Mtoto wa nzi
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 10,397
- 19,323
Unafahamu jumla ya wapiga walioiandikisha 2015!!?? .... Ni 23.78M.. Leo uje useme upande wa ccm tu na mazombi yetu tufike 20M !!?? Fuvu lako litakuwa na matege linapitisha upepo.
Uwanyime au uwape uwepo wako, wao hawajali, .........kama hata damu ya asiye mwana CCM haitakiwi kule blood bank, kura ilopigwa kwa mpinzani itahesabiwa kweli?????.. kumbuka pia kumchagua mpinzani ni kum-expose kwenye mauti.Swali linalonitatiza ni moja. Tukishawanyima 'uwepo wetu,' na bado wakajitangaza washindi hata kwa kura 50 zilizopigwa na makada; kwa maana kwao lililo mhimu ni 'ushindi' wa aina yoyote.... ni kipi kitakachoonekana tumefaidika nacho sisi ambao hatukupiga kura kwa kugomea uovu wao?
Sijui kama tuna kundi tena linalojali 'heshima na kuheshimika'.
Ndugu yangu, kama kutangaza tu matokeo sahihi wahusika wanapigwa mkwara, je huo umuhimu wa kukusanya taarifa sahihi na za uhakika utawezekanaje? Ili iweje? Ngoja nikukumbushe kidogo...katika uchaguzi wa mwaka 2015, idadi ya waliodaiwa kujiandikisha kupiga kura walikuwa ni watu 23,254,485. Hata hivyo idadi ya kura alizodaiwa kupata jiwe na kutangazwa mshindi ilikuwa ni 8,882,935 sawa na asilimia 38% ya waliojiandikisha. Hiyo ndio Tanzania...karibu sana nyumbani.Ni muhimu kukusanya taarifa sahihi na za uhakika
Mmm, mzee mwenzangu, kweli unaishi dunia hii! Eti tuwe na data za nini kinaendelea...hapa naomba nikumbushie alichosema Nguruvi3, utawala huu wa kidikteta hauhitaji kura yako kwa sababu ya kufanya maboresho, wanahitaji uwepo wako ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi, oops, mchakato wa uchafuzi!...na hivyo kuwa na data za nini kinaendelea.
Yule mkurugenzi wao mpk leo hajarudishiwa passport yake na takwimu siku hizi lazima uzipeleke NBS ndo wazithibitishe.Huyu Jafo anajiamini nini?.Hivi TWAWEZA bado wapo?
Mmm, mzee mwenzangu, kweli unaishi dunia hii! Eti tuwe na data za nini kinaendelea...hapa naomba nikumbushie alichosema Nguruvi3, utawala huu wa kidikteta hauhitaji kura yako kwa sababu ya kufanya maboresho, wanahitaji uwepo wako ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi, oops, mchakato wa uchafuzi!
Nikweli"Mzee Mwanakijiji, post: 33118308, member: 118"]
Sidhani kama itakuwa shida sana kuunganisha kupungua kwa watu kujiandikisha kupiga kura na hali ya kisiasa nchini. Sasa, watu wanaweza kuandika kwa hisia lakini kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi (facts).
Kiuhalisia hiki ndicho kinapaswa kufanyika, kutafuta 'data'Ni makosa kudhania tu kuwa watu hawajiandikishi kwa kiwango kikubwa kwa sababu moja au nyingine. Ni muhimu kukusanya taarifa sahihi na za uhakika na hivyo kuwa na data za nini kinaendelea.
kwa nn mkuu?kwan mtoa siredi n ccm kindakindaki?naona akili zinaanza kukurudi. waambie mimi na familia yangu sitanyanyua mguu kuenda kupiga kura uchaguzi wa serikali za mtaa wala ule mkuu wa mwakani.
Wakati wengine walikuwa wanalia na kutokubaliana na mfumo mzima wa uchaguzi pamoja na hitaji kuu la uwepo wa tume huru ya uchaguzi mlijitaidi kukosoa kweli na kujinadi kwamba walikuwa wanalialia ..
Wakilalamika polisi kutumika kimabavu kupendelea chama kimoja mliziba masikio kabisa...
Wqnanchi wamekata tamaa. .wanaona hawana haja ya kupiga kura isiyo na thamani
Yet siku ya kupiga kura uwezekano wa risasi kupotea njia upo..
Watu wapo majumbani jichagueni nyie wenyewe na mjitangaze. .
RIP Akwilina.
Shida ni pale wanapotumia hata hela zako za NSSF kujipa mikopo na kutengeneza miradi hewa........Milele ya duniani kama ulivosema... no longer at ease....Wasilielie mazingira ya kuendelea kutawala wameyaweka wao na wataendelea shida ni nn. Sisi tunachapa kazi na watawale hadi milele ya duniani. Sio ile ya Muumba
Tunaweza hata tukaacha kulitumia hilo neno "Demokrasia," badala yake tukaamua maksudi kuheshimu HAKI za watu kuchagua kwa uhuru na utashi wao wenyewe kuwachagua viongozi miongoni mwao wanaotaka wawaongoze.
Mtu anapoporwa haki yake kwa kura yake isihesabike baada ya kupiga kura, mtu huyo ananajisiwa na anayemnyima haki hiyo ni mharifu anayestahili kuadhibiwa.
Kuna watu wanasema wapinzani wanachochea vurugu kwa kuwahimiza wananchi kuhakikisha kwamba kura zao haziibiwi, au mtu ambaye hawakumchagua ndie anatangazwa kuwa mshindi!
Na kuna watu wanashangilia wanaposikia upotoshaji huu. Mharifu ni anayeiba kura. Huyo ndie anayesababisha vurugu na sio wapinzani.
Kinachokosekana sasa ni kumkosa mtu mwenye ushawishi, anayeaminiwa na wengi. Akipatikana mtu kama Dr Martin Luther King Jr, au Mwalimu Kambarage Nyerere, vitisho na mitutu inayotangulizwa mbele kuwatia hofu wananchi itageuzwa na kuelekezwa kwa wahalifu wenyewe.
Nadhani ni swala la muda tu. Taratibu watu wataanza na kugoma kujiandikisha kupiga kura..., na tutaanzia hapo kwenda mbele kama wanaowakandamiiza wenzao hawatajirudi.
Vitisho na ubabe havijawahi kuwa njia za kudumu za kuwanyamazisha watu.
Huna uwezo wa kuelewa tungo hiyo. Wewe endelea kupinga kila kitu.Hujielewi wewe. Bure kabisa.
"maendeleo" usituandikie kilugha chenu.ni mpumbavu tu awezaye kutofautisha siasa na maeneleo
Leo umeongea ukweli una siku nyingi Sana husemi Maneno mazito Kama HayaKatika nchi ya kidemokrasia uchaguzi unafanyika kwa sababu mbili kubwa.
Kwanza, ni kwa ajili ya wananchi kupima na kutoa hukumu juu ya yale yaliyofanywa katika kipindi kilichopita. Wale wanaomaliza muda wao waliingia na ahadi kadha wa kadha. Je, wametimiza ahadi hizo kwa kiasi gani? Je, wapewe muda mwingine wa kumalizia zile ambazo hazikutimizwa? Je, wanastahili Kuelewa nafasi nyingine?
Hivyo, wananchi wanapewa nafasi ya kufanya uamuzi juu ya uongozi na utawala wa maeneo yao. Endapo wananchi wanakubali na kuridhishwa na kilichofanywa basi watawarudisha viongozi waliopita. Na kama ni la, basi watawaingiza madarakani viongozi wengine.
Sababu ya pili ya kufanya uchaguzi katika nchi ya kidemokrasia inatokana na sababu ya kwanza. Nayo ni kutoa hukumu ya kisiasa juu ya chama tawala. Chama kilichopo madarakani kinaweza kudhania kuwa kinastahili kuwepo madarakani. Hata hivyo ni wananchi ndio wanatakiwa kutoa hukumu hiyo kila baada ya muda fulani, kwa Tanzania ni kila baada ya miaka mitano, kwa Marekani ni kila baada ya miaka minne kwa Urais, miaka miwili kwa wawakilishi na sita kwa maseneta.
Lengo la hili la pili ni kutoa nafasi kwa chama mwingine kuja na mwelekeo tofauti na ule wa chama tawala na kuwapa wananchi viongozi wapya nje ya wale wanaomaliza muda wao kutoka chama tawala.
Katika kuhakikisha sababu hizi mbili zinafanikiwa, nchi zenye demokrasia iliyokomaa zimefanya mambo makubwa kadhaa:
1. Kutengeneza na kusimika mfumo wa uchaguzi unaoweka uwezekano wa aliyeko madarakani (incumbent) kushindwa. Mfumo, unahakikisha aliyeko madarakani anaweza kushinda au kushindwa bila dhulma, hadaa, au matumizi ya njia za mkato.
2. Walioko madarakani hawaogopi au kuhofia wapinzani wao walio nje. Kama wanaongoza vizuri na wanatimiza ilani yao, hawahitaji virungu au vurugu kujitangaza. Kazi zao zinajionesha na mafanikio yao yanajipigia panda yenyewe.
3. Ili kuhakikisha kila mtu yuko sawa, nauli zozote au maagizo yoyote yenye kuashiria kutokujiamini au yenye kutaka kuvuruga mfumo wa uchaguzi yatapingwa na kukataliwa. Ukimpa mtu nafasi ya kuchagua vitu vitatu halafu ukamwekea bastola kichwani na kumwambia achague cha kwanza basi kinachofanyika siyo uchaguzi bali uchafuzi wa kidemokrasia! Hakuna uchaguzi mbele ya shurti! Huwezi kuwa huru kuchagua kama familia, mtaa, jamii yako inashikiliwa mateka.
Ni kwa sababu hiyo naamini ukuu wa dhamira na ukweli (the supremacy of conscience and truth) unamtaka mtu kuamua kama anaitaka kushiriki katika uchaguzi au uchafuzi wa kidemokrasia. He, mtu ajiandikishe kupigika kura wakati chama chake hakiko huru kufanya shughuli same za kisiasa? Je, ashikiri huku akijua wasimamizi wamekatazwa kumtangaza mshindi kama akiwa wa chama chá upinzani? Je, ashiriki uchaguzi huku akijua muda yake haitahesabiwa?
Basi katika nchi ya kidemokrasia Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa kinachofanyika ni uchaguzi na siyo uchafuzi, na mfumo ni wa demokrasia na siyo demoghasia na kuwa mwisho wa siku watawala hawageuki kuwa watuwala.