Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Yakubu,
Makosa yako kwenye website ya CCM. Wamerudia namba 16 mara mbili na ndio maana imekuja 35 badala ya 36. Lakini hata hivyo bado namba sahihi ni 35 kwasababu Migiro sio mjumbe tena wa kamati kuu ya CCM.

Hiyo list ya Komandoo ES hapo juu ndio balaa kabisa maana bado inasema Mwenyekiti ni Mkapa na katibu mkuu ni Mangula. Hizo ndio habari za jikoni tunazolishwa hapa!!!

1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu John Samwel Malecela - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu

5. Ndugu Jaka Mwambi - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe


8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
13. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
14. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
15. Ndugu Aggrey Mwanri - Mjumbe
16. Dr. Asha - Rose Migiro - Mjumbe
16. Ndugu Samwel Sitta - Mjumbe
17. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
18. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
19. Ndugu Amina Salum Ali - Mjumbe
20. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
21. Ndugu Pindi Chana - Mjumbe
22. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
23. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
24. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
25. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
26. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
27. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
28. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
29. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
30. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
31. Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru - Mjumbe
32. Ndugu Juma Suleiman N'hunga - Mjumbe
33. Ndugu Salim Ahmed Salim - Mjumbe
34. Ndugu Abiud Mugini Maregesi - Mjumbe
35. Ndugu Yussuf Moh'd Yussuf - Mjumbe
 
Quote:

Katika usahihisho wako umesema kuwa, wajumbe wa Kamati Kuu ni 35, ukweli ni kwamba ulikuwa unajaribu kuidanganya hii forum, tena kwa makusudi makubwa, maana wajumbe wa kamati kuu ni 36, kama ninavyoleta uthibiti hapa chini, na hii ni kwa sababu safari hii sikuandika kwa haraka haraka, ila nilikaa chini na kuweka vitu, ukweli ni huu chini:-!

WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (2002-2007)


1. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mwenyekiti
2. Ndugu John Samwel Malecela - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Philip Mangula - Katibu Mkuu
!



Looh! kama hiyo list ndio imetayarishwa baada ya kukaa chini na kuweka vitu chini, kuna kazi mwaka huu. Mkapa na Mangula wanatafuta nini hapo juu?
 
Quote:

"Evidence based arguments- Ila real life arguments are a function of values and facts or values only!"

Mzee Mzalendohalisi, pole pole mkuu, wengine shule tulisoma zamani mkuu! damn!
 
Mimi naona huu mjadala si mkubwa sana. Ila kama ni hivyo basi, idadi sawa ni 33, kwa maana ya kwamba Amina Salum Ali, ambaye sasa ni Balozi wa Umoja wa Afrika kule Washington, na Abihud Maregesi, aliyekuwa Mjumbe kwa nafasi yake ya Chair wa Jumuiya ya Wazazi, ambaye sasa amesimamishwa, sio wajumbe tena.
 
Mugongo Mugongo,

Uko sahihi, huenda idadi kwasasa ni chini ya hiyo 35. Matatizo ni CCM kushindwa kurekebisha taarifa zao ontime.
 
"WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (2002-2007)"

Wazee mambo mengine hayahitaji kwenda hata shule, wajumbe waliotajwa hapo kwenye hiyo list, ujumbe wao unaisha pale tu uchaguzi mkuu wa CCM utakapofanyika mwisho wa mwaka huu, yaani 2007, kwa hiyo hata wakiwa nje au ndani ya nchi bado nchi bado ni wajumbe active, wa kamati hiyo hata kama hawahudhuriii, na wanaweza kuhudhiria wakitaka at anytime,

Mkapa, ni mjumbe wa kudumu wa kamati hiyo kutokana na kuwa ex-mwenyekiti wa CCM, kama Mwinyi, katiba ya CCM inasema any ex chairman na veep, ni wajumbe wa kudumu wa kamati kuu, Mangula ujumbe wake unaisha tu baada ya uchaguzi ujao wa members hao, na uongozi mzima wa CCM.

Hizi nazo zinahitaji data? heee!
 
Mimi ndio nimeweka hapa kwamba Kamati Kuu ina wajumbe 35 na sikukurupuka nimetoa hapa:

http://www.ccmtz.org/0kamatikuu.htm na katika kuangalia jina la Mwenyekiti wa chama Jakaya Mrisho Kikwete lipo.

Hii ya wajumbe 36 hata wengine wamenitumia kwenye PM wakisema hivyo lakini sijui kwanini official website ya chama ionyeshe wajumbe 35!

Hawa 36 sina hakika Komandoo ES amewatoa wapi....ingawa kama nilivyosema majina ni yale yale more or less na yale ya wajumbe 36 ila Mzee ndio hivyo tena kaghafilika kutoa source!

Said Yakubu, ingawa sijasoma Katiba ya CCM, nadhani Komandoo ES yuko sahihi kuwa Central Committee ya CCM ina wajumbe 36 kwa vile kwenye ile orodha uliyoleta inayonyesha wajumbe 35 kwenye website ya CCM kuna makosa kidogo. Serial namba ya 16 imerudiwa mara mbili:

16. Dr. Asha - Rose Migiro - Mjumbe
16. Ndugu Samwel Sitta - Mjumbe
 
Ninaona kuwa muundo huu una walakini fulani. Umechukulia kuwa CCM itaendelea kuwa chama tawala na chenye wabunge wengi. Nafasi ya Waziri Mkuu, Spika wa bunge, Makamu wa Rais, Waziri Kiongozi, na Spika wa Baraza la Wawakalishi zipo pale kame vile wana uhakika kuwa CCM itakuwa inashikilia nafasi hizo miaka yote.
 
Mama Migiro kajiuzulu nafasi za uongozi kwenye chama. Hata Salim alivyoenda OAU alifanya hivyo hivyo na kujiuzulu. Hivyo Migiro sio mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri ya CCM. Hayo mambo ya mpaka mwisho wa mwaka huu hayana ukweli.

Katiba ya CCM haisemi mahali popote kwamba rais mstaafu wa CCM ni mjumbe kamati kuu ya CCM. Kama una kipengere hicho ebu tutumie. CCM ina utaratibu wake nje ya katiba unaowaruhusu wazee wao kwenye vyama kuhudhuria vikao vya chama. Sidhani kama hata wanapiga kura, ila kwa CCM wanavyoenda mambo hovyo hovyo sitashangaa nikisikia wanapiga kura.

Mzee Kawawa alikuwa Makamu wa Mwenyekiti na bado ni mjumbe, hao wengine wanakuwa waalikwa tu kama wazee waliotumikia chama.
 
Kichuguu,

Soma ujumbe wa Mugongo Mugongo, utagundua kamati kuu ya CCM ina wajumbe chini ya hata hiyo 35. Migiro sio mjumbe tena wa kamati kuu ya CCM, si ajabu hata yule mama wa Zanzibar naye sio mjumbe.
 
Mzee mbona unajichanganya, Kawawa alijiuzulu nafasi zote za chama, sasa anaenda kufanya nini kwenye vikao?

Ninaomba nirudie tena kuwa Mwinyi, Mkapa, na sasa Muungwana, wao ni wajumbe wa kudumu wa kamati hiyo, kutokana na kuwahi kushika nafasi ya mwenyekiti.

Kawawa, JM nao pia ni wajumbe wa kudumu wa kamati hiyo kutokana na kuwahi kushika nafasi ya umakamu na sio anything else,

Kushauri vinginevyo ni kujaribu kutudanganya.

Salim na Mama Migiro, hawakuwa na sababu za kujiuzulu, kama walijiuzulu ilikuwa ni kwa matakwa yao binafsi, lakini hawakulazimishwa na yoyoye, ikiwa ni pamoja na hata katiba,

maana Lusinde alikuwa balozi, na bado alikuwa mjumbe wa kamati hiyo na alikuwa kihudhuria mikutano yote, ya chama taifa na kurudi kituo chake Beijing, na hata alipohamia Nairobi, bado aliendelea tu, mpaka alipoamua kuacha, siasa kabisa. Mangula, bado ni mjumbe wa kamati hiyo mpaka uchaguzi utakapofanyika mwisho wa mwaka huu!
 
Komandoo ES,

NImekuuliza ni kipengere gani cha katiba ya CCM kinasema hivyo kwamba hao ni wajumbe wa kudumu?

Kawawa aliteuliwa kuingizwa kwenye hiyo kamati na sio kwamba anaenda tu kama makamu mwenyekiti mstaafu. Hata asingeteuliwa angeendelee kuhudhuria kama anataka kama mjumbe mwalikwa kwa utaribu wa CCM.

Najua akina Mwinyi, Mkapa, wana uwezo wa kuhudhuria vikao vya chama lakini hilo halimo kwenye katiba ya CCM. Sina hata uhakika kama wanaweza kupiga kura, lakini kama wanapiga basi itakuwa kinyume cha katiba yao wenyewe.

Kazi kwenye vyombo vya kimataifa kuna masharti yake, sio sawa na balozi ambaye bado aliendelea kuwa balozi anayeiwakilisha Tanzania. Ni wajibu wao kuachia nafasi za kisiasa kwenye nchi zao.
 
Mzee hapa nilipo sina katiba, vipi for once na wewe ukaitafuta na kutuwekea hapa, badala ya kusubiri kutafutiwa na mimi all the time,

anayealikwa kwa mujibu wa katiba ya CCM ni mwanasheria mkuu tu, wa serikali, CCM inapokuwa madarakani. Pia waziri mkuu na spika wa bunge, wao wanakuwa wajumbe automatically wa kamati hiyo kutokana na kazi zao.

Please for once unaweza kutitafuta hiyo katiba, Mwinyi, Mkapa, Kawawa, na JM, wanaingia kamati hiyo for th rest of their life on this earth, sio kwa kualikwa bali kwa mujibu wa katiba, anyealikwa ni mwanasheria mkuu tu!
 
Nimesoma Katiba ya CCM, kwa bahati mbaya haionyeshi idadi ya wajumbe wa Kamati kuu ya halmashauri ya CCM. Wanaweza kuwa idadi yoyote kuanzia 17 hadi 36. Inategemea kama Rais wa Muungano na wa Zanzibar wote wanatoka CCM, vile vile kama CCM ina wabunge.


109. (1) Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na wajumbe wafuatao:-

  • Mwenyekiti wa CCM.
  • Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
    anayetokana na CCM.
  • Makamu wawili wa Mwenyekiti wa CCM.
  • Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM.
  • Katibu Mkuu wa CCM.
  • Manaibu Katibu Mkuu wa CCM.
  • Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizasheni.
  • Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.
  • Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
  • Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
  • Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano anayetokan a na CCM, na
    Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anayetokana na CCM.
  • Wajumbe wengine wasiozidi kumi na wanne waliochaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wakiwemo wanawake wasiopungua wanne, wawili kutoka Tanzania Bara na wawili kutoka Tanzania Zanzibar.
  • Mwenyekiti wa Taifa wa kila Jumuiya ya Wananchi inayoongozwa na CCM.
  • Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM.
  • Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.

Kulingana na muundo huo, utaona kuwa wajumbe wa kuchaguliwa ni wale kumi na wanne tu wa group (l), wengine wote huingia kulingana na nyadhifa zao kwenye CCM na serikalini.

Katiba haielezi kama viongozi wastaafu ni wajumbe wa kudumu wa kamati kuu. Ila nadhani wanakuwa accomodated kwenye ile idadi ya kumi na nne ya group (l).
 
hebu tuangalie impact ya majina yalioptishwa na wasi wasu\i wa baadhi yao na hali nzima ya uptishaji majina

Homa ya Uchaguzi Mkuu CCM Wanamtandao sasa wahofu kupigiwa kura za chuki

*Kauli ya Kikwete yawachanganya vichwa
*Yapongezwa kuziba ufa ndani ya chama
*Yadaiwa wengine walishaandaa safu zao

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=3423
Na Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC -CCM) kupitisha majina ya wanachama wanaogombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu ujao Novemba mwaka huu, baadhi wagombea wamekumbwa na kihoro kufuatia msimamo wa chama hicho.

Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kwamba maamuzi mazito ya kukinusuru chama yaliyofikiwa kwenye vikao vya juu vya CCM, vilivyomalizika hivi karibuni mjini Dodoma na 'kumiminiwa zege' na msimamo Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya kikwete, kupitia hotuba yake ya Julai kwa Taifa

Akihutubia Taifa muda mfupi baada ya kumalizika Kikao cha NEC mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wana CCM kuwakataa viongozi wataojinadi kwamba wametumwa na viongozi wa juu akiwemo yeye, mwenyewe kugombea nafasi hizo.

Rais Kikwete alibainisha kuwa binafsi hajamtuma mwanachama yeyote kugombea uongozi kwa nafasi yoyote na kuwataka wanaCCM kuwakata watakaowarubuni kwa mbinu hizo.

Alisema sifa kubwa kwa wanaogombea ni uwezo na kuzidi kuwatahadharisha wanachama hao kuzingatia hilo kwani wanaowachangua ni wawakilishi wao na hawaendi kumwakilisha yeye( Rais).

Kauli ya Rais Kikwete ilikuja siku chache baada ya Kamati Kuu ya CCM (CC) kupitisha maamuzi mazito zikiwemo taarifa za kupigwa marufuku kundi la wanamtandano ndani ya chama hicho ili kukinusuru chama .
Kundi la wanamtandano lilibuka na kujipatia umaarufu mkubwa ndani ya siasa za CCM baada ya kuongoza mapambano kwenye mchakato wa kinyang'anyiro cha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Mei mwaka 2005 ambapo Rais Kikwete, aliibuka kidedea akiwabwaga wagombea wenzake 10 wa nafasi hiyo.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2005 na mgombea wa CCM Rais Kikwete kushinda kwa kishindo dhidi ya wagombea wa vyama vingine, wanamtandao waliuona ushindi huo ni neema na pepo ya kisiasa kwao na kujenga dhana ya kuwaona wanaCCM wengine, 'wapangaji wao wenye nyumba.'

Dhana hiyo iliyowafanya baadhi ya wanachama, kutumia ukaribu wao na viongozi wa juu wa chama, kusaka maslahi zaidi ya uongozi ndani ya CCM na serikalini kwa kigezo kwamba ni washirika wa karibu wa viongozi.

Muda na wakati vilibainisha tishio la mshikamano ndani ya chama kutokana na dhana hiyo na kuchukuliwa hatua ya haraka za kusambaratishwa kundi hilo huku Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete 'akipigilia msumari wa mwisho' kwa kubainisha kuwa hakuna aliyemtuma kugombea uongozi na yeyote atakayesema hiyo wananchi wajue kuwa ni mwongo.

Baada ya vikao vya Dodoma, wanachama waliokuwa na dhana ya mtandao wamekumbwa na dhoruba nzito bila kujua pa kukamata hatua inayoelezwa kuwa imewachanganya wengi kisiasa.

Uchunguzi wa Majira umebani kuwa baadhi ya wanachama waliokuwa kwenye kundi hilo sasa wanahaha kutafuta namna nyingine ya 'kuelea' ndani ya chama baada 'nembo' ya uanamtandao kupoteza thamani yake huku wakiogopa kupigiwa kura za chuki na kukosa nafasi walizoomba.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti juzi baadhi ya wanachama, walisema kuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete amewafumbua macho kwani tayari baadhi ya watu waliokuwa kwenye kundi hilo walikuwa wanaendesha kampeni kwa mwavuli wa wanamtandao na wengine wakitamba kuwa wameagizwa na kiongozi wa juu wa chama kuogombea ili wamsaidie majukumu yake.

Imeelezwa kuwa baadhi ya vigogo ndani ya chama na Serikali ndani ya chama hicho wamekuwa wakilikumbatia na kulienzi kundi la mtandao kwa maslahi yao binafsi.

Vyanzo vyetu vya habari vimedai kuwa wanachama hao wamekuwa wakitumia mtandao huo kupanga safu kwa maslahi ya kisiasa ndani ya chama hicho kikongwe na chenye mtandao mkubwa zaidi nchini.

Baadhi ya viongozi hao wanadaiwa kuandaa mikakati ya kuwasaidia baadhi ya wanamtandao wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho hususan kuanzia ngazi za wilaya hadi ujumbe wa NEC ili kuandaa mazingira mazuri ya kisiasa.

Mmoja wa wabunge mkoani Dar es Salaam (jina na Jimbo tunalihifadhi ) anadaiwa aliwahi kumtahadharisha mmoja wa vigogo hao kuachana na harakati za kuwasaidia wanamtandao hao na kumtaka asiingilie uchaguzi wa chama mkoani humo.

Wakati baadhi ya wanamtandao wakitafuta 'tawi la kushika' Majira limedokezwa kuwa wapo wengine wanahaha kuandaa mkakati mwingine kulikana kundi hilo kwa kutafuta baraka za wakongwe wachama hicho ili waweze kushinda nafasi walizoomba.

Habari zaidi zinadai kwamba pamoja na kundi hilo kusambaratishwa, baadhi ya wanamtandao sasa wanajaribu kupanga mbinu chafu za kuwachafua na 'kuwazibia' baadhi ya wagombea wanaoonekana tishio ambao hawakuwa kwenye kundi la mtandao kabla ya uchaguzi huo.

Hatua ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Kikwete kukemea makundi ndani ya chama na kuwakana wanaotaka kutumia jina lake kujipatia uongozi, imepongezwa na wana CCM wengi na kuonekana kama zege iliyoziba ufa mkubwa uliokuwa unainyemelea CCM.
 
Komandoo ES,

Mimi nilikuwa na katiba hapa na wala sikukuambia unitafutie katiba. Nilichouliza ni kipengere gani cha katiba kinasema hivyo?

Kwa wengine jikoni ni kwa mzee google. Kabla ya kutuma kitu anamtuma mzee google akutafutie ukweli. Mambo kama ya vikao na katiba za vyama yako kwenye mtandao, kwahiyo wala huhitaji kitu zaidi ya a click of a mouse.

Any way sio muhimu tena maana Kichuguu kishaandika kwamba hakuna kipengere hicho. Ni makubaliano yao ya chini chini nje ya katiba.

Hao retired wengi hata hawahudhurii hivyo vikao vingi isipokuwa Kawawa ambaye ujumbe wake ni wa zaidi ya kuwa former VC wa CCM.

Kuhusu hao wastaafu kwamba labda wako kwenye kundi la L, sio kweli maana majina ya hilo kundi kama walivyochaguliwa 2002 tunayo pia. Hawa wastaafu wameingizwa kwa makubaliano nje ya katiba, sishangai maana CCM inafanya mambo mengi kiholela bila kufuata katiba yao.
Wao kuanzia enzi za Nyerere hawatajwi mahali popote ila kama mkutano una umuhimu mkubwa hasa kwenda kuchomoa majina ya watu basi wanaenda.

Hata hao wajumbe 14 wanasema waliochaguliwa na NEC, ukweli ni kwamba NEC inapitisha tu majina baada ya kupendekezwa na Mwenyekiti wao. Huwezi kugombea kuwa mjumbe wa kamati kuu ya NEC. Mwenyekiti ndio anateua watu anaowataka na NEC inaweka mhuri wake tu.
 
Mtanzania said:
Kuhusu hao wastaafu kwamba labda wako kwenye kundi la L, sio kweli maana majina ya hilo kundi kama walivyochaguliwa 2002 tunayo pia. Hawa wastaafu wameingizwa kwa makubaliano nje ya katiba, sishangai maana CCM inafanya mambo mengi kiholela bila kufuata katiba yao.
Wao kuanzia enzi za Nyerere hawatajwi mahali popote ila kama mkutano una umuhimu mkubwa hasa kwenda kuchomoa majina ya watu basi wanaenda.

Hapana, wastaafu wanaingia CC kwa kupitia kundi (L); inawezekana hawapigiwi kura kule kwenye Halmasahsuri kuu ya CCM kwa kuheshimiwa, hivyo wanapita bila kupingwa.

Ikiwa serikali zote mbili zinaundwa na CCM na vile vile maspika wote wawili ni wa CCM, idadi ya wajumbe wa CC itakuwa 36 tu kama nafasi zote 14 za kundi za (L) zimejazwa. Kwenye Uchaguzi wa mwaka 2002 CC ilikuwa na watu 36 ikiwa ni pamoja na Kawawa, Mwinyi, na Salmin Armour. Hiyo inaonyesha kuwa wastaafu hawa walikuwa ni kati ya wale 14 wa kundi (L), labda kama kundi (L) halikujazwa na watu kumi na nne kwa makusudi ya kuacha nafasi kwa wastaafu hawa. Hata hivyo kikatiba bado watahesabika kuwa ni wa kundi (L).
Hata hao wajumbe 14 wanasema waliochaguliwa na NEC, ukweli ni kwamba NEC inapitisha tu majina baada ya kupendekezwa na Mwenyekiti wao. Huwezi kugombea kuwa mjumbe wa kamati kuu ya NEC. Mwenyekiti ndio anateua watu anaowataka na NEC inaweka mhuri wake tu.

Katiba inasema kuwa NEC itachagua majina 14 kuingia kwenye CC kutokana na majina yatakayopendekezwa na mwenyekiti. Kwa hiyo huo ndio uchaguzi wenyewe kwa msingi wa katiba ya CCM; inawezekana Mwenyekiti akapendekeza majina mengi, kwa hiyo wengine wataachwa baada ya uchaguzi (ingawa hii huwa haitokei).
 
Kichuguu,

Nakubaliana na wewe, Nakumbuka Dr. Salim Ahmed Salim, alipendekezwa kama sio na Kamati Kuu, ni Mwenyekiti lakina ilibidi NEC iridhie pendekezo hilo ndio akawa mjumbe wa kamati kuu,,, nadhani hata marais wastahafu wanapitia hapa hapo kwenye kifungu (l). Jamaa wako makini sana kwenye mambo ya katiba yao. Lakini pia wakati mwingine wanaweza kutumia mkutano mkuu ambao unauwezo wa kufanya mambo kulingana na wanavyotaka

Kuna mchangiaji alisema jamaa walifanya kama watakuwa madarakani siku zote, especially walivyokuwa wanaongelea maspika kuwa wajumbe wa mkutano mkuu. lakini si kweli waliweka provision kwamba wasipokuwa wao... basi si lazima spika awepo...

Nanukuu...

109 (1)

(k) Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano anayetokan a na CCM
, na
Spika wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar anayetokana na CCM.
 
Back
Top Bottom