PostGE2025 Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulivyoonesha vazi la Demokrasi la Tanzania linavyochakaa kupitia INEC, Vyama vya Upinzani

PostGE2025 Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulivyoonesha vazi la Demokrasi la Tanzania linavyochakaa kupitia INEC, Vyama vya Upinzani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Joined
Dec 6, 2025
Posts
6
Reaction score
3
Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyamavingi Mwaka 1992, Tanzania imejengwajuu ya msingi wa kikatiba unaotambuademokrasia, utawala wa sheria na heshimakwa haki za binadamu.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano inawekawazi haki za msingi, ikiwemo uhuru wakukusanyika na kujiunga na vyama vyasiasa, uhuru wa maoni na kujieleza, pamoja na haki ya kushiriki katika uongoziwa nchi moja kwa moja au kupitiawawakilishi waliochaguliwa.

Katika ngazi ya kimataifa, Tanzania niMwanachama wa Umoja wa Mataifa naimeridhia Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR), ambalo katika Ibara ya 19 na 21 linatambua uhuru wa maoni nahaki ya kila mtu kushiriki katika utawalawa nchi yake kupitia uchaguzi huru na wahaki.

Aidha, kupitia Umoja wa Afrika, Tanzania imeridhia African Charter on Human and Peoples’ Rights, unaosisitiza haki yakushiriki katika uongozi wa umma, uhuru wa kujiunga na vyama na haki yakukusanyika kwa amani.

Misingi hii ya Kikatiba na kimataifa ndiyokipimo cha ubora wa demokrasia katikataifa lolote. Hata hivyo, katika muktadhawa Tanzania ya leo, kumekuwa na mjadalampana kuhusu kama misingi hiyoinatekelezwa kikamilifu au imebaki kuwaahadi iliyoandikwa kwenye maandishi yasheria.

Uchaguzi Mkuu wa 2025 umeongeza uzitowa mjadala huo, huku ukiibua maswalikuhusu ushindani wa haki, uhuru wavyama vya siasa na usawa katikamchakato wa uchaguzi.

Uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 na taswirakidemokrasia
Umeibua mjadala mpana kuhusu hali yademokrasia nchini. Moja ya hoja kuuimekuwa ni ushiriki huru na wa haki wavyama vya siasa.

1. Vizuizi dhidi ya vyama vya upinzani
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinachotambulika kamachama kikuu cha upinzani, kilikumbwa namisukosuko kadhaa kabla na wakati wauchaguzi. Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa yauhaini, jambo lililoibua mjadala wa kitaifana kimataifa kuhusu uhuru wa kisiasa.

Kwa mujibu wa taarifa za chama hicho, mikutano ya kisiasa ilizuiwa au kuvunjwa, baadhi ya viongozi walikamatwa, nakulikuwa na hatua za kusitisha ruzuku nashughuli za ofisi katika maeneo kadhaa. Hali hii ilitafsiriwa na wadau kamakikwazo kwa ushindani wa haki katikauchaguzi.

Tarehe Desemba 13, 2025 chama hichokilitangaza msimamo wao wa kutoitambuaserikali iliyopo madarakani kwa madaikwamba uchaguzi mkuu haukukidhivigezo vya kidemokrasia pamoja na sheria za uchaguzi. Hivyo, chama hicho kikauitakuwa haukuwa Uchaguzi bali ni uchafuzi.


View: https://www.instagram.com/reel/DSNp4Sdkksc/?igsh=MXQzcGVrNTE2anh5Yg==

Hata baadhi ya vyama vilivyoshirikiuchaguzi vilitoa maoni yanayoashiriakutoridhishwa na mwenendo wamchakato. Mwenyekiti wa Civic United Front (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alieleza hadharani kuwa uchaguzihaukuwa huru na wa haki kwa kiwangokilichotarajiwa na kutaja kuwaulikukuwa ni 'ubakaji wa demokrasia'hivyo akatamka wazi kuwa kunahitajikaserikali ya mpito. Kauli kama hizizimeongeza uzito wa hoja kuwa bado kuna mapungufu katika mfumo wa ushindaniwa kisiasa.


View: https://www.instagram.com/reel/DQuPGwjDAmu/?igsh=dzFmcGFyYjQzNWZo

Kuenguliwa kwa wagombea wa upizani
Suala la kuenguliwa kwa wagombealimeendelea kuwa sehemu ya mijadala yachaguzi mbalimbali. Mchakato wa 2025, mgombea Urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina alienguliwa kwa madai yakutokidhi masharti ya kisheria yakugombea, hatua iliyozua maswali kuhusuuwazi na usawa wa utekelezaji wa kanuni.

Wakati huohuo, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan alikabiliwa na malalamiko kutoka kwabaadhi ya wanachama waliodai uteuziwake haukufuata taratibu za chama, ingawa hakukuwa na hatua ya kuenguliwa.
Tofauti hizi za maamuzi zimeibua mjadalampana juu ya usawa wa kisheria nakiutawala.


View: https://www.instagram.com/reel/DQEt-sVjA8l/?igsh=a3p2ZjNia2xqYjl2

Asasi za kiraia, kupitia ilani yake yauchaguzi kwa vyama vya siasa ya mwaka2024, zilisisitiza haja ya marekebisho yasheria za uchaguzi ili kuepushakuenguliwa kwa wagombea kwa makosamadogo yanayoweza kurekebishika bilakuathiri haki ya msingi ya kushiriki katikauongozi.


View: https://www.instagram.com/p/DIViI3Yi_t-/?igsh=aTczanN6ZWo5a3Jr

Mbali na yote hayo bado Tume Huru yaUchaguzi inanyooshewa vidole kwambahaiko huru kwenye utendaji wake kutokana na namna tume hiyoilivyoundwa, kwani mwenye mamlaka yakuteua makamishna naye ni mmoja wawashindani kwenye uchaguzi hivyoinatajwa kuwa kwa kigezo hicho, Tume hiyo haiwezi kuwa halali na kusimamiahaki na usawa kwa wagombea wote.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Deus Kibamba ambaye ameonyeshakusikitishwa na suala la kuona kwambamoja ya makamishna wa tume hiyo nikada wa CCM, hivyo alihoji uhuru wautendaji wake wa kazi bila kupendeleachama chake.


Suala la kupotea na kutekwa kwa watuwanaoonekana kukosoa mifumo yaserikali na viongozi wa kisiasa linazidikuonyesha namna ambavyo demokrasiainazidi kuzorota, kwani kutoweka kwawakosoaji kunaleta hofu ambayo inazibauhuru wa maoni.

Mwaka 2025, kabla ya uchaguzi mkuuwapo wakosoaji wengi waliodaiwakutekwa akiwepo aliyekuwa Balozi waTanzania nchini Cuba, Humphrey Polepoleambaye kabla ya kutoweka alikuwaakikosoa vikali uteuzi wa mgombea uraiskwenye chama chake akidai kuwahaukufuata katiba ya chama cha mapinduzi, huku akikisitiza uhuru waushiriki wa vyama vingine vya siasakwenye uchaguzi mkuu na kuunga mkonomabadiliko ya mifumo ya kiuchaguzi.

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa wateteziwa haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wakili, Onesmo Olengurumwa kwaupande wake anaona kuwa mfumo waDemokrasia ulianzia kwenye mfumoambao hauendani na Demokrasiayenyewe, ndio maana imekuwa ni ngumukuimarisha Demokrasia hapa nchini.

"Tulijenga Mfumo wa vyama vingi katikamsingi usio imara, tulijenga ghorofa tatu kwenye msingi wa nyumba a kawaida ndiomaana imekuwa rahisi sana kuporomoka. Tulijenga Demokrasia katika mfumo usiowa demokrasia, tulipaswa kuwa na katibampya tangu mwaka 1995 kabla ya kuingiarasmi kwenye uchaguzi wa vyama vingi," amesema.

Ameongeza kuwa, ili kutoka hapo lazimakatiba ibadilishwe kukidhi mfumo uliopo, na suala hilo limekuwa gumu kutokana nakwamba wapo watu ambao wananufaikana mfumo uliopo.

"Mtu yeyote anayenufaika na mfumouliopo, hawezi kuona umuhimu wakubadilisha mfumo. Na mwalimu Nyerere alisema watu wote wanaoogopamabadiliko ni wanyonyaji, hivyo tunabakihapa kwa kuwa kuna watu ambaohawapendi maboresho na mifumo yaDemokrasia, hawataki vyama vingi, Uhuru wa Asasi za Kiraia, uhuru wa vyombo vyahabari kwasababu ya tabia zao za kinyonyaji," anasema Olengurumwa.


View: https://www.instagram.com/reel/DPUUQh6iiY_/?igsh=MXVjeGVqYTNrNDI2dg==

Naye Deus Kibamba, mtaalamu wasayansi ya siasa na mchambuzi waMasuala ya siasa, kwa mtazamo wake anaona Demokrasia imerudi nyuma sana hadi mwaka 1982, analeza kuwa ushirikiwa wananchi kwenye masuala yakidemokrasia una mkanganyiko mkubwahuku akitaja sheria kuwa kuna watuzinawapendelea na kuna watuzinawakandamiza.

"Katiba yetu ina mapengo kuliko ya mzee asiye na meno, kuna kipindi watu wenginewalihoji kuwa Rais ametoa wapi mamlakaya kumteua Naibu waziri Mkuu, katibaimempa Rais nguvu ya kuteua mtu yeyotekwa nafasi ambazo zipo na zisizokuwepo, anaweza kutengeneza nafasi na hapo hapoakamteua mtu kumpa nafasi hiyo, sasawewe utapata wapi nguvu ya kuhoji?"

Hata hivyo ametoa mtazamo wake juu yauwepo wa wagombea binafsi, ambapoamesema kuwa ili kutowanyima haki yawanachi kuchagua au kuchaguliwa, nimuhimu kuwepo pia kwa wagombea huruambao kama wakienguliwa kwa kuonewakwenye vyama vyao wanaweza kusimamapeke yao kugombea nafasi wanazotaka.


View: https://youtu.be/TZP4_KB5F4o?si=fqRD3dYJwbPAhRHe

Kwa kuzingatia viwango vya Katiba, Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamuna African Charter on Human and Peoples’ Rights, tathmini ya demokrasia nchiniTanzania haiwezi kuepuka kupima uwianokati ya maandishi ya sheria na uhalisia wakisiasa.

Iwapo misingi ya uhuru wa kujieleza, kukusanyika, kushindana kwa haki nautawala wa sheria haitaimarishwa kwavitendo, basi mjadala kuhusu kudhoofikakwa demokrasia utaendelea kuwa sehemuya ajenda ya kitaifa, ndani na nje yamipaka ya nchi.
 
Kabla ya October 29 nilijua Tanzania ni nchi ya democracy kumbe ni Kama Burundi na Rwanda na Uganda na congo
 
Back
Top Bottom