Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Looh! kama hizi habari zilizoletwa hapa ndio za jikoni, afadhali kukaa mbali na jiko la namna hiyo.
 
If the kitchen is too hot, si wote tunajua mlango ulipo au? Kuna haja hata ya kumwambia mtu kuwa tunatoka jikoni?

Ni kutoka tuuuu, hiii forum haina babysitters!
 
Siwezi kutoka JF kwasababu sio jikoni, huko jikoni mnakotoa habari za udaku ndiko ambako siko hata tempted kukusogelea.
 
If the kitchen is too hot, si wote tunajua mlango ulipo au? Kuna haja hata ya kumwambia mtu kuwa tunatoka jikoni?

Ni kutoka tuuuu, hiii forum haina babysitters!

Kaka acha ubabe......unaweza kutoa hoja bila ya "mikwala mizito"..

Natin personal...

Idumu heshima ya forum

Tanzanianjema
 
Kama alivyouliza Mh.Rufiji!,kuna vitu vinababaisha hapa.Naomba yeyote mwenye upeo wa Muundo mzima wa vikao vya CCM atuweke sawa!.Nini majukumu na kazi/na namna gani wanachaguliwa wajumbe wa vikao vifuatavyo:

1; Central Committee (CC). - Kamati Kuu Ya Chama.

2; National Executive Committee (NEC)-Halmashauri Kuu Ya Chama.

3; Mkutano Mkuu wa Chama.
 
hivi haya majungu mnapigana yataisha lini,ila vizuri kuambiana ukweli,,haya majungu myaache nyie videbwedo,msituaribie jf yetu,jamani???ila naulizaga hawa mastar wenye ukimwi,...,inakuwaje,mbona wote wanasambaza sioni.hata alie mzima,
 
Gazeti la mwananchi liliandika kuwa Maregesi wa jumuyia ya wazazi amesimamishwa uongozi pamoja na wenzake kama wanne,CCM wakakanusha,baadaye ikatokea kama ilivyoandikwa na Mwananchi,habari hii pia iliandikwa na gazeti la serikali HabariLeo.Majina ambayo yametoka niwanao wania nafasi za NEC.Ridhwani anawania kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM kuwakilisha wilaya ya Bagamoyo.Mangula hayumo Nec kwa sababu yeye anawania umwenyekiti wa CCM Iringa.
Kwenye kapu la watu 20 kazi ipo.Nchimbi hakugombea nafasi ya ujumbe NEC,nadhani aliogopa maana 2002 alipigwa chini.
 
Wakubwa Jamani Hii Ni Ya Kweli Na Kamakweli Vijana Tutaisha..maana Hao Vijana Wote Ni Hatari???jamani Nimeona
Picha Ya Dadayangu Miss Tanzania Amepona Nimeona Picha Ya Shem Wangu Kanumba..loh Jamani,,wapi Tid?
 
Quote:

"Siwezi kutoka JF kwasababu sio jikoni, huko jikoni mnakotoa habari za udaku ndiko ambako siko hata tempted kukusogelea"

Next time usisome udaku no body will care as of now, Just CRYING BABIES!, hakuna maziwa hapa kuna mawe tu Take it or leave it, next time nenda Uhuru na Mzalendo, upate za uhakika zaidi!
 
Siku zote naangalia sana CNN,Lakini kuna mkuu mmoja humu aliniambia nibadilishe kidogo taste, na kuwaangalia FOX kwani ni energetic/dynamic zaidi,kuliko CNN ambao hurudia habari karibu siku nzima.Sikuelewa!!,nilipoanza kuangalia nilikuwa naona habari ni za mitaani mno,hazina uzito na nyingi ni rumours,lakini Muungwana huyo aliniambia kumbuka kuwa Signature ya Fox ni "We Report You Decide".Sasa naona Motto huo wa Fox ndio upo hapa!!.Habari yoyote Ruksa atachuja Msomaji!Naomba nisivamiwe.Huo ni Mtazamo wangu.
 
Quote:

"Siwezi kutoka JF kwasababu sio jikoni, huko jikoni mnakotoa habari za udaku ndiko ambako siko hata tempted kukusogelea"

Next time usisome udaku no body will care as of now, Just CRYING BABIES!, hakuna maziwa hapa kuna mawe tu Take it or leave it, next time nenda Uhuru na Mzalendo, upate za uhakika zaidi!

Du!!! kazi kweli kweli. Lete data, asiyetaka kuziona afumbe macho.
 
Siku zote naangalia sana CNN,Lakini kuna mkuu mmoja humu aliniambia nibadilishe kidogo taste, na kuwaangalia FOX kwani ni energetic/dynamic zaidi,kuliko CNN ambao hurudia habari karibu siku nzima.Sikuelewa!!,nilipoanza kuangalia nilikuwa naona habari ni za mitaani mno,hazina uzito na nyingi ni rumours,lakini Muungwana huyo aliniambia kumbuka kuwa Signature ya Fox ni "We Report You Decide".Sasa naona Motto huo wa Fox ndio upo hapa!!.Habari yoyote Ruksa atachuja Msomaji!Naomba nisivamiwe.Huo ni Mtazamo wangu.

""Habari yoyote ruksa atachuja msomaji!"

Wasomaji wakisha kuwa 'conditioned' kwa kupata habari zilizo pindika mara kwa mara kutoka kwenye source zile zile zenye nyeti hufikia mahala wakawa wanaepa kama waendesha baiskeli kwenye barabara yenye mashimo
 
Wswahili wanasema busara ni pamoja na kunyamza kimyaa sometimes, badala ya kupayuka ovyo,

wakati watu wanaenda Mars huko hewani, sisi bado hapa tunajisifia kuendesha baiskeli na kukwepa mashimo, masikini wa Mungu!
 
Quote:

"Kaka acha ubabe......unaweza kutoa hoja bila ya "mikwala mizito"..

Busara ni pamoja na kunyamaza kimya kwenye usiyoyajua, haya huyajui ni vyema ukanyamaza kama unanyolewa!
 
nnazani tumetoka kwenye mstari, lakini ndio kuwekana sawa.

sasa turudini kwenye issue:

hapa tulielezwa kuwa Ridhwan amegombea NEC mara Mkutano mkuu, mara NEC na Mkutano mkuu watu wanavichanganya.

kuna mmoja aliomba na mimi nnarejea kusisitiza tueleweshwe kazi na uteuzi wa vyombo hivi:

CC CCM

NEC
mkutano mkuu
 
Kwa haraka haraka,

1. Ridhiwani, aligombea ujumbe wa kuiwakilisha Bagamoyo, kwenye Mkutano Wa Halamashauri Kuu ya CCM, Taifa kwa jina la kizungu NEC.

2. NEC = National Executive Commitee, yaani Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ambayo kazi yake ni pamoja na kuishauri kamati kuuu ya CCM, na pia kushughulikia na kuzichambua ishus inazopewa na Kamati kuu ya CCM.

3. Kamati Kuu ya CCM, au Executive Committee pia huitwa Central Committee, ni kikao chenye kauli ya mwisho kuhusu maamuzi mengi ya CCM, lakini pia mwenyekiti wa CCM, anayo power ya kui-overrule kamati hiii na pia Halmashauri kuu, kitu ambacho Mkapa alikuwa akikifanya mara nyingi na kwa makusudi, akitumia ubabe na hii power!

kamati hii ina wajumbe 100!
 
Mkuu unasema kuwa Kamati kuu (CC) ina wajumbe 100,Je Halmashauri kuu(NEC)Ina Wajumbe wangapi?na Nini kazi ya Mkutano Mkuu wa Taifa? ambao ndio nafikiri ni kikao kikubwa cha Chama,Nakumbuka Enzi zile za Kizota na Chimwaga!Natanguliza Shukran kwa ufafanuzi wako wa Mwanzo!.Na Mwenyekiti wa Chama anachaguliwa/Thibitishwa na kikao gani kati ya Hivyo!
 
