1. 22/11/2013 - 14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama,
2. 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji,
3. 16 hadi 30 Januari 2014 Rufaa na ukaguzi,
4. 01 hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.
5. 16 hadi 29 Februani ni kusikiliza rufaa na ukaguzi,
6. Majimbo utaanza rasmi 1 hadi 10 Aprili,
7. Uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi Mei 5 mwaka 2014,
8. Na ngazi ya Mikoa ni 20 hadi 25 Mei.
9. Uchaguzi wa kanda unatarajiwa kufanyika Julai 9,
10. Julai 23 hadi 30 utakuwa ndiyo muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na Baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha Uchaguzi wa ndani ya Chama.
UPDATES
===================================================
Kwa mujibu wa katiba yao ya mwaka 2006 muundoo wa chama chao upo kama nilivyoweka hapo chini, na tukiangalia hii ratiba nadhani kuna tatizo kweli maana hakuna uchaguzi wa kata, sasa sijuhi labda wamebadilisha muundo.
VI. SURA YA SITA
6.0 MUUNDO, VIKAO NA UONGOZI WA CHAMA
6.1 Muundo wa Chama
6.1.1 Kutakuwa na ngazi saba za uongozi wa Chama kama ifuatavyo:
(a) Ngazi ya Msingi
(b) Tawi
(c) Kata/Wadi
(d) Jimbo/Wilaya
(e) Mkoa
(f) Jimbo.
(g) Taifa
6.1.2 Uundaji wa ngazi moja ya juu utafanyika tu baada ya kuwa na muundo na uongozi katika
ngazi ya chini kwa angalao 50% ya maeneo ya kiutawala yanayostahili kuwa na muundo
na uongozi wa kikatiba wa Chama kwa ngazi hiyo.
6.1.3 Kwa kuzingatia Ibara 6.1.2 hapo juu, ngazi ya juu ya chama itateua kamati ya muda
itakayokuwa na wajibu wa kuratibu shughuli za chama na kuwaunganisha wanachama
katika eneo lisilo na uongozi wa kikatiba mpaka wanapofikia uwezo wa kuwa na uongozi
wa kikatiba.