Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
msekwa always a loser! short on vision and long on poor judgement!

Kaiyurankuba,
Siku zote twamjua hivo, ila kwa mshangao wake wa matumizi makubwa ya chama anacho kiongoza yeye ama yanamdhihirisha jinsi alivo, ama yanatuhabarisha kwamba chama kinaenda ndivyo sivyo, yaani hakuna mawasiliano kati ya viongozi wakuu hata kwa matumizi makubwa ya mabilioni is just one man show!
 
Mkuu PM,

Heshima mbele, jana nilikuwa ninaongea na Mkulu mmoja wa CCM aliyetoka Tarime, nilipomuuliza kuhusu majimbo ya Biharamulo na Mwibara, kwa furaha sana alinijibu kua "....kijana kumbe hujui kuwa bunge lilishapitisha muswaada wa kupiga marufuku chaguzi ndogo za ubunge miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu?..." akaniambia kuwa maana yake ni kwamba hakutakuwa na mbunge au uchagiz kwenye haya majimbo mpaka uchaguzi mkuu wa 2010,

Nilipombana zaidi, akaniambia "....kijana uchaguzi ukifanyika leo hatushindi CCM..., kwa hiyo hii sheria ni nzuri sana kwetu..."

Sasa hebu wakuu wanaojua vizuri je hiyo sheria ipo kweli au?

wanawanyima wananchi haki ka kwa na muwakilishi wa kuwawakilisha mawazo na mattz yao bungeni kwa miaka mi3, hivi hawa kwa nini wasichukiwe na wananchi, wanafikiria mwisho wa pua zao tuu, CCM wajinga kweli yani
 
Khaaa

Mwe, ndio tusema'ge wamewakumbukia'ga wake sao? au ndo tusemage wamesoka kasi?

after all kauli yao inaonyesha kuwa wanachama wa chadema wanapenda ugomvi kitu ambacho sio kweli kwa asili. wameonyesha ugomvi baada ya kuona kulikuwa na dalili za kuingizwa King na CCM hivi hivi, si unajua hiki chama cha mafisadi siku hizi hakiaminiki?
 
..kabisa mkuu ..kikwete also shares party of blames....unajuwa strategy ya chadema ilikuwa kali....kuhusu kumshirikisha mwenyekiti wao wa chama...they left people guessing ...and never disclose if he would attend....has ukizingatia na zile shutuma kuwa mbowe alikimbia tarime na anaogopa kwenda.....kila mtu alikuwa anajuwa hangekwenda.....IWAPO MBOWE ANGEWAHI TARIME KAMA WENGINE...ANGESABABISHA CHADEMA KUSHINDWA KWANI ANGEKUWA NA MUDA MREFU ZAIDI WA KUWA CENTRE OF ALLEGATION ,...NA ANGEISHIA KUGEUZWA KITUKO ..ZAIDI PIA ANGEWEZA KUANDALIWA WATU WA MUMZOMEA KWELI...KWA KITENDO CHA KWENDA MWISHONI ..AMEKUWA THE REALLY LAST CARD NA MSAADA KWA CHAMA CHAKE.....

Sasa kitendo cha mbowe kutua ghafla tarime kama mwewe kilimfanya kila mmoja kujuwa atasema nini hasa ukizingatia propaganda zilizokwisha mwagwa mwezi mzima....that helped mbowe to pull crowd......na kwa kuwa alikuwa ameshaandaa maneno ya kuwaambia kutokana na propaganda chafu kuwa hangeenda ..that gave chadema more credits..

The fact kwamba mbowe alienda zimebaki siku 4 ....was good kwa kuwa kina makamba walishaongea yote ...hawakuwa tena na jipya.....kina zitto pia walishasema yao...so mbowe alikuja kumalizia kazi yao nzuri.....na ukizingatia aliingia na nguvu ya helicopter na ndani ya siku nne alipita kila mahali..

Kwa uchambuzi wangu...mtu pekee ambaye angeweza angalau ku cover hiyo gap ya kura 7000 walizowazidi chadema..ni kikwete ...tena hata kina makamba wamejitahidi sana....hawakuwa tena na hoja...laiti na yeye angeingia mwishoni kama mbowe ........angeweza kubadili mawazo ya undecided voters ......kwani waliotoa ushindi tarime ni undecided voters ..kwa hali ile ya low voters turn out..kila chama kilipigiwa kura na wapenzi wake walio sacrifice kujitokeza .......na wachache ambao si wakereketwa walishawishika kujitokeza ndio waliamua
mshindi....

Lakini vile vile kitendo cha rais kutokwenda kinaweza kuwa kimemsaidia....kiusalama ..na pili kisiasa....kwani angeweza kuvuna aibu ya kuzomewa..kurushiwa mchanga,mawe ..potelea mbali hata kama yasingemfikia kutokana na ulinzi wake...but ujumbe ungekuwa umefika...na pia angeweza kushindwa uchaguzi vilevile..matokeo yake ingeporomosha zaidi umaarufu wake kitaifa...

Mbeleni tutarajie upinzani kuendelea kupata nguvu kwani uchaguzi huu umebakisha vyama makini vitatu tanzania..ccm.chadema na cuf...vyama vya nccr,tlp ..et al vimejimaliza uchaguzi huu kwa kuonekana wazi kukubali kutumiwa ...hasa kueneza propaganda chafu...hii itawasaidia watanzania kujua waweke wapi matumaini yao...na kwa hapo tutafikia kwenye utabiri wa nyerere kuwa vyama vibaki vichache makini na kwa tanzania [bara]..chadema ndicho chama makini kwa mtazamo wa mwalimu julius kambarage nyerere,,,,.

Kweli kabisa Philemon,

Ninaamini kama Kikwete angekuja Tarime labda hali ingekuwa tofauti kidogo. Watu wamechoka, watu Tanzania wamechoka, wamedhoofu, wana njaa na shida nyingi sana. Wengi wa wananchi wa Tarime sio kwamba wanataka pesa toka kwa serikali yao, wanachotaka ni kusikilizwa, kuheshimiwa, kupewa hali mbadala baada ya dhahabu ambayo wamekuwa wanachimba kwa miaka yote hii kuchukuliwa na wazungu kimizengwe.

Kikwete angekuja akawaeleza wananchi anachofanya au anachotaka kufanya kwa kizazi chao na vizazi vijavyo. CCM inabidi irudi kule ilikokuwa zamani sana kabla ya Nyerere kung'atuka- chama kinachojaribu (au kuonekana) kuwajali wakulima na wafanyakazi wa Tanzania. Haya mengine ya kuleta matajiri wa Mwanza, Musoma na watendaji wa ccm kwenye mashangingi zaidi ya arobaini ni mchezo uliopitwa na wakati kwenye siasa za Tarime.
 
Ikifikia polisi wa Tanzania wanatumia magari kama ambayo yalikuwa yanatumiwa na polisi wa makaburu kule Afrika kusini wakati wa Apartheid basi ujue nchi inaelekea kubaya sana.
Yaliyofanywa (na yaliyotaka kufanywa) na polisi Tarime ni aibu kwa serikali na inabidi sasa wakuu wa polisi na majeshi wakae chini na kujiuliza kama wao ni watanzania kama sisi au wao ni wafanyakazi wa wakoloni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom