SUDAN: Maafisa wa ubalozi wa Marekani wameondolewa nchini Sudan

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Rais Joe Biden wa Marekani amesema jeshi la Marekani likiwa na ndege 6 za kijeshi za kubeba mizigo limewaondoa maafisa wa ubalozi na familia zao kutoka Sudan mpaka eneo la Siri nchini Ethiopia. Akiongea na waandishi wa habari, rais Biden amesema kwamba katika harakati hizo walishirikiana na Majenerali wa RSF na jeshi la Sudan.

Awali, msemaji wa Mambo ya nje ya Marekani aliwaonya viongozi wote wa pande mbili katika mzozo huo dhidi ya kuwalenga kimakusudi raia wa Marekani katika mashambulizi yao kwani itakuwa na madhara makubwa sana. Jeshi la Marekani linaanda jitihada za kuwaondoa raia wa Marekani wapatao 16,000 waliokwama nchini Sudan na kuwapeleka Kenya.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amekuwa akizungumza mara kwa mara na viongoi wa juu wa pande mbili zinazo hasimiana katika mzozo huo juu ya umuhimu wa kusitisha mapigano na kuupa nafasi mwanya wa majadiliano ya kidiplomasia.

Mpaka sasa, si Marekani wala Urusi iliyojitokeza hadharani na kuonesha kuunga mkono upande wowote katika mzozo huo. Lakini Wapiganasi wa kundi binafsi la WAGNER linashirikiana na wapiganaji wa RSF katika usimamizi wa uchimbaji wa dhahabu katika Migodi 18 ya dhahabu kaskazini mwa Sudan na kuzisafirisha nchini Urusi na China.

Sudan’s paramilitary Rapid Support Forces said that it had coordinated the evacuation with US forces on Sunday. US embassy staff, families evacuated from war-torn Sudan
 
Back
Top Bottom