ujinga wetu ni nini sasa? Mbona kwenye nchi za watu hakuna matatizo sugu kama hili? Wao wamewezaje kufumbua matatizo kama haya?
 
Mbinu za Lowassa hazikuwa sahihi kama mkakati wa muda mrefu. Zilikuwa za kutatua tatizo la umeme wa muda mfupi na zilikuwa za gharama sana, na kikubwa zaidi zilijaa ujanja mwingi wa kiulaji.
Mkakati wa kudumu wa tatizo la umeme TZ si kutafuta majenereta ya kutumia diesel au gas, ni kufua umeme toka mto rufiji kule stiglers gorge wenyewe wanapaita stigo. Palishapimwa na uwezo wake unajulikana. Panaweza kuzalisha umeme wa kuuza hata nchi zingine lakini ubinafsi wa viongozi ndio ulifanya ikajengwa mtera badala ya stigo. Umeme wa diesel na gas kwa eneo kubwa unapaswa kuwa ni wa dharura tu



haya sasa kaeni gizani sasa hakuna kulalamika.
 
Naripoti nikiwa maeneo ya tabata Kimanga, Eneo lote hili umeme umekatika mida ya saa nne kasoro kama dakika 15 (2145hrs)

Nahisi ndo mpango wa kuchakachua kura za Segerea

Mlishaambiwa kwamba yale yaliyokuwa yakifanyika katika kipindi kilichopita cha jk sasa yatafanyika kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Wameanza na mgawo wa umeme, wameongeza bei ya mafuta, style hiyo itaendelea kwenye maeneo mengine. Ndiyo raha ya jk. Anatunyonga huku akiendelea kutabasamu.
 
sisi wiki ya tatu hatuna amani wanakata muda wanaotaka na kurudisha na kukata yaani kwa kweli tunaipata uchaguzi umeisha tunalipa tulichopanda ,kwa kweli serikali inadharau sana hata hawajatutahadgarisha jamani nchi hii tunasafari ndefu
 
Back
Top Bottom