Komandoo ES

Kabla ya kusahihisha naomba ieleweke kwamba kukosea ni sehemu ya kujifunza, katika hili la Uchaguzi you have got pretty much lots of information right lakini nadhani comment yako ya mwisho inahitajia marekebisho kidogo:

1. Habari ambazo zimeandikwa sehemu zote na kufanyiwa uhakiki na source yake kuwekwa hapa ziliarifu kuwa Ridhiwani Kikwete anagombea nafasi ya uwakilishi wa wilaya ya Bagamoyo katika MKUTANO MKUU wa chama sio NEC [HALMASHAURI KUU], Wagombea wa Mkutano mkuu kwa lugha za kichama wanatamkwa kama wagombea uwakilishi wa wilaya X, wagombea wa Halmashauri hutajwa kama wagombea Ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, hili tulikosoana awali naona mkuu kama vile umerejea kule kule, nadhani tunachanganyana kidogo hapa,

Labda kama una source nyingine lakini mimi niliona hapa:

http://dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=2046


2. Nadhani maelezo yako ya hapa yamekuwa ni kama oversimplification ya kazi za Halmashauri Kuu lakini kimsingi hasa Halmashauri kuu ya CCM kazi zake ni kutoa muongozo wa kisera kwa chama na kuandaa na kupitisha Ilani ya Uchaguzi, katiba ya CCM iliyopo mtandaoni inaonesha kuna jumla ya kazi/majukumu 25! Nadhani maelezo yako yalikuwa ni kujumuisha majukumu yote hayo ingawa kauli yako kama ulivyoitoa haipo kabisa kwenye majukumu ya Halmashauri Kuu.



3. Mheshimiwa hapa kidogo idadi ya wanachama wa Kamati Kuu umeichanganya kidogo, Kamati Kuu ina wajumbe 35 na Halmashauri Kuu ina wajumbe 215 tu. Hii figure ya 100 nadhani ndio zile lapses tulizozungumzia kwenye role ya JF lakini nadhani tuwe makini katika kutoa facts as hizi errors sometimes zinaepukika...

Kwa sasa wajumbe wanaomaliza muda wao hawa hapa:

http://www.ccmtz.org/halmashaurikuu.html

Na Kamati Kuu kama nilivyoandika hapo ina wajumbe 35 ambao wanaingia kwa nafasi zao kutokana na kofia zao nyingine kichama ni hawa hapa kwa sasa:

http://www.ccmtz.org/0kamatikuu.htm

Nadhani hapo Mwawado umepata majibu ya maswali yako hapo juu.Kazi za Mkutano Mkuu Taifa nazo pia ni nyingi ila ndio kama ulivyosema ndio kikao kikubwa zaidi katika chama na kinakutana mara tatu kwa miaka mitano [at least] lakini unaweza kuzipata kazi za mkutano mkuu Taifa kikamilifu hapa:

http://www.ccmtz.org/Katiba_%20ya_ CCM.pdf



Hivyo Komandoo ES Ukifuatilia kwa karibu pia kazi na majukumu ya kamati kuu utaona kuwa ni sawa kabisa kama ulivyosema,

OMBI:
Nisaidie kidogo source ya hizi power za mwenyekiti wa CCM katika ku-overulle maamuzi ya Kamati Kuu, na hakika utaisaidia sana forum kama ukitoa mifano ya kibabe ya Mkapa kwenye Kamati Kuu. Inawezekana ikawa ni nyeti kubwa ''ya jikoni'' nitaelewa ukisema hivyo lakini kwa jinsi ulivyoieleza nadhani inawezekana tukapata chachu kidogo hapa....

Ndimi katika kujaribu kuweka mambo sawa, haya ni maoni binafsi tu katika issue hii ya NEC niliyokuwa nikiifuatilia kwa karibu kama wengine wengi humu....
 
Bw Said kweli sasa unajiandaaa, jitahidi maana Tido kakwaaaaaaaa gwaru pengine ww utakwaa Dola.
 
Back
Top Bottom