Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
2008-08-09 09:37:58
Na Simon Mhina

Kuna taarifa kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kumshawishi Profesa Samwel Wangwe Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, awanie ubunge Jimbo la Tarime, kumrithi mdogo wake marehemu Chacha Wangwe.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Bw. Makongoro Nyerere, alisema japokuwa mchakato wa kumpata mgombea atakayesimama katika uchaguzi huo haujaanza, lakini wanamkaribisha Profesa Wangwe awanie nafasi hiyo.

``Profesa Wangwe ni mwanachama wetu, kama kuna watu wanataka agombee, tunamkaribisha, au hata kama yeye mwenyewe anataka ruksa, yule ni mtu wetu, ni mwanachama wetu mwaminifu akija tutafurahi, hakuna chama kinachoweza kukataa msomi bwana,``alisema.

Pamoja na Profesa Wangwe, pia Mwenyekiti huyo aliwakaribisha wanachama wengine wenye sifa wajitokeze muda utakapofika.

Alipoulizwa ni vipi wanakaribisha watu wengine wachukue fomu, wakati Mbunge aliyewania nafasi hiyo mwaka 2005, Bw. Kisyeri Chambiri yupo, Mwenyekiti huyo alisema kwa mazingira ya Tarime, lazima mchakato wa kumpata mgombea wa CCM uanze upya.

Alisema lazima kura za maoni zitaitishwa upya kwa vile hawawezi kumpeleka Bw. Chambiri moja kwa moja kwenye sanduku la kura, kwa vile alishashindwa.

``Hatuwezi kumpeleka moja kwa moja mtu ambaye alishashindwa, lazima tumchuje upya sambamba na wenzake wengine watakaojitokeza,``alisema Bw. Makongoro.

Habari hizo zinasema katika kuhakikisha CCM inapata kura za huruma kupitia Profesa Wangwe, imeweka mkakati kuhakikisha familia `inashikia bango` kifo cha mdogo wake Bw. Chacha Wangwe na kuendelea kuhoji mazingira ya ajali iliyosababisha umauti wake, ili wananchi wajenge hisia kwamba kifo hicho hakikuwa cha kawaida na kwamba kilisababishwa na `wabaya wake`.

``Hizi tuhuma na maswali mengi kuhusu kifo cha Wangwe hazitaisha sasa hivi, kwa vile ni ajenda ya kisiasa katika uchaguzi wa marudio kule Tarime,`` kilisema chanzo chetu.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo Profesa Wangwe alisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo.
Alisema suala la kujiingiza kwenye siasa, linahitaji fikra kwanza na si kitu cha kukurupuka.

``Jamani mambo haya mbona mnayapeleka haraka, kwanza mimi nipo kwenye msiba, kama kuna jambo linalotakiwa nilifanyie uamuzi, au nitoe ufafanuzi, nitafanya hivyo baada ya 40 kwisha,`` alisema.

Habari hizo zinasema vyama vitatu vya upinzani NCCR-Mageuzi, CUF na TLP, navyo vimejipanga kuweka mgombea wao na kuitenga Chadema, kwa madai kwamba, haikubariki kutokana na msiba wa Wangwe.

Habari za wasiwasi wa kuitenga Chadema, zimethibitika pale wenyeviti wa vyama hivyo walipoitisha mkutano na waandishi wa habari huku CHADEMA ikiachwa.

Alipoulizwa habari hizo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, alikiri kwamba hakualikwa kwenye mkutano huo.

``Lipumba (Mwenyekiti wa CUF), alinipigia simu kwamba vyama vitatu visivyofungamana na upande wowote tutafanya mkutano, lakini mimi sikualikwa,`` alisema Bw. Mbowe.

Duru za kisiasa toka ndani ya upinzani, zinasema hatua za hekima zisipochukuliwa, uchaguzi mdogo wa Tarime utavunja `ndoa` ya vyama vinne vya upinzani.

SOURCE: Nipashe


BTW.Kuna siku nilisema CCM watataka kumsimamisha kaka wa Marehemu ili kupata Sympathy votes maanke katika hali ya kawaida walijua itakua ngumu sana.Nina mashaka sana na hili jambo,interest za CCM kwenye hiki kifo ,imenishangaza sana
 
Last edited by a moderator:
Ben,

wewe unashangazwa na interest za CCM tu?bila hata kuongelea na interest za NCCR na TLP?

huu ni mwanzo,ila tusubiri tuone
 
Ben,

wewe unashangazwa na interest za CCM tu?bila hata kuongelea na interest za NCCR na TLP?

huu ni mwanzo,ila tusubiri tuone

Mkuu,hata mwili bado hujapoa? They are faster like nothing!

Sasa hapa nimeachwa hoi kabisa.
 
Mnachekesha kweli, CCM haina nafasi hapa nyumbani, hata tuchukue gogo na huyo wa CCM gogo litashinda, CHADEMA NI CHAMA MBADALA ,
 
Mnachekesha kweli, CCM haina nafasi hapa nyumbani, hata tuchukue gogo na huyo wa CCM gogo litashinda, CHADEMA NI CHAMA MBADALA ,

Isayamwita,

Kiteto mungeliweka gogo pia labda lingeshinda. Ndio maana CCM wanashinda kirahisi, kuna watu wanashindwa hata kukubali the reality na matokeo yake badala ya kutafuta mbinu za kupambana na CCM wanabaki kushinda kwenye vijiwe wakiamini CCM wataanguka.

Sitashangaa CCM wakishinda Tarime safari hii hasa kama Prof. Wangwe ndiye atakuwa mgombea wao.
 
Isayamwita,

Kiteto mungeliweka gogo pia labda lingeshinda. Ndio maana CCM wanashinda kirahisi, kuna watu wanashindwa hata kukubali the reality na matokeo yake badala ya kutafuta mbinu za kupambana na CCM wanabaki kushinda kwenye vijiwe wakiamini CCM wataanguka.

Sitashangaa CCM wakishinda Tarime safari hii hasa kama Prof. Wangwe ndiye atakuwa mgombea wao.

Mtanzania

Hata tukikuchukua jinsi ulivyo mzee ukasimama upande wa chadema kule Tarime, basi mjengoni ni lazima ulindime.Kwa habari za kiteto sisemi kitu. tumekubali kwa yote yaliyojili.
 
Mtanzania

Hata tukikuchukua jinsi ulivyo mzee ukasimama upande wa chadema kule Tarime, basi mjengoni ni lazima ulindime.Kwa habari za kiteto sisemi kitu. tumekubali kwa yote yaliyojili.

Mhh,No comment!
 
Ili prof ashinde ni lazima akisaliti chama chake cha CCM na aingie CHADEMA hapo ushindi ni mnono, hana mpinzani kwa hilo

Mkuu,

Sasa unajua CCM ni ma-opportunists ndio maana wanaanza kumshawishi Prof.Wangwe.Unakumbuka hata kwenye Mazishi ya mdogo wake bado kuna watu walimtukana kwamba au na yeye anataka lile Jimbo? So in order to compromise with political situation hana budi kuingia kupitia Chadema au chama kingine.

Nakuambia CCM hapa wameonyesha uroho wa madaraka wa hali ya juu kuliko kuthamini ubinadamu.

Makamba na ule waraka pia hawawezi kutenganishwa ingawa aliona moto unamuwakia akakwepa.Makongoro nae anajaribu kuwa smart ktk siasa zetu hizi lakini kwa sasa ni bora akakaa kimya zaidi
 
Mtanzania

Hata tukikuchukua jinsi ulivyo mzee ukasimama upande wa chadema kule Tarime, basi mjengoni ni lazima ulindime.Kwa habari za kiteto sisemi kitu. tumekubali kwa yote yaliyojili.

Isayamwita,

Kwi kwi kwi!! ujumbe umefika mkuu. Waswahili walisema akutukanaye hakuchagulii tusi.
 
Isayamwita,

Kwi kwi kwi!! ujumbe umefika mkuu. Waswahili walisema akutukanaye hakuchagulii tusi.

Mtanzania,

Usinielewe vibaya kabisa, nasema hivyo kwa sababu za msingi kabisa, je wajua kuwa sisi wana Tarime Serikali ya CCM ilitutelekeza siku nyingi? wajua kuwa uchaguzi wa 1995,2000 walikwiba ? ugomvi wetu uko hivi , mji wa tarime umejengwa na dhahabu ya nyamongo, kitendo cha serikali ya ccm kuwanyang'anya wachimbaji wadogowadogo hakika iko siku kitaeleweka.

Na ndiyo maana nasema wewe jiite mkurya nenda pale tarime gombea kupitia CHADEMA Mjengoni ni lazima ulindime Mkuu.
 
SISIEMU wanahangaika bure, na wala hawana haja ya kuharibu pesa yao kwa ajili ya kampeni katika jimbo la Tarime. SISIEMU haikubaliki hata kidogo, nakubaliana na IsayaMwita kuwa unaweza kuweka gogo against mgombea wa SISIEMU na gogo likashinda. Watu wa Tarime ni watu wa principle na msimamo thabiti. Hawataangalia kama Prof. Wangwe ni mdogo wa Marehemu, hakuna cha sympathy kwenye maslahi ya jimbo lao. Kama Prof. Wangwe atakuwa na mpango huo wa kurithi jimbo ni vema akaamia chama kingine tofauti na SISIEMU.
Ukweli utabaki palepale, SISIEMU haikubaliki Tarime.
 
SISIEMU wanahangaika bure, na wala hawana haja ya kuharibu pesa yao kwa ajili ya kampeni katika jimbo la Tarime. SISIEMU haikubaliki hata kidogo, nakubaliana na IsayaMwita kuwa unaweza kuweka gogo against mgombea wa SISIEMU na gogo likashinda. Watu wa Tarime ni watu wa principle na msimamo thabiti. Hawataangalia kama Prof. Wangwe ni mdogo wa Marehemu, hakuna cha sympathy kwenye maslahi ya jimbo lao. Kama Prof. Wangwe atakuwa na mpango huo wa kurithi jimbo ni vema akaamia chama kingine tofauti na SISIEMU.
Ukweli utabaki palepale, SISIEMU haikubaliki Tarime.

Indume
Naona umenisoma, hakika CCM haina chake hapa nyumbani na si vinginevyo,
 
Jimbo apewe Mzalendo wa kweli...Ajiunge na chadema ama wafanye makubaliano...All in all...Vyama vyote ni muhimu kusimamisha mgombea mmoja wa upinzani hapo....Ama hata mgombea HURU kama ikiruhusiwa..Maana wote tunajuwa watu wa Tarime ni wajanja sana tu na wanajuwa utajiri wao..Kutokuwasikiliza ni sawa na kukaribisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Naomba niwawekee habari hii iliyotoka kwenye Tanzania Daima mara baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo wa Kiteto kutangazwa

MATOKEO ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Kiteto yaliyompa ushindi wa asilimia 57 mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Benedict ole Nangoro, yanaonekana dhahiri kukichanganya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kuchanganyikiwa kwa CHADEMA, chama ambacho viongozi wake wakuu walikuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi wa kishindo, yanatajwa kuwa yamesababishwa na kubainika kwa ukweli kwamba watu waliopiga kura ni asilimia 47 tu ya watu wote waliokuwa wamesajiliwa kwa ajili ya uchaguzi katika jimbo zima.

Kupungua huko kwa wapiga kura kumewafanya viongozi na makada hao kuingiwa na hofu kuwa ushindi huo wa CCM kwa kiwango kikubwa unatokana na kufanyika kwa jitihada za chini kwa chini za kununua shahada za wapiga kura ambao walikuwa wakionyesha mwelekeo wa kukikataa chama hicho tawala.

Wasiwasi huo tayari umeifanya CHADEMA itangaze rasmi kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo mdogo wa ubunge, ambao umefanyika kutokana na kufariki dunia kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Benedict Lusurutia.

Katika kuonyesha namna wanavyopinga ushindi huo wa CCM, viongozi wa CHADEMA na mgombea wake, Victor Kimesera, aliyevuna asilimia 41 ya kura zilizopigwa, hawakutokea katika hafla ya kutangaza matokeo hayo, licha ya kusubiriwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi takriban saa 11:45 jioni jana.

Kushindwa kwa wapinzani katika uchaguzi huo, kunazidi kuifanya kambi hiyo ishindwe kuweka rekodi iliyowekwa kwa mara ya mwisho na John Cheyo, aliyeshinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa Magu, mkoani Mwanza miaka 10 iliyopita.

Akizungumza muda mfupi baada ya NEC kutangaza matokeo hayo rasmi, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kuwa chama chake kimedhamiria kwenda mahakamani kupinga ushindi huo wa CCM ambao alisema umepatikana katika misingi ya hila na udanganyifu.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana jioni baada ya kuchelewesha kutangaza matokeo hayo kwa takriban siku nzima, zinaonyesha kuwa Nangoro alishinda kwa kupata kura 21,506, huku Kimesera akifuatia kwa kupata kura 12,561.

Mgombea wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mashaka Fundi, aliambulia kura 300 wakati yule wa PPT-Maendeleo, Juma Saidi, ambaye alitangaza awali kumuunga mkono mwenzake wa CHADEMA alipata kura 110.

Takwimu hizo za NEC zinaonyesha kuwa kati ya wapiga kura 74,629 walioandikishwa katika daftari hilo mwaka 2005 ni watu 35,261 tu walijitokeza kupiga kura hiyo juzi, idadi ambayo kwa kiwango kikubwa ndiyo iliyoishtua CHADEMA.

Kwa upande mwingine, matokeo hayo ya NEC yanaonyesha kwamba, kura halali zilizohesabiwa katika uchaguzi huo zilikuwa ni 34,477, wakati zilizoharibika zikiwa ni kura 784.

Akizungumza baada ya kutangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Faustime Kang’ombe, alisema kuwa, kujitokeza kwa watu wachache kupiga kura kunatokana na wengi wao kuwa mashambani wakati huu, wakiendelea na shughuli za kilimo.

Kwa upande wake, Mbowe alisema kuwa, pamoja na hujuma hizo, kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, ambaye ni kada wa CCM kufanya ziara na kufungua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Kiteto wakati wa kipindi cha kampeni ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi, ambazo hazina budi kupata majibu ya kisheria.

Mbowe alisema kitendo hicho cha Shekifu ambaye ni kada wa CCM kufanya vitendo hivyo, ilikuwa ni ishara ya wazi kuwa alichokuwa akikifanya kilikuwa ni kampeni za wazi kwa mgombea wa chama hicho tawala.

Hata hivyo, kwa siku kadhaa sasa, Shekifu ambaye alikuwa mbunge hadi mwaka 2005, alikana kufanya kampeni kuisaidia CCM, kwa kusema kuwa ziara alizokuwa anazifanya ni za kawaida kwa yeye kama mkuu wa mkoa.

Alisema kuwa hakuna sheria inayomzuia yeye kutembelea eneo lolote la mkoa wake na kuwa hakufanya hivyo wakati huu kwa lengo la kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea wa CCM bali kuhimiza maendeleo.

Kwa muda mrefu jana asubuhi, Mbowe alikuwa na kazi nzito ya kuwazuia wafuasi wa chama hicho wa maeneo yote ya Kibaya, waliokuwa wakitaka kuandamana kwenda kwenye ofisi za NEC kupinga matokeo hayo.

Vijana hao waliandaa mabango ambayo wangeyatumia katika maandamano yao lakini Mbowe aliwazuia akisema kuwa hakuna busara yoyote katika kufanya maandamano katika mazingira ambayo yalikuwepo jana mjini hapa.

“Turudi Dar es Salaam na tutafungua kesi. Hakuna haja ya kuandamana, mtaumizwa na polisi bila sababu,” alisema Mbowe na akawataka vijana hao kuwa watulivu, kwani mapambano ya kusaka ushindi huo bado hayajaisha.

Hata hivyo, aliwalaumu watu ambao walikubali kuingia katika mtego wa kuuza shahada zao na kubainisha kuwa wao ndio waliosababisha matokeo hayo yawe kama yalivyo.

Alisema kuwa chama hicho kina ushahidi wa tuhuma zote ambazo wamezitoa na hivyo wana uhakika wa kushinda katika kesi watakayofungua.

Mbali ya hilo, Mbowe alisema chama chake kinatarajia kufungua kesi ya kikatiba dhidi ya Daftari la Wapiga Kura ambalo limepoteza matumaini yaliyojengeka juu yake, hasa baada ya wapinzani wao kuanza kulitumia kujinufaisha.

Alisema iwapo hatua za makusudi na za mara moja hazitachukuliwa dhidi ya udhibiti wa Daftari la Wapiga Kura, basi litakuwa ni jambo gumu kwa wagombea wa kambi ya upinzani kushinda katika uchaguzi mwingine wowote.

Naomba habari hii ijadiliwe kuhakiki nguvu ya ushindