Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Status
Not open for further replies.

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,281
8,987
Upigaji kura unaendelea huko Igunga. Watu wengi wamejitokeza na kura zinaendelea katika hali ya amani na utulivu.

Waliojitokeza kwa wingi ni wazee na kina mama.

-------------------
CLOSED: KUPATA MATOKEO FUATILIA THREAD HII - MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO IGUNGA

05:24 PM - Mbowe on Channel 10: Tumeripoti vitendo vingi vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu lakini vyombo vya dola havichukui hatua

05: 10 PM
Mwigulu Nchemba on Channel 10: Ktk kata ya Nhongo (Igunga) kuna mwanamke kapewa karatasi ya kura huku ikiwa imetikiwa sehemu ya mgombea wa CHADEMA
Meneja wa kampeni wa CCM (Mwigulu) anasema ameshitushwa na habari kwamba kuna mama kapewa karatasi imeshawekewa tiki kwenye mgombea wa CHADEMA. Na habari hiyo wamepeleka katika tume ya uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi kahojiwa.

Kuhusu hela zilizokuwa zinagawiwa na mbunge wao si rushwa bali ni hela walizokuwa wanagawa kwa mawakala wake.


05:04 PM
Dr. Slaa anaongea Channel 10:

Anasema watu Igunga wamejitokeza wachache, form namba 17 hazipo na zilizopo hazitumiwi ipaswavyo.

Kasema kuna vurugu zimetokea Tarime na mabomu yamepigwa na DC kaingilia uchaguzi, vurugu nyingine zimetokea Shinyanga kata ya Ndara na huko Njombe.

Kuhusu kukamatwa kwa gari la mbunge likiwa na mil 20 - ni kweli na mbunge wa CCM kaenda kutoa taarifa polisi eti kaibiwa gari na mil 20.

Hivyo wale vijana waliowakamata wafuasi wa CCM na mbunge wao wakigawana hela wamewekwa selo!


05:00PM - KURA SASA ZINAHESABIWA KATIKA VITUO

14.16pm - ITV/Radio One wameripoti kuwa kuna watu wamekamatwa kwenye kituo wakiwa na shahada halisi za watu wengine pamoja na photocopies.

Pia kuna vituo feki (hewa) vimeripotiwa.

Inasuburiwa neno la polisi katika mkutano na waandishi baada ya muda.
Tumemkamata mgambo akiwa kwenye foleni ya kupiga kura huku akitoa rushwa ya shs 5,000/= kata ya Swingizi, baada ya kumweka chini ya ulinzi, tukamkuta na shs laki saba, kwa sasa anashikiliwa na polisi, anasema alitumwa na viongozi wa CCM.

Nchemba anapita kila kituo anamwita msimamizi na kumpa hela, kwa sasa amedhibitiwa na vijana wetu
Habari za hivi punde kutoka Igunga zinasema vijana walinzi wawili wa CDM wanashikiliwa na polisi mjini Igunga kwa kile polisi wanachodai kuwa walitaka kuliteka gari la wafuasi wa CCM ambalo nalo polisi wanalishikilia.

Walinzi hao walifika eneo la Simbo na kukuta kundi dogo la wafuasi wa CCM wakigawa fedha karibu na zahanati ya Simbo.

Baada ya vijana hao kuwashtukia pale ghafla wale watu wa CCM waliamua kutimua mbio na kuliacha gari lao na vijana wa CDM wakaamua kulichukua na kuliendesha hadi kituo cha polisi.

Baada ya upekuzi polisi walikuta mfuko wa plastiki (Rambo) ndani yake mkiwa Sh 20 milioni ambazo ndizo zilikuwa zinagawaiwa kwa watu au wafuasi wa CCM.

Hivyo vijana hao wamegeuziwa kibao na polisi kama kawaida yao na hivyo wameambiwa wameliteka nyara hilo gari.

Kashindye (ambaye ni mgombea wa CHADEMA) kahojiwa sasa hivi ITV baada ya yeye kupiga kura na kusema kwa hapo alipo hali ni shwari ila atapata uhakika zaidi ya mwenendo wa uchaguzi baada ya kutembelea vituo zaidi ya kumi.

Amesema yupo postive na matokeo yoyote yatakayotoka lakini ana uhakika wa yeye kufanya vizuri na kuibuka kidedea.
Abdala Tilata wa StarTV anaongea

Ametembelea vituo 10 hali ni nzuri, usumbufu kidogo.

Askari aliyepotelewa na shahada ya kura aruhusiwa kupiga kura.

Mzee mmoja kaibiwa kadi na mkewe, kafanya kama afande alivofanya hapo juu na karuhusiwa kupiga kura. Mzee kaapa atampa likizo ya unyumba mkewe kwa siku kadhaa kuanzia leo.

Tundu Lissu amekubali hali ni shwari.

Tilata anasifia polisi.

Esta Bulaya live MTV.

Anasifia polisi.

Anasema kinamama, wazee wamejitokeza kwa wingi.

anaulizwa kuhusu mwamko wa vijana.

Anajibu, ati kwamba amekuwa sapraizdi kwamba vijana hawajajitokeza kwa wingi.
Live Mlimani TV: Heche.

mwanahabari: hali ikoje?

heche: ni nzuri, kuna hujuma, shahada zimenunuliwa na mabalozi, vijana wanakamatwa sana, lakini hali ni shwari.

mwanahabari: mahudhurio ya vijana na wazee:

heche: watu mchanganyiko wamejitokeza, vijana ni wengi, watu wazima pia, vijana wanakamatwa, mawakala wanazuiwa kuingia kwenye vituo ati si wakazi wa igunga, wakati sheria haisemi kama wakala lazima awe mkazi.

heche: hao wazee wanaosemwa na esther bulaya na wao wamechoka na maisha magumu, na hawapigii kura ccm.
TBC imeripoti zoezi la kupiga kura Igunga na kumwonyesha mwanamke anayejipambanua kuwa ni wa CHADEMA ambaye amesema balozi mmoja wa nyumba kumi kareport kuwa yeye kafariki dunia ili asipige kura kwa kuwa alikataa kuiunga mkono CCM.
Mlezi wa vyama vya siasa Mh. Tendwa, hajakerwa na wanasiasa (Mbunge Aden Rage) "kupanda na silaha jukwaani" wakati wa kampeini (maana hakutaja kama hilo lilimkera) bali amekerwa na tukio la Mkuu wa wilaya kufanyiwa fujo, kijana kumwagiwa tindikali, na tukio la kurushiana risasi.

Ameyasema haya wakati akihojiwa na Mtangazaji wa TBC1 kuhusu ni mambo gani yalimkera katika uchaguzi mdogo wa Igunga

source: TBC1 saa saba mchana leo.
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,179
657
naam asubuhi kumekucha, wananchi waigunga wakijazana vituoni kwa wingi, hali ya hewa ni nzuri na shuwari. vituo vimefunguliwa mambo yote yako mazuri hadi sasa nimo nikipita hapa na pale
 

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
Kwenye baadhi ya vituo watu hawaoni majina yao.

Mawakala wavutana kwani walikuwa hawatambuani lakini limetatuliwa.
 

Bukutonaga

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
246
46
OK! Pamoja na hayo wana-JF hawa watu ni wezi sana Waangalie hata namna masanduku yatavyo kuwa yana safirishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine humo kwenye magari pawe na raia wetu CDM,kumbukeni vitendo alivyofanya Mahanga Makongoro pale segerea wakati anabadilisha masanduku yake mwenyewe kama hayo yaliyopo Nzega kwa DC.
 

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
279
tatizo la kuhamisha majina ya watu kutoka vituo walivyopiga kura 2010 na kuwapeleka vituo vingine limeanza kuonekana
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
Uchaguzi mdogo wa Igunga unafanyika leo ambapo vyama ninane vinashiriki (tofauti na vyama viwili tu uchaguzi wa 2010) Nani kuvuna nini ni hapo jioni maana kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi matokeo yatatangazwa leo hii.

Kwa wale mnaopenda kufuatilia maendeleo ya yanayojiri Igunga ITV wana program maalum ya siku nzima ku cover uchaguzi huo
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Wana JF Igunga tafadhali tupasheni yanojiri Igunga.

Updates kutoka kwa Wa Jikoni:

  • Hali ni tulivu.
  • Watu wamejitokeza kupiga kura asubuhi hii, wengi wakiwa ni kina mama.
  • Watu wanahakiki majina yao.
  • Hakuna malalamiko, so far
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,228
8,722
vipi kuhusu vituo hewa?hivi cdm ina mawakala wa kutosha vituo vyote?

inao wa kutosha kwa mjibu chanzo kilichoko huko igunga kwa vita hii ukisikia chadema hawana wakala kituo fulani itakuwa ni upumbavu kwasababu makama kutoka mikoa mbalimbali wako tayari kwenda kusimamia na nec imeruhusu mawakala kutoka mikoa mbalimbali..
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,365
OK! Pamoja na hayo wana-JF hawa watu ni wezi sana Waangalie hata namna masanduku yatavyo kuwa yana safirishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine humo kwenye magari pawe na raia wetu CDM,kumbukeni vitendo alivyofanya Mahanga Makongoro pale segerea wakati anabadilisha masanduku yake mwenyewe kama hayo yaliyopo Nzega kwa DC.

Nani hao? CHADEMA?
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

12 Reactions
Reply
Top Bottom