Uchaguzi ni wa nini basi?

Uchaguzi ni wa nini basi?

naona akili zinaanza kukurudi. waambie mimi na familia yangu sitanyanyua mguu kuenda kupiga kura uchaguzi wa serikali za mtaa wala ule mkuu wa mwakani.
Embu search Mada zangu zinazohusu uchaguzi labda utapata ajili kidogo
 
Well said, na huyu Nzee Mwenzangu alichangia sana kumsifia mwamba! Aache unafikii
Haya uliyoandika Watanzania wanayaelewa sana. Ndiyo maana wameamua kutuma ujumbe kwa watawala kuwa maneno na matendo yao hayakubaliki katika nchi ya kidemokrasia. Wamewaachia uchaguzi wao ili wafanye comedy yao ya uchaguzi wenyewe.
 
Kiongozi yule hatakuelewa. Anaamini kabisa kutoka moyoni kwamba demokrasia inachelewesha maendeleo na kwamba yeye, so mwingine, ndo mtume aliyekuja kuleta maendeleo.
 
Sijaona maendeleo Wala uzalendo
Ndio maana mnaambiwa fyatueni ili wapatikane wale wanaoitwa wanyonge au wapiga Kura....mm sitafyatua nitazalisha wawili niyawatengenengeneza Kwa nguvu zote Kisha Kwa vyoyote vile watakuwa watoa maamuzi
Mimi si muumini wa demokrasia halikadhalika Mimi si muumini wa udikteta.

Baada ya kujifanyia tathmin nikajigundua mimi ni muumini wa MAENDELEO na UZALENDO.
 
Embu search Mada zangu zinazohusu uchaguzi labda utapata ajili kidogo
hakuna sababu. lakini ukweli ni kuwa umekuwa ukishadadia utawala huu unaominya demokrasia na sasa na ajabu wanapita mitandaoni wakitumia wakuu wa wilaya na wakuu wa nini sijuwi kuhimiza watu wajiandikishe. uzandiki. sijiandikishi na kura sipigi.
 
Uchaguzi au Uchaguzwiii?

Sijawahi kuona Maana ya Uchaguzi kama kamati kuu pale dodoma watu 2000 tu wanaamua kura za watanzania 50,000,000 ?

Mbaya zaid mwaka 2026 Rais ajaye ataamuliwa na mtu mmoja tu Mwenye Vinasaba vya nchi jiran
Aiseee
 
Mimi si muumini wa demokrasia halikadhalika Mimi si muumini wa udikteta.

Baada ya kujifanyia tathmin nikajigundua mimi ni muumini wa MAENDELEO na UZALENDO.
Kwa hiyo ushauri wako ni upi katika namna ya kuwapata watu wa kusaidia kufanikisha hayo.
 
hakuna sababu. lakini ukweli ni kuwa umekuwa ukishadadia utawala huu unaominya demokrasia na sasa na ajabu wanapita mitandaoni wakitumia wakuu wa wilaya na wakuu wa nini sijuwi kuhimiza watu wajiandikishe. uzandiki. sijiandikishi na kura sipigi.

Mkuu sio kushadadia.
Anahusika asilimia 100.
Huyu ndiye aliyemshawishi Dr. SLAA KUKATAAA JUSHIRIKI UCHAGUXI.

Mpaka kesho nashangaa ni hasa ikikuwa nia yake huwa najiuliza ni Ukatoliki au ni Ulowassa.
 
Kwa hiyo ushauri wako ni upi katika namna ya kuwapata watu wa kusaidia kufanikisha hayo.

Asichojua nikuwa hata kikwete aliambiwa usiondoje.
Mkapa pia aliambiwa usiondoke.
Nyerere hivyohivyo.
Asome signature yangu jibu la nyerere utaliona.

Then utagundua mashabiki wote ni wafaidika wa mfumo.
 
Aisee wananchi nimewakubali sana.

Yaani mmeamua kuususia Uongozi wa Muhimbili uzike maiti ya ndugu yenu, kwa kuwa Uongozi huo unawadai 'mahela' mengi, tena kwa 'vitisho' vingi! Mko sawa kabisa.

Samahani kwa mfano huu ☝ unaoonekana hauendani na uzi, ila unaofikirisha.

NA BADO 2020, HII NI TRELA TU!
 
Muda mrefu utawasikia wakisema kuna watu wanatumiwa na mabeberu kuihujumu nchi na uchaguzi kwasababu nchi imekuwa tajiri inanunua ndege 11 cash, inajenga Stigulaz goji, SGR, vituo vya afya na kutoa elimu bure hivyo wanatuonea wivu
Haya uliyoandika Watanzania wanayaelewa sana. Ndiyo maana wameamua kutuma ujumbe kwa watawala kuwa maneno na matendo yao hayakubaliki katika nchi ya kidemokrasia. Wamewaachia uchaguzi wao ili wafanye comedy yao ya uchaguzi wenyewe.
 
Kwa bongoland uchaguzi wa haki bado sana. Kiukweli sioni haja ya kujiandikisha zaidi ya kupata kitambulisho kwa ajili ya shughuli zenye kuhitaji uwepo wa kitambulisho, ila si kwa kupiga kura.

!
!
Cha Kura Hakina Ishu Siku Hizi. Tafuta Leseni Passport Au Cha Taifa Tu Basi.
 
Bandiko zuri kuhusu hali / mazingira ya demokrasia yasivyo huru na haki kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa.

Hata Waziri wa wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) iliyo chini ya Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya kusimamia, kuratibu na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, Mh. Jafo anaelezea jinsi hali isivyokuwa nzuri wananchi hawajiadikishi. Waziri Suleiman Jafo akisoma ripoti za awali kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya amebainisha mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha inaongoza kwa kuwa na idadi ndogo ya wananchi kujiandikisha. Lakini serikali na mamlaka zinazohusika wanajifanya hawajui sababu wananchi kutojitokeza kwa wingi kujiandikisha.

11 Oktoba 2019
Waziri wa TAMISEMI Mh. Jafo anatoa ripoti ya takwimu zinazoonesha muelekeo wa wananchi kususa uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania ambapo ktk siku anaongea na viongozi wa mikoa na wilaya ni asilimia 20 tu ya wananchi wenye sifa za kupiga kura ndiyo wamejiandikisha Tanzania (Tanganyika ) nzima.

Back
Top Bottom