Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,777
Bondia anaetulia afungwe kamba mikononi na miguuni si bondia.
Bondia anapigana hadi round ya 11.
Unaelewa implication ya hiki ulichokiandika hapa lakini?
Bondia anaetulia afungwe kamba mikononi na miguuni si bondia.
Bondia anapigana hadi round ya 11.
na tena cku hizi ukishakua na kitambulisho cha taifa hilo garasha lao la kupigia kura wala halina kazi tena,maana ofisi nyingi zinahitaji cha taifa kuliko cha mpiga kura,,au kimojawapo kati ya hivyo,mm cha mpiga kura cjui hata nilipokiweka huko hom na cna mpango wa kukitafuta,,,cha taifa tu kinanitoshelezaKwa Tanzania uchaguzi wa haki bado sana. Kiukweli sioni haja ya kujiandikisha zaidi ya kupata kitambulisho kwa ajili ya shughuli zenye kuhitaji uwepo wa kitambulisho, ila si kwa kupiga kura.
Kwahiyo kumbe wananchi hawaendi kujiandikisha kupiga kura kwasababu hawaoni umuhimu wa vyama vya upinzani? Au umekosea uzi?Write your reply...bado sana kwa tanzania demokrasia ni changa maana sioni umuhimu wa vyama pinzani kama kunauwezekano vingefutwa tuu kikaundwa chama kimoja tu
Dooooh! kumbe hivi sasa siyo kuhamasisha, ni mwendo wa virungu na kutishana, nikulipe mshahara halafu ukatae kujiandikisha kupiga kura.....anyway tutafika tu.Haya kumekucha. Mtaani kwetu difenda kibao na mapolisi wanakamata kila aliiyefungua duka kabla ya saa tano maana iliamriiwa hakuna kufungua biashara na watu waende kujiandikisha. Sasa imekuwa kupiga kura sio haki tena bali wajibu. Na huku kwetu ndo maa unaoongoza Tanzania nzima kwa kususia kujiandikisha kupiga kura dadadeki
Mitaa ya Namanga hapa karibu na polisi oysterbay ukifungua duka tu unao. Nasikia ni amri kutoka juuDooooh! kumbe hivi sasa siyo kuhamasisha, ni mwendo wa virungu na kutishana, nikulipe mshahara halafu ukatae kujiandikisha kupiga kura.....anyway tutafika tu.
SIKU NI KILUDIA KITENDO CHA KWENDA KUPIGA KURA HAPO NITAAMINI KWELI DAWAKatika nchi ya kidemokrasia uchaguzi unafanyika kwa sababu mbili kubwa.
Kwanza, ni kwa ajili ya wananchi kupima na kutoa hukumu juu ya yale yaliyofanywa katika kipindi kilichopita. Wale wanaomaliza muda wao waliingia na ahadi kadha wa kadha. Je, wametimiza ahadi hizo kwa kiasi gani? Je, wapewe muda mwingine wa kumalizia zile ambazo hazikutimizwa? Je, wanastahili Kuelewa nafasi nyingine?
Hivyo, wananchi wanapewa nafasi ya kufanya uamuzi juu ya uongozi na utawala wa maeneo yao. Endapo wananchi wanakubali na kuridhishwa na kilichofanywa basi watawarudisha viongozi waliopita. Na kama ni la, basi watawaingiza madarakani viongozi wengine.
Sababu ya pili ya kufanya uchaguzi katika nchi ya kidemokrasia inatokana na sababu ya kwanza. Nayo ni kutoa hukumu ya kisiasa juu ya chama tawala. Chama kilichopo madarakani kinaweza kudhania kuwa kinastahili kuwepo madarakani. Hata hivyo ni wananchi ndio wanatakiwa kutoa hukumu hiyo kila baada ya muda fulani, kwa Tanzania ni kila baada ya miaka mitano, kwa Marekani ni kila baada ya miaka minne kwa Urais, miaka miwili kwa wawakilishi na sita kwa maseneta.
Lengo la hili la pili ni kutoa nafasi kwa chama mwingine kuja na mwelekeo tofauti na ule wa chama tawala na kuwapa wananchi viongozi wapya nje ya wale wanaomaliza muda wao kutoka chama tawala.
Katika kuhakikisha sababu hizi mbili zinafanikiwa, nchi zenye demokrasia iliyokomaa zimefanya mambo makubwa kadhaa:
1. Kutengeneza na kusimika mfumo wa uchaguzi unaoweka uwezekano wa aliyeko madarakani (incumbent) kushindwa. Mfumo, unahakikisha aliyeko madarakani anaweza kushinda au kushindwa bila dhulma, hadaa, au matumizi ya njia za mkato.
2. Walioko madarakani hawaogopi au kuhofia wapinzani wao walio nje. Kama wanaongoza vizuri na wanatimiza ilani yao, hawahitaji virungu au vurugu kujitangaza. Kazi zao zinajionesha na mafanikio yao yanajipigia panda yenyewe.
3. Ili kuhakikisha kila mtu yuko sawa, nauli zozote au maagizo yoyote yenye kuashiria kutokujiamini au yenye kutaka kuvuruga mfumo wa uchaguzi yatapingwa na kukataliwa. Ukimpa mtu nafasi ya kuchagua vitu vitatu halafu ukamwekea bastola kichwani na kumwambia achague cha kwanza basi kinachofanyika siyo uchaguzi bali uchafuzi wa kidemokrasia! Hakuna uchaguzi mbele ya shurti! Huwezi kuwa huru kuchagua kama familia, mtaa, jamii yako inashikiliwa mateka.
Ni kwa sababu hiyo naamini ukuu wa dhamira na ukweli (the supremacy of conscience and truth) unamtaka mtu kuamua kama anaitaka kushiriki katika uchaguzi au uchafuzi wa kidemokrasia. He, mtu ajiandikishe kupigika kura wakati chama chake hakiko huru kufanya shughuli same za kisiasa? Je, ashikiri huku akijua wasimamizi wamekatazwa kumtangaza mshindi kama akiwa wa chama chá upinzani? Je, ashiriki uchaguzi huku akijua muda yake haitahesabiwa?
Basi katika nchi ya kidemokrasia Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa kinachofanyika ni uchaguzi na siyo uchafuzi, na mfumo ni wa demokrasia na siyo demoghasia na kuwa mwisho wa siku watawala hawageuki kuwa watuwala.

Mzee Mwanakijiji; imebidi niangalie lini uli-post huu uzi. Wewe wa sasa umekuwa tofauti na wewe wa zamani.
Haya; hebu tuambie, kipi kimekusibu hata akili yako ya zamani ikakurudia? Having said that; nakubaliana nawe kwa hiki ulichokiandika. Na ndio maana sitapoteza muda wangu kujiandikisha.
Tunafanya uchaguzi kupima na kuona ni kwa kiasi gani upinzani upo na kama unakubalika/haukubaliki.
Pia tunafanya uchaguzi kuchagua wabunge.
Raisi tunaye na tunamjua.
Muongo mnapiga kura sema lengo lenu kuwafanya wenzenu wasione umuhimu wa kujiandikisha ili mwisho wa siku mpige kura ninyi wenyewe tu. tumewastukia.Kwa Tanzania uchaguzi wa haki bado sana. Kiukweli sioni haja ya kujiandikisha zaidi ya kupata kitambulisho kwa ajili ya shughuli zenye kuhitaji uwepo wa kitambulisho, ila si kwa kupiga kura.
wozaaaaa Takwimu zinaonesha waliojiandikisha mpaka ni asilimia 49% ya watu wenye sifa.Huku mali mali nasikia vijiwe nongwa vyote havina watu.
Mtaani kupo kimya ni mwendo wa doria.
Tunafanya uchaguzi kupima na kuona ni kwa kiasi gani upinzani upo na kama unakubalika/haukubaliki.
Pia tunafanya uchaguzi kuchagua wabunge.
Raisi tunaye na tunamjua.
Inasemekana (sijui kama ni kweli); kwamba CCM inao wanachama hai zaidi ya milioni nane (8 milioni).
Ukichanganya na mashabiki tu wa Chama hicho, pengine idadi yao inaweza kuwa milioni tano (5 mililioni) hivi, na kuna watu ambao hawafungamani na vyama vya siasa, na kundi kubwa la 'takrima' lipo tayari kutumika.
Ukiwachanganya wote hawa kwa pamoja unaweza kutoka na idadi kubwa tu ya wapiga kura, pengine inayokaribia milioni ishirini (20 milioni) na ushee.
CCM inaweza kuwatumia hawa kutafuta uhalali wa ushindi wao kwenye kura, pamoja na kususa kwa wengi ambao walistahili kuwachagua viongozi wanaowataka.
Haya tunayaandika, sio kwa kuwatetea CCM, ni kuuweka tu ukweli wa mambo mbele watu wajue uhalisia wa mambo.
Mabadiliko hayawezi kupatikana kwa kususia uchaguzi pekee. Kazi kubwa inatakiwa kufanyika zaidi ya kutopiga kura tu.