UCHAGUZI CHADEMA: Ratiba yatoka Rasmi

UCHAGUZI CHADEMA: Ratiba yatoka Rasmi

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Posts
19,094
Reaction score
9,261

1. 22/11/2013 - 14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama,

2. 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji,

3. 16 hadi 30 Januari 2014 Rufaa na ukaguzi,

4. 01 hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.

5. 16 hadi 29 Februani ni kusikiliza rufaa na ukaguzi,

Mkuu

Mleta uzi atakuwa ameiruka. kwenye bandiko lake hajagusa Mwezi Machi, Mwezi husika utafanyika uchaguzi wa ngazi husika, sikumbuki tarehe ya kuanza ila mwisho ni tarehe 20.

kwa hiyo uchaguzi wa ngazi hiyo upo.

6. Majimbo utaanza rasmi 1 hadi 10 Aprili,

7. Uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi Mei 5 mwaka 2014,

8. Na ngazi ya Mikoa ni 20 hadi 25 Mei.

9. Uchaguzi wa kanda unatarajiwa kufanyika Julai 9,

10. Julai 23 hadi 30 utakuwa ndiyo muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na Baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha Uchaguzi wa ndani ya Chama.

UPDATES
===================================================
Kwa mujibu wa katiba yao ya mwaka 2006 muundoo wa chama chao upo kama nilivyoweka hapo chini, na tukiangalia hii ratiba nadhani kuna tatizo kweli maana hakuna uchaguzi wa kata, sasa sijuhi labda wamebadilisha muundo.

VI. SURA YA SITA
6.0 MUUNDO, VIKAO NA UONGOZI WA CHAMA
6.1 Muundo wa Chama
6.1.1 Kutakuwa na ngazi saba za uongozi wa Chama kama ifuatavyo:
(a) Ngazi ya Msingi
(b) Tawi
(c) Kata/Wadi
(d) Jimbo/Wilaya
(e) Mkoa
(f) Jimbo.
(g) Taifa
6.1.2 Uundaji wa ngazi moja ya juu utafanyika tu baada ya kuwa na muundo na uongozi katika
ngazi ya chini kwa angalao 50% ya maeneo ya kiutawala yanayostahili kuwa na muundo
na uongozi wa kikatiba wa Chama kwa ngazi hiyo.
6.1.3 Kwa kuzingatia Ibara 6.1.2 hapo juu, ngazi ya juu ya chama itateua kamati ya muda
itakayokuwa na wajibu wa kuratibu shughuli za chama na kuwaunganisha wanachama
katika eneo lisilo na uongozi wa kikatiba mpaka wanapofikia uwezo wa kuwa na uongozi
wa kikatiba.
 
Afadhaali zitto atagombea rasmi nafasi aliyoitaka toka zamani na atashinda ila wachaga watamchakachua kwa ubinafsi wao na hili linawezekana kama hawajamfukuza kabisa uanachama, lkn na uhakika kufukuzwa ni ngumu na kwa kauli ya zitto NTAKUWA WA MWISHO KUTOKA CHADEMA.
 
Ok, taarifa imefika, wale wa makundi "wajiandae kupanga" / "waendelee kupanga mikakati"!! Teh teh teh teeeehe!
 
Afadhaali zitto atagombea rasmi nafasi aliyoitaka toka zamani na atashinda ila wachaga watamchakachua kwa ubinafsi wao na hili linawezekana kama hawajamfukuza kabisa uanachama, lkn na uhakika kufukuzwa ni ngumu na kwa kauli ya zitto NTAKUWA WA MWISHO KUTOKA CHADEMA.

....unajipa matumaini next time mjifunze!!!

Chadema haikujengwa kwa majina...
 
Nauliza. ile kauli ya Dr Slaa aliposema kwamaba Chadema haitofanya uchaguzi mpaka pale chama kitakopokomaa ni INVALID?

Inakuwaje maamuzi yanabadilika katika kipindi hiki?
hizo zote ni juhudi za zzk aidha direct or indirectly!!
 
Nauliza. ile kauli ya Dr Slaa aliposema kwamaba Chadema haitofanya uchaguzi mpaka pale chama kitakopokomaa ni INVALID?
Inakuwaje maamuzi yanabadilika katika kipindi hiki?
Uchaguzi ilikuwa ufanyike december 2013 lakini ili kusaidia kupata viongozi wazuri wasio wasaliti imeoneka ni vizuri kusafisha chama ndio uchaguzi ufanyike kwahiyo mpaka July 2014 chama kitakuwa kimekomaa kwasababu hakitakuwa na mapandikizi tena
 
Miezi sita?? Why muda mrefu sana ilhali general election yenyewe ya taifa haichukui muda mrefu hivyo

Angalia kwanza muundo wa chama kwanza kabla ya kuangalia muda wa miezi sita!

General Elections uhusisha ngazi ngapi za uchaguzi? Lakini pia si mbaya ukaweka mapendekezo yako juu ya muda kila ngazi ichukue naamini hauko peke yako unayeona hivyo labda kilio chako/chenu kitawafikia wahusika na pengine wanaweza kufanyia marekebisho kalenda/ratiba hiyo
 
Uchaguzi ilikuwa ufanyike december 2013 lakini ili kusaidia kupata viongozi wazuri wasio wasaliti imeoneka ni vizuri kusafisha chama ndio uchaguzi ufanyike kwahiyo mpaka July 2014 chama kitakuwa kimekomaa kwasababu hakitakuwa na mapandikizi tena
Ndugu hapo kwenye red ni vitu viwili tofauti. Dr Slaa alisema sababu ni chama kutokomaa na hakutaja mapandikizi.
Kwahiyo kabla chama kuwa na mapandikizi kilikuwa kimekomaa lakini baada ya kugundulika mapandikizi kikarudi katika hali ya kutokomaa?
Mapandikizi wanaondolewa, chama kitakomaa tena?
Mh!!
 
Nauliza. ile kauli ya Dr Slaa aliposema kwamaba Chadema haitofanya uchaguzi mpaka pale chama kitakopokomaa ni INVALID?

Inakuwaje maamuzi yanabadilika katika kipindi hiki?

Mkuu mara nyingine inabidi kubadilika according to the situation.Hii ndo muarobaini wa yote yanayoendelea hivi sasa.Nawapongeza sana kwa hatua hii muhimu.
 
Ndugu hapo kwenye red ni vitu viwili tofauti. Dr Slaa alisema sababu ni chama kutokomaa na hakutaja mapandikizi.
Kwahiyo kabla chama kuwa na mapandikizi kilikuwa kimekomaa lakini baada ya kugundulika mapandikizi kikarudi katika hali ya kutokomaa?
Mapandikizi wanaondolewa, chama kitakomaa tena?
Mh!!
Huyu Msaliti lazima atimuliwe akaungane na gaidi mwenzake Mwigulu
 
Mkuu asante kwa taarifa, hapa bila shaka waje wale wenye kidomodomo.

CHADEMA ni zaidi ya jina la mtu

Bila kelele za ZZK , babu slaa na DJ mbowe walishasema hakuna uchaguzi hadi chama kiimarike, sasa kwa kuwa uchaguzi unakuja wale mayahaya na makarubandika wa makao makuu ufipa mtafute mahali pa kula maana chama kinatolewa mikononi mwa saccos ya mtei na kurudi kwa wanachama, copy, mungi,yerico and co.
 
Back
Top Bottom