Uchaguzi ni wa nini basi?

Uchaguzi ni wa nini basi?

Mimi si muumini wa demokrasia halikadhalika Mimi si muumini wa udikteta.
Baada ya kujifanyia tathmin nikajigundua mimi ni muumini wa MAENDELEO na UZALENDO.
Demokrasia ni mfumo unaokutawala, utake usitake.
Meandeleo unayosema yanatokana na mchakato wa demokrasia
Huwezi ukawa mzalendo ikiwa hushiriki katika kupanga na kuamua shughuli za kizalendo.

Hata kusema unapenda maendeleo na Uzalendo dhidi ya Demokrasia tayari umeshatumia demokrasia kuamua hivyo.

Hii hoja ya maendeleo na uzalendo bila demokrasia imepandikizwa vichwani ili watu waimbe na kusahau haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kutoa ''hukumu' dhidi ya wanasiasa kama alivyosema mleta mada.

Kwa mtu mwenye kutumia fuvu lake vizuri, itampa tabu sana kutenga demokrasia, maendeleo na Uzalendo. Hata hivyo, kwa fuvu tikitiki maji anything is possible!
 
Haya yanayoendelea kwenye kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi, yamedhihirisha pasi na shaka kile tunachosema kila siku rais na chama chake hawakubaliki, bali hutisha watu ili waonekane wanakubalika. Haiwezekani useme unakubalika, siasa ufanye mwenyewe ww na chama chako, hujuma ufanyie wapinzani wako, kisha siku ya ukweli wa hiyo hadithi kuwa unakubalika watu hawatokei kupiga kura. Hii inathibitisha wananchi wana uelewa wa kupima mambo, na wanafahamu fika uhuru na demokrasia yao hauporwi kwa sababu ya uwepo wa vitu.
Kuna dhana potofu ya kwamba, wananchi ni majuha hawajui au hawajitambui.
Kuna kusahau kuwa Tanzania ya 1951, 1961, 1981 na 2019 ni tofauti kabisa.

Hili la wananchi kususia kujiandikisha ni ujumbe mzito sana.
Wananchi hawasusii uchaguzi kama tukio , wanasuasia mchakato mzima

Wananchi wanajua kura zao hazina maana, isipokuwa uwepo wao vituo vya kura una maana ya kuhalalisha hujuma dhidi ya kura zao.

Ikiwa wasimamizi wameambiwa wasitangaze mshindani nje ya CCM! kura ina maana gani?

Ikiwa NEC wapo, hawakemei vitendo vya ''dhulma'' kwasababu vinafanywa na wateuzi wao , kura ina maana gani?

Ikiwa NEC wanaruhusu watumishi wao kukimbia ofisi ili wasipokee fomu za wasiowataka, kura ina maana gani?

Ikiwa Polisi wanaimba nyimbo za vyama achilia mbali kusherehekea ushindi wa chama ndani ya Barracks, kura ina maana gani?

Ikiwa DC kaamuriwa ''ole wako' eneo lako lipoteze ushindi, na DC huyu ndiye mkuu wa vyombo vya usalama, kura ina maana gani?

Ikiwa kampeni ni za chama kimoja, kura ina maana gani?

Ukisikia wanasisitiza kuhusu kujiandikisha, si kwamba wanahitaji ushiriki wako katika mchakato wa utawala, la hasha! hawahitaji kura yako kwasababu haiwezi kubadili kilichopangwa.
Wanahitaji uwepo wako ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi!
 
Nchi ya kidemokrasia haiwezi kuwa na watawala, bali huwapata viongozi. Madikteta na wafalme ndio hutawala. Wanademokrasia huchagua watu wachache miongoni mwao wenyewe wawaongoze ili waweze kufikia hali bora zaidi katika nyanja zote za ubinadamu.

Tofauti na wanademokrasia, watawala (madikteta na baadhi ya wafalme) hutaka kutimiza matakwa yao kuliko malengo ya wanaowatawala. Watawala hawa mara zote huanza na kuulinda utawala wao usije ukawaponyoka. Hawa watawala mara nyingi hutumia njia zozote ziwazo kuendesha vitisho na maapizo kuwa wao wamewekwa na Mungu na watatawala milele.

Sote ni mashahidi wa watawala tuliopatiwa na CCM kwa lazima. Tunazidi kushuhudia kila kukicha namna hawa watawala wanavyojaribu kuua vyama mbadala na kuwatisha wanaharakati na waandishi wa habari. Dikteta Magufuli na CCM yake badala ya kuchagua kuwa viongozi, wameamua kuwa watawala na kuwafanya wananchi kama watumwa wao.

Cha ajabu kabisa ni kuwa hata sheria haziheshimiwi. Mahakama haziwezi kutoa hukumu za haki, kila siku ni vitisho, na hofu tupu.
 
Basi katika nchi ya kidemokrasia Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa kinachofanyika ni uchaguzi na siyo uchafuzi, na mfumo ni wa demokrasia na siyo demoghasia na kuwa mwisho wa siku watawala hawageuki kuwa watuwala.
Tunaweza hata tukaacha kulitumia hilo neno "Demokrasia," badala yake tukaamua maksudi kuheshimu HAKI za watu kuchagua kwa uhuru na utashi wao wenyewe kuwachagua viongozi miongoni mwao wanaotaka wawaongoze.

Mtu anapoporwa haki yake kwa kura yake isihesabike baada ya kupiga kura, mtu huyo ananajisiwa na anayemnyima haki hiyo ni mharifu anayestahili kuadhibiwa.

Kuna watu wanasema wapinzani wanachochea vurugu kwa kuwahimiza wananchi kuhakikisha kwamba kura zao haziibiwi, au mtu ambaye hawakumchagua ndie anatangazwa kuwa mshindi!
Na kuna watu wanashangilia wanaposikia upotoshaji huu. Mharifu ni anayeiba kura. Huyo ndie anayesababisha vurugu na sio wapinzani.

Kinachokosekana sasa ni kumkosa mtu mwenye ushawishi, anayeaminiwa na wengi. Akipatikana mtu kama Dr Martin Luther King Jr, au Mwalimu Kambarage Nyerere, vitisho na mitutu inayotangulizwa mbele kuwatia hofu wananchi itageuzwa na kuelekezwa kwa wahalifu wenyewe.

Nadhani ni swala la muda tu. Taratibu watu wataanza na kugoma kujiandikisha kupiga kura..., na tutaanzia hapo kwenda mbele kama wanaowakandamiiza wenzao hawatajirudi.

Vitisho na ubabe havijawahi kuwa njia za kudumu za kuwanyamazisha watu.
 
Uchaguzi au Uchaguzwiii?

Sijawahi kuona Maana ya Uchaguzi kama kamati kuu pale dodoma watu 2000 tu wanaamua kura za watanzania 50,000,000 ?

Mbaya zaid mwaka 2026 Rais ajaye ataamuliwa na mtu mmoja tu Mwenye Vinasaba vya nchi jiran
Mkuu na wewe umeshakata tamaa kiasi.hicho?? kama mti mbichi umekuwa hivyo sisi mti mkavu itakuwaje?
 
Ukisikia wanasisitiza kuhusu kujiandikisha, si kwamba wanahitaji ushiriki wako katika mchakato wa utawala, la hasha! hawahitaji kura yako kwasababu haiwezi kubadili kilichopangwa.
Wanahitaji uwepo wako ili kuhalalisha mchakato wa uchaguzi!
Swali linalonitatiza ni moja. Tukishawanyima 'uwepo wetu,' na bado wakajitangaza washindi hata kwa kura 50 zilizopigwa na makada; kwa maana kwao lililo mhimu ni 'ushindi' wa aina yoyote.... ni kipi kitakachoonekana tumefaidika nacho sisi ambao hatukupiga kura kwa kugomea uovu wao?

Sijui kama tuna kundi tena linalojali 'heshima na kuheshimika'.
 
Kwa muda huo ambao tungekaa foleni huku tukionekana mazuzu na wapita njia, badala yake angalau tutafanikisha kazi moja au mbili zenye tija. Hata kama ni kulima bustani, inshalla ipo siku tutakula mboga za majani.
 
Mkuu, nimesoma mahala humu JF, kwamba kuna pendekezo la 'kuwasomba', nyote! Mtaadhibiwa!
 
Sasa kama rais mwenyewe ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala alishasema wazi kabisa na bila kificho kuwa hatarajii watu anaowateua na kuwalipa mshahara, kuwapa gari na nyumba halafu wanaposimamia uchaguzi wamtangaze mgombea wa upinzani kushinda, Hivi katika mazingira kama hayo ambapo matokeo "yatalazimishwa" kushinda mgombea wa CCM kwa hali yoyote ile, kuna haja gani ya mtu mwenye akili zake timamu kwenda kujiandikisha achilia mbali kupiga kura?????!!!!!
 
Inasemekana (sijui kama ni kweli); kwamba CCM inao wanachama hai zaidi ya milioni nane (8 milioni).
Ukichanganya na mashabiki tu wa Chama hicho, pengine idadi yao inaweza kuwa milioni tano (5 mililioni) hivi, na kuna watu ambao hawafungamani na vyama vya siasa, na kundi kubwa la 'takrima' lipo tayari kutumika.

Ukiwachanganya wote hawa kwa pamoja unaweza kutoka na idadi kubwa tu ya wapiga kura, pengine inayokaribia milioni ishirini (20 milioni) na ushee.

CCM inaweza kuwatumia hawa kutafuta uhalali wa ushindi wao kwenye kura, pamoja na kususa kwa wengi ambao walistahili kuwachagua viongozi wanaowataka.

Haya tunayaandika, sio kwa kuwatetea CCM, ni kuuweka tu ukweli wa mambo mbele watu wajue uhalisia wa mambo.

Mabadiliko hayawezi kupatikana kwa kususia uchaguzi pekee. Kazi kubwa inatakiwa kufanyika zaidi ya kutopiga kura tu.
 
Bandiko zuri kuhusu hali / mazingira ya demokrasia yasivyo huru na haki kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa.

Sidhani kama itakuwa shida sana kuunganisha kupungua kwa watu kujiandikisha kupiga kura na hali ya kisiasa nchini. Sasa, watu wanaweza kuandika kwa hisia lakini kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi (facts). Ni makosa kudhania tu kuwa watu hawajiandikishi kwa kiwango kikubwa kwa sababu moja au nyingine. Ni muhimu kukusanya taarifa sahihi na za uhakika na hivyo kuwa na data za nini kinaendelea.
 
Kama vile haujui kinachoendelea nchin,Unafiki bana.
 
Bandiko zuri kuhusu hali / mazingira ya demokrasia yasivyo huru na haki kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa.

Hata waziri wa wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) iliyo chini ya Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya kusimamia, kuratibu na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, Mh. Jafo anaelezea jinsi hali isivyokuwa nzuri wananchi hawajiadikishi. Waziri Suleiman Jafo akisoma ripoti za awali kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya amebainisha mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha inaongoza kwa kuwa na idadi ndogo ya wananchi kujiandikisha. Lakini serikali na mamlaka zinazohusika wanajifanya hawajui sababu wananchi kutojitokeza kwa wingi kujiandikisha.

11 Oktoba 2019
Waziri wa TAMISEMI Mh. Jafo anatoa ripoti ya takwimu zinazoonesha muelekeo wa wananchi kususa uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania ambapo ktk siku anaongea na viongozi wa mikoa na wilaya ni asilimia 20 tu ya wananchi wenye sifa za kupiga kura ndiyo wamejiandikisha Tanzania (Tanganyika ) nzima.
Huyu Jafo anajiamini nini?.Hivi TWAWEZA bado wapo?
 
Hatari itakuja pale ambapo haki haipatikani katika sanduku la kura, Hivyo Watu wakaamua kutafuta Viongozi kwa njia mbadala,

Lissu amewahi kusema hakuna Kiongozi ambaye ametufudisha thamani ya Utu Kama huyu..

Uchaguzi wa Wabunge waliyounga juhudi ulishatoa picha.. Hata kupoteza Maisha kwa Mwanafunzi Akwilina hakukupewa uzito zaidi ya kunyanyasa Viongozi wa CDM,

Hivi sasa hakuna uchaguzi ni bora liende tu.
Mhe lissu alisema, na pia mhe zitto kabwe kasema, watu wakishidwa kuchagua viongozi wanaowapenda kwa sanduku la kura basi watatumia njia zingine, maombi yangu ni hii taifa letu lisifike hapo, maana damu itawagika, maombi yangu ni huyu jiwe aondoke kwa amani hapo 2020, la si hivyo mungu amuondoe katika dunia hii kabla ya 2020, hatujasahau kina akwillina, azory, ben saa nane na wengine, mungu bariki tz
 
Mm nimejiandiksha tu ili siku ya kupiga kura nichague upinzani ili hv vizee vinavyopita mtaan kununua kura vijue kua tuko baadhi watanzania wenye akili
 
Back
Top Bottom