Uchaguzi Kenya: Ubalozi wa Marekani watoa tahadhari ya Usalama kwa raia wake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Wakati Mahakama Kuu ikisubiriwa kutoa uamuzi wa kuidhinisha au kubatilisha Pingamizi la Matokeo ya Urais Jumatatu Septemba 5, 2022, Ubalozi Marekani umeweka vizuizi vya watu kusafiri kwenye mji wa Kisumu, eneo analotokea Raila Odinga

Taarifa ya Ubalozi imenukuliwa ikisema mara kwa mara Kenya imekuwa na migogoro baada ya uchaguzi hivyo kuna uwezekano wa kutokea maandamano yenye vurugu yanayoweza kuhitaji Polisi kuingilia kati, pia migomo na mizozo ya hali ya kiuchumi inaweza kusababisha vurugu

Kutokana na tahadhari hizo, Ubalozi wa Marekani umeweka vikwazo vya usafiri kwa wafanyakazi wa serikali ya Marekani mjini Kisumu. Wizara ya Mambo ya Nje pia imewakumbusha raia wa Marekani kuchukua tahadhari zote.
 
Attachments

  • Security Alert for U.S. Citizens_ Kenya... Court Ruling  - U.S.pdf
    407.6 KB · Views: 2
ki ukweli odinga kashinda na kama hakushinda mfumo tu uliotendeka kwenye uchuguzi na ulikuwa wa kihuni !.

Nilishangaa matokeo kuona ruto yupo standby fasta alipotangazwa haraka haraka na mda mfupi kuanza kutoa order kama kujikinga
 
Mkuu,bado sana.Raila na Ruto kupata mshindi.Kama ni kuiba wote waliiba tatizo ni kwamba walizidiama sehemu.Hawa wanaweza pigana ila uwezekano wa Raila kushinda ni mdogo sana.Kupata 2% ya kura kwenye recount ni mziki mzito.
 
Vipi akiongezewa zile kura elfu 4 plus.?
 
Hii petition ya Raila ni upepo tu, hamna kitu, lakini wafuasi wake ni wepesi wa kuzusha vurugu licha ya kwamba wanajua jamaa kashindwa. Ndio maana marekani wanatoa tahadhari.
 
Hao wamarekani wanaoishi Kenya wenyewe washazoea hizo tahadhari hua hawazifwatilii tena... Juzi mmoja wao alinipigia baada ya kusoma hio taarifa akiniuliza, 'we waonaje, bado niende Kisumu ama nisubiri?' nikamwambia atupilie mbali hio tahadhari, Kisumu iko sawa, na hata kama kutatokea vurugu, yeye hatakua target so hana la kuhofia ... Sahii ywaji enjoy akiogelea ndani ya ziwa kazi kupost insta...
 
Ukishaona marekani imetoa tamko hilo we beba virago vyako usepe haraka,,,,naomba Raila akubali maamuzi ya mahakama tusifikie huko tu,,,
Siku ya uchaguzi mkuu pia walitoa tahadhari wananchi wake kusafiri Kisumu, lakini hapakutokea lolote.
 
Back
Top Bottom