Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,157
2008-08-09 09:37:58
Na Simon Mhina
Kuna taarifa kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kumshawishi Profesa Samwel Wangwe Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, awanie ubunge Jimbo la Tarime, kumrithi mdogo wake marehemu Chacha Wangwe.
SOURCE: Nipashe
BTW.Kuna siku nilisema CCM watataka kumsimamisha kaka wa Marehemu ili kupata Sympathy votes maanke katika hali ya kawaida walijua itakua ngumu sana.Nina mashaka sana na hili jambo,interest za CCM kwenye hiki kifo ,imenishangaza sana
Na Simon Mhina
Kuna taarifa kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kumshawishi Profesa Samwel Wangwe Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, awanie ubunge Jimbo la Tarime, kumrithi mdogo wake marehemu Chacha Wangwe.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Bw. Makongoro Nyerere, alisema japokuwa mchakato wa kumpata mgombea atakayesimama katika uchaguzi huo haujaanza, lakini wanamkaribisha Profesa Wangwe awanie nafasi hiyo.
``Profesa Wangwe ni mwanachama wetu, kama kuna watu wanataka agombee, tunamkaribisha, au hata kama yeye mwenyewe anataka ruksa, yule ni mtu wetu, ni mwanachama wetu mwaminifu akija tutafurahi, hakuna chama kinachoweza kukataa msomi bwana,``alisema.
Pamoja na Profesa Wangwe, pia Mwenyekiti huyo aliwakaribisha wanachama wengine wenye sifa wajitokeze muda utakapofika.
Alipoulizwa ni vipi wanakaribisha watu wengine wachukue fomu, wakati Mbunge aliyewania nafasi hiyo mwaka 2005, Bw. Kisyeri Chambiri yupo, Mwenyekiti huyo alisema kwa mazingira ya Tarime, lazima mchakato wa kumpata mgombea wa CCM uanze upya.
Alisema lazima kura za maoni zitaitishwa upya kwa vile hawawezi kumpeleka Bw. Chambiri moja kwa moja kwenye sanduku la kura, kwa vile alishashindwa.
``Hatuwezi kumpeleka moja kwa moja mtu ambaye alishashindwa, lazima tumchuje upya sambamba na wenzake wengine watakaojitokeza,``alisema Bw. Makongoro.
Habari hizo zinasema katika kuhakikisha CCM inapata kura za huruma kupitia Profesa Wangwe, imeweka mkakati kuhakikisha familia `inashikia bango` kifo cha mdogo wake Bw. Chacha Wangwe na kuendelea kuhoji mazingira ya ajali iliyosababisha umauti wake, ili wananchi wajenge hisia kwamba kifo hicho hakikuwa cha kawaida na kwamba kilisababishwa na `wabaya wake`.
``Hizi tuhuma na maswali mengi kuhusu kifo cha Wangwe hazitaisha sasa hivi, kwa vile ni ajenda ya kisiasa katika uchaguzi wa marudio kule Tarime,`` kilisema chanzo chetu.
Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo Profesa Wangwe alisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo.
Alisema suala la kujiingiza kwenye siasa, linahitaji fikra kwanza na si kitu cha kukurupuka.
``Jamani mambo haya mbona mnayapeleka haraka, kwanza mimi nipo kwenye msiba, kama kuna jambo linalotakiwa nilifanyie uamuzi, au nitoe ufafanuzi, nitafanya hivyo baada ya 40 kwisha,`` alisema.
Habari hizo zinasema vyama vitatu vya upinzani NCCR-Mageuzi, CUF na TLP, navyo vimejipanga kuweka mgombea wao na kuitenga Chadema, kwa madai kwamba, haikubariki kutokana na msiba wa Wangwe.
Habari za wasiwasi wa kuitenga Chadema, zimethibitika pale wenyeviti wa vyama hivyo walipoitisha mkutano na waandishi wa habari huku CHADEMA ikiachwa.
Alipoulizwa habari hizo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, alikiri kwamba hakualikwa kwenye mkutano huo.
``Lipumba (Mwenyekiti wa CUF), alinipigia simu kwamba vyama vitatu visivyofungamana na upande wowote tutafanya mkutano, lakini mimi sikualikwa,`` alisema Bw. Mbowe.
Duru za kisiasa toka ndani ya upinzani, zinasema hatua za hekima zisipochukuliwa, uchaguzi mdogo wa Tarime utavunja `ndoa` ya vyama vinne vya upinzani.
SOURCE: Nipashe
BTW.Kuna siku nilisema CCM watataka kumsimamisha kaka wa Marehemu ili kupata Sympathy votes maanke katika hali ya kawaida walijua itakua ngumu sana.Nina mashaka sana na hili jambo,interest za CCM kwenye hiki kifo ,imenishangaza sana
Last edited by a moderator: