UCHAGUZI CHADEMA: Ratiba yatoka Rasmi

UCHAGUZI CHADEMA: Ratiba yatoka Rasmi

Huyu Msaliti lazima atimuliwe akaungane na gaidi mwenzake Mwigulu
Hata kama ni msaliti ajibiwe tu ili aondoe mashaka aliyonayo, ila kwenye vyama vya siasa mapandikizi na wasaliti karne hii lazima wawepo maana zamani siasa ilikuwa inachukuliwa kama ni sehemu ya kujitolea huku watu wakipiga mishemishe nyingine lakini siku hizi kuna ambao wanatumia siasa kama sehemu ya ajira na ndio maana katika vyama vyetu vya siasa utakuta vijana ambao wapo wapo tu lakini wanaishi mjini vizuri kwa kuji-involve kwenye vyama huku nyadhifa zao hazijulikani.

Dawa ya wasaliti ni kuwaondoa pale wanapoonekana na si kutumia nguvu kuwabaini na kuwachuja pia na kuepuka huu utaratibu kuelekea uchaguzi mkuu wa kupokea wanachama wapya kutoka vyama vingine na kuwapa nafasi ya uongozi badala ya kumchukua kama mwanachama wa kawaida mwisho wa siku watu kama hawa hurudi kule halikotoka au hatokuwa na mapenzi ya chama, wachache kama Slaa aliweza kukaa na ndio maana mpaka leo hii yupo anaelekeza mapambano lakini wengi kiukweli huwa wana ajenda yao mioyoni
 
acheni kupotezea watu muda wao kisha mnaanza kugombania madaraka! Mthamini utu wa watu sio kuchezea vichwa vyetu kwa chaguzi uchwara

uchaguzi wa cdm unakuhusu nini wewe mbulumundu? tunayashangaa sana magamba kwa kuulizia uchaguzi cdm wakati hauwahusu!
 
ZZK Zaidi yao wanajua atawaumbua jembe la Kigoma hilo ndo maana wamemtoa kafara wanaogopa atakuwa M/kiti akigombea

Naona hilo jembe linahtaji kuchomekewa mpini,na litumikishwe na mwenye shamba vingnevyo halina maana yoyote!
 
Naipenda TANZANIA ILA SIPENDI VYAMA VYA SIASA!

huku kwenye jukwaa la siasa unafanya nini? utakuwa gamba tu wewe,
maana huu ndio mtindo wa misukule ya magambani kujifanya haina chama kwa kuhofia kuzomewa kitaa! kweli hiki chama
kimenuka!
 
Nahisi viongozi wa CMD wanataka uchaguzi ndani ya chama uchelewe kidogo!
 
Mmefanya busara sana kwanza kusafisha chama ili ufate uchaguzi bila hivyo yangerudi zzk yaendelee kutusumbua, big up sana Mbowe/CDM
 
1. 22/11/2013 - 14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama,

2. 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji,

3. 16 hadi 30 Januari 2014 Rufaa na ukaguzi,

4. 01 hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.

5. 16 hadi 29 Februani ni kusikiliza rufaa na ukaguzi,

6. Majimbo utaanza rasmi 1 hadi 10 Aprili,

7. Uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi Mei 5 mwaka 2014,

8. Na ngazi ya Mikoa ni 20 hadi 25 Mei.

9. Uchaguzi wa kanda unatarajiwa kufanyika Julai 9,

10. Julai 23 hadi 30 utakuwa ndiyo muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na Baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha Uchaguzi wa ndani ya Chama.

UPDATES
===================================================
Kwa mujibu wa katiba yao ya mwaka 2006 muundoo wa chama chao upo kama nilivyoweka hapo chini, na tukiangalia hii ratiba nadhani kuna tatizo kweli maana hakuna
uchaguzi wa kata, sasa sijuhi labda wamebadilisha muundo.

kwani madiwani, wanaochauliwa wakati wa uchaguzi mkuu si ni viongozi wa kata ? halafu kwani umeuliza na ukaambiwa ni lini walichagua viongozi wa kata na je wanamaliza lini muda wao, kajipange upya ndio urudi tena ku bwabwaja
 
Afadhaali zitto atagombea rasmi nafasi aliyoitaka toka zamani na atashinda ila wachaga watamchakachua kwa ubinafsi wao na hili linawezekana kama hawajamfukuoza kabisa uanachama, lkn na uhakika kufukuzwa ni ngumu na kwa kauli ya zitto NTAKUWA WA MWISHO KUTOKA CHADEMA.
Kanjanja lazma akachukue pesa kwa dear ujeruman ndo aje kwenye uchaguz
....hahahaha kibaraka kajitimua mweny we kwa kwenda mahakaman
 
Mimi Ni Mwanachama Wa Chadema Tawi La Ally Hassani Mwinyi Kata Ya Mikocheni Kadi Namba 502,515..
chadema Makao Makuu Kupitia Mkurugenzi Wa Ogainaizesheni Na Mafunzo Benson Kigaila Kilitangaza Kuwa Uchaguzi Wa Ndani Utaanza Katikati Mwa Mwezi Decemba Kwa Kuanzia Ngazi Ya Misingi, Lakini Mpaka Sasa Hv Ninavyoandika Ikiwa Na Siku 11 Kabla Ya Mwezi Wa Pili Kuingia Uchaguzi Haujaanza, Kwa Ratiba Iliyotolewa Na Kigaila Ni Kuwa Mwezi Huu Ilitakiwa Tuwe Tumemaliza Ngazi Ya Tawi Na Tunaelekea Ngazi Ya Kata..
gazeti La Mwananchi Wiki Iliyopita Liliripoti Kuwa Uchaguzi Wa Ndani Chadema Utafanyika 2016 Watu Tukataharuki Mnyika Akatuweka Sawa Kuwa Si Kweli, Wanaccm Wamekuwa Wakitumia Propaganda Kuwa Chadema Hakina Demokrasia Kwani Kimegoma Hata Kufanya Uchaguzi Wa Ndani Mimi Kama Mwanachadema Nafadhaishwa Sana Na Suala Hili, Nimeongea Na Marando-m/kiti Wa Kanda, Pia Kilewo-katibu Wa Kanda Maalum Ya Dar Na Nimeongea Na Mbaga-katibu Jimbo La Kawe Wote Hawana Majibu Ya Kuridhisha, Mnyika, Makene Au Saa8 Fafanueni Hili..
 
huu ukimya viongozi wetu mpaka sasa bado unatia mashaka kama huu uchaguzi utakuwepo au la
 
Na sisi ndio wanachama sasa cjui huu uchaguzi anachaguliwa nani maana hakuna taarifa za haja. Nafikiri labda chama hakijaona umuhimu wa ngazi za chini kufanya uchaguzi kwa hiyo labda imasubiri ngazi ya kata ili isonge mbele na kata mpaka taifa
 
Back
Top Bottom