UCHAGUZI CHADEMA: Ratiba yatoka Rasmi

UCHAGUZI CHADEMA: Ratiba yatoka Rasmi

Chadema wananchi wapi ndugu siasa inawenyewe Wananchi Lema analilia posho hadi povu linamtoka kubishana na Zitto acha watanzania tufe tu kwa njaa wao wakinenepa na jasho la mkulima!
 
ZZK Zaidi yao wanajua atawaumbua jembe la Kigoma hilo ndo maana wamemtoa kafara wanaogopa atakuwa M/kiti akigombea
 
Zitto%20Kabwe%285%29.jpg

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.


Uwezekano wa kumpata mrithi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara iliyokuwa inashililiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye alivuliwa wadhifa huo mwishoni mwa wiki ni Juni 30 mwakani.

Pia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema ambao umekuwa chanzo cha mzozo ndani ya chama hicho, utafanyika Juni 29, mwakani.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za chama hicho kuanzia ngazi ya vitongoji hadi taifa, wanachama wataanza kuchaguana kuanzia Desemba 15 mwaka huu hadi Janauri 15, mwakani, huku viongozi wakuu wa kitaifa wakipatikana wote ndani ya Juni mwakani.

Ratiba hiyo ilitangazwa jana na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa chama hicho, Benson Kigaila, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema, nafasi za katibu mkuu na manaibu wake wawili hupatikana baada ya mwenyekiti kuwasilisha majina mawili kwa kila nafasi kwenye Baraza Kuu kwa ajili ya kupigiwa kura.

Kulingana na ratiba hiyo, uchaguzi huo unamaliza Juni 29, mwakani na uwezekano wa kukutana na Baraza Kuu ni siku moja baada ya kupatikana kwa Mwenyekiti na makamu wake wawili kwa nia ya kuunda sektretariati ambayo huongozwa na Katibu Mkuu akisaidiwa na Manaibu Katibu wakuu wawili, mmoja kutoka Bara na mwingine Zanzibar.

Alisema ratiba hiyo ni utekelezaji wa programu ya ujenzi wa Chadema na mchakato ulianza Novemba 22, mwaka huu kwa kazi ya kusajili wanachama kwenye misingi (ngazi ya vitongoji) yote, ambayo inaendelea hadi Desemba 14, mwaka huu.

Kigaila alisema kwa mujibu wa ratiba hiyo, Desemba 15, mwaka huu hadi Januari 15, mwakani, utafanyika uchaguzi ngazi ya vitongoji na kwamba, Januari 16-30, kitakuwa kipindi cha rufaa na kukagua ukamilifu wa uchaguzi katika ngazi hiyo

Alisema Februari 1-15, mwakani, utafanyika uchaguzi ngazi ya matawi, ambao vijiji kwa vijijini na mitaa kwa mijini na kwamba, Februari 16-29, kitakuwa kipindi cha rufaa na ukaguzi kwenye ngazi hiyo.

Kigaila alisema Aprili 1-10, utafanyika uchaguzi ngazi ya majimbo 139 ya uchaguzi, wakati uchaguzi ngazi ya wilaya utafanyika Aprili 25 hadi Mei 5.

Alisema Mei 20-25, utafanyika uchaguzi ngazi ya mikoa na kwamba, uchaguzi kwenye kanda zote 10 za chama utafanyika Juni 9.

Kwa mujibu wa Kigaila, uchaguzi ngazi ya Taifa Juni 25-30, kwa kuanzia na uchaguzi wa Baraza la Wazee, ambao utafanyika siku moja na ule wa Baraza la Vijana (Bavicha).

Alisema siku ya pili yake (Juni 26) utafanyika uchaguzi wa Baraza la Wanawake (Bawacha) na siku inafuatia (Juni 27) kitafanyika kikao cha Kamati Kuu (CC) inayomaliza muda wake.

Kigaila alisema siku inayofuata (Juni 28) kitafanyika kikao cha Baraza Kuu linalomaliza muda wake kabla mkutano mkuu, ambao utafanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa.

Baadaye, kitafanyika kikao cha Baraza Kuu jipya kwa ajili ya kuchagua CC mpya na siku ya mwisho CC mpya itaweka utekelezaji wa maazimio ya Baraza Kuu na mkutano mkuu kwa kipindi kijacho.

Mapema, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema ratiba hiyo imetokana na maamuzi yaliyofanywa na sekretarieti ya chama hicho.

Mnyika alisema kabla ya hapo, CC katika kikao chake cha Novemba 20-22, mwaka huu, ilijadili kuhusu utekelezaji wa programu mbalimbali za chama, ikiwamo ya ‘Chadema ni Msingi' na operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwenye Kanda.

"Kamati Kuu ikapitisha maamuzi juu ya mwendelezo wa operesheni hizi baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwa sekretarieti ya chama na sekretarieti ikatakiwa kwenda kufanyia kazi hizi ambazo chama kinaendelea kuzifanya," alisema Mnyika.

Awali, Kigaila alisema CC katika kikao hicho ilipokea taarifa ya utendaji ya programu ya ‘Chadema ni Msingi' na kuazimia mambo kadhaa ya namna ya kulipeleka mbele na kuandaa ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama, kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.

Alisema Januari 28, mwaka huu, Baraza Kuu la chama lilikaa jijini Dar es Salaam na kupitisha programu ya kugatua mamlaka ya kupanga, kusimamia na kuendesha programu za ujenzi wa chama kutoka makao makuu na kupeleka mamlaka hayo katika ngazi za kanda.

Alizitaja kanda hizo zilizoundwa na Baraza Kuu kuwa ni Ziwa Magharibi, Ziwa Mashariki, Magharibi, Pemba, Unguja, Kusini, Kaskazini, Kati na Nyanda za Juu Kusini.

Alisema mkakati wa kugatua madaraka, una hatua nne; ambazo ni pamoja na kuzindua na kupata uongozi wa kanda, kutoa mafunzo kwa timu za Taifa, kanda, mikoa, majimbo, kata, vijiji/mitaa na vitongoji, kuunda misingi ya chama na kufanya uchaguzi wa ndani ya chama.

Kigaila alisema kanda zote nane za Bara zimekwishazinduliwa na zina uongozi kamili na kwamba, zile za Zanzibar zimekwishawasilisha mkakati wao na zitazinduliwa mwanzoni mwa Desemba, mwaka huu.

Kigaila alisema jana timu 13 ziliondoka makao makuu kwenda katika kanda kushirikiana na kuunda timu kwenda katika majimbo 103 kwa ajili kukagua utekelezaji wa zoezi, kutambua changamoto zilizopo ili kusaidia upatikanaji wa suluhisho na kutoa mafunzo kwa watekelezaji.

CHANZO: NIPASHE
 
Inaonekana wewe mgeni humu jf, la sivyo ungejuwa kuwa ZZK MATATIZO YA KUKIGAWA CHAMA ameyaanza zamani sana na baadhi ya wafuasi wake walishahamia kwa wanaowatuma (ccm) bado yeye tu, kwa hiyo kama ingekuwa ni juhudi zake uchaguzi ungefanyika tangu 2009. Lakini tulikuwa tunasubiri chama kikomae, na sasa wakati umefika kwani hata mamruki tunaweza kuwabaini. PEOPLEZ! hebu sema POWER. Ni ujinga kujiona kuwa unanguvu zaidi ya CHAMA
mkuu kutofautiana mtizamo usianze ku classify,kwani wewe na dr Nkumbo au ZZK nani anaijua sana CDM?shame on you
 
unavo msifia zzk ndo mumeo mtarajiwa nini? maana niliona mwanaume akiolewa, na kwa kuiga wewe mwekundu ujambo, lazima zzk akuoe b4 december 13
bora wewe ambaye mbowe anakuosha na kukufuta shombo!!
 
Mbowe anagombea tena awamu nyingine?!

Kwasababu katiba ya sasa haina ukomo!

Sent from BlackBerry 9520
 
Haya sasa Nape, kile kipengele kilichokuwa ndiyo hoja yako kuu, sasa ndcho hicho kimetangazwa. Sijui utakuwa na hoja gani uliyobakiwa nayo masikini?
 
Katiba iliyoandikwa na watu watatu ndo hiyo hiyo itazingatiwa Kwenye huo uchaguzi au mtafuata maagizo ya mbowe.

Kweli kabisa, si unajua ile ya sisiemu iliandikwa na wanachama wooote milioni 2, walikaa pale lumumba kwa miezi mitatu wakaikamilisha!!!
 
0777691839 Kamanda mbowe nakuunga mkono ndani ya jimbo la ubungo

Ubungo??!!! ni masikitiko kuwa watu wanapomtaka mbunge wao hawamwoni....jimbo limekuwa kama enzi ya Keenja. Mtahadharisheni mbowe na mnyika.
 
Mkuu asante kwa taarifa, hapa bila shaka waje wale wenye kidomodomo.

CHADEMA ni zaidi ya jina la mtu


Uchaguzi huu unafanyika Mwaka 2014 ikiwa ni Miaka Mitano baada ya Uchaguzi wa Mwisho uliofanyika Mwaka 2009, ninachoshangaa wale waliokua waking'ang'ania uchaguzi haufanyiki, au ufanyike mwaka huu walikua wana maana gani?
Uongozi wa Chama sio sawa na Umonita wa shule ya msingi kwamba kila mwaka lazima watu wachague upya!!
 
Hwcome ule uvumi wa jana ulipata baraka za jf na post haikufutwa wala haikuwa moved inamaana kurugenzi ya habari ya chadema haukiliona hilo na kuwasiliana na chadema?? Au ilikuwa kweli uchaguzi ilibidi ufanyike baada ya uchaguzi na chadema wameamua baada ya kuona upepo umewaenda vibaya???
 

1. 22/11/2013 - 14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama,

2. 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji,

3. 16 hadi 30 Januari 2014 Rufaa na ukaguzi,

4. 01 hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.


5. 16 hadi 29 Februani ni kusikiliza rufaa na ukaguzi,



6. Majimbo utaanza rasmi 1 hadi 10 Aprili,

7. Uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi Mei 5 mwaka 2014,

8. Na ngazi ya Mikoa ni 20 hadi 25 Mei.


9. Uchaguzi wa kanda unatarajiwa kufanyika Julai 9,

10. Julai 23 hadi 30 utakuwa ndiyo muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na Baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha Uchaguzi wa ndani ya Chama.


UPDATES
===================================================
Kwa mujibu wa katiba yao ya mwaka 2006 muundoo wa chama chao upo kama nilivyoweka hapo chini, na tukiangalia hii ratiba nadhani kuna tatizo kweli maana hakuna uchaguzi wa kata, sasa sijuhi labda wamebadilisha muundo.

VI. SURA YA SITA
6.0 MUUNDO, VIKAO NA UONGOZI WA CHAMA
6.1 Muundo wa Chama
6.1.1 Kutakuwa na ngazi saba za uongozi wa Chama kama ifuatavyo:
(a) Ngazi ya Msingi
(b) Tawi
(c) Kata/Wadi
(d) Jimbo/Wilaya
(e) Mkoa
(f) Jimbo.
(g) Taifa
6.1.2 Uundaji wa ngazi moja ya juu utafanyika tu baada ya kuwa na muundo na uongozi katika
ngazi ya chini kwa angalao 50% ya maeneo ya kiutawala yanayostahili kuwa na muundo
na uongozi wa kikatiba wa Chama kwa ngazi hiyo.
6.1.3 Kwa kuzingatia Ibara 6.1.2 hapo juu, ngazi ya juu ya chama itateua kamati ya muda
itakayokuwa na wajibu wa kuratibu shughuli za chama na kuwaunganisha wanachama
katika eneo lisilo na uongozi wa kikatiba mpaka wanapofikia uwezo wa kuwa na uongozi
wa kikatiba.

hizi ni szccos za watu mkipenda mtafanya siasa za tz ni uongo mtupu
 
Back
Top Bottom