Habari za masiku Wana-JF,
Samahani sikuwepo ila uchaguzi huku
CCM umepamba moto sana na kazi ni mingi sana! Nimerudi sasa kwa habari motomoto huko
CCM kwenye Uchaguzi Mkuu!
Soma Habari Hapo Chini Kwa Zaidi!!!
Mchuano CCM leo
Kutoka gazeti la 'Wapinzani Wetu' Tanzania,
Na Nasra Abdallah
MBIO za kuwania uongozi ndani ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ngazi ya taifa, mikoa na wilaya zinaanza rasmi leo.
Taarifa ya Katibu Mkuu wa chama hicho,Yussuf Makamba, kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, ilisema fomu za kuwania nafasi hizo zinaanza kutolewa leo hadi Juni 5, ambayo pia itakuwa ndiyo siku ya mwisho kuzirejesha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi za uongozi zitakazogombewa kwa ngazi ya wilaya ni pamoja na mwenyekiti, katibu wa siasa na uenezi na katibu wa uchumi na fedha.
Nafasi nyingine katika ngazi hiyo ya wilaya ni wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa
CCM Taifa, wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya na wajumbe wawili wa mkutano mkuu wa
CCM Mkoa.
Katika ngazi ya mkoa, nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti wa
CCM Mkoa, mjumbe au wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, yaani mmoja kwa mikoa ya Tanzania Bara na wanne kwa mikoa ya Zanzibar.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM Mkoa, wajumbe wawili kutoka kila wilaya ya Tanzania Bara na watano kutoka kila wilaya ya Tanzania Zanzibar, ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Nafasi nyingine katika ngazi ya mkoa ni katibu wa siasa na uenezi wa
CCM mkoa na katibu wa uchumi na fedha wa
CCM wa mkoa.
Katika ngazi ya taifa, nafasi zinazogombewa ni ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, nafasi 85.
Orodha hiyo ya taifa ya viti 85, imegawanyika katika makundi matano, ambayo ni kundi la Bara nafasi 20, kundi la Zanzibar nafasi 20 na kundi la wanawake nafasi 20.
Makundi mengine ambayo kihistoria yamekuwa na mchuano mkali ni kundi la vijana nafasi 15 na kundi la wazazi nafasi 10.
Katika taarifa yake hiyo, Makamba alitoa wito kwa wote wenye sifa za kugombea nafasi hizo kujitokeza kugombea.