Swali zuri sana kama swali la
Mzee Mwanakijiji . Ni maswali yanayofikirisha.
Naomba niweke sawa kauli zako. Sina uhakika kama watu ''wanaogomea '' kama usemavyo.
Mada nyingi zinazozungumzia hili suala zinazungumzia ''kususia'' kauli isiyo ya kweli.
Wananchi hawajasusia au kugomea uchaguzi.
Wananchi wanatafsiri na kutekeleza kauli za ma-DC, Wakurugenzi na viongozi wote wa chama na serikali isemayo ole wako umtangaze mtu nje ya CCM. DC wa Dodoma alisema hilo ni tatizo lako. Hivyo basi kauli hiyo inatoa tafsiri hii;
1. CCM unasababu gani za kujiandikisha ikiwa una uhakika mgombea wako atatangazwa mshindi?
2. Ukiwa mpinzani unasababu gani za kujiandikisha ikiwa umehakikishiwa mgombea wako hatatangazwa mshindi?
Pengine wananchi wanatafsiri hivyo ! sina uhakika ni maoni tu
Kuhusu swali la pili, kuna kitu kinaitwa '' legal legitimacy'' Kwa maana ya uhalali wa kisheria hata kama mtu atashinda kwa kura 7. Ni halali kwasababu mchakato mzima umekamilika, kura zimepigwa, zimehasabiwa na mshindi katangazwa.
Halafu kuna kitu kinaitwa ''political legitimacy'' yaani uhalali wa kisiasa. Kwamba, kura zimepigwa, zimehesabiwa au kutohesabiwa, mshindi katangazwa.
Huyu ana uhalali wa kisiasa kwasababu kafuata utaratibu mzima hadi kutangazwa hata kama utaratibu huo haukupata ''legal legitimacy''
Kwa taarifa, wanasiasa hawaogopi ''legal legitimacy'' wanaogopa sana ''political legitimacy''
Political legitimacy ndiyo inawapa ''authority to influence''
Wanapiokosa hulazimika kurudi katika mstari wa tafakuri.
Angalia historia ya nchi za dunia hii. Hata viongozi walioingia madarakani kwa nguvu, iwe za kijeshi n.k. au kwa kutumia 'Falme'' bado hubumba bumba ''uchafuzi'' ili wapate political legitimacy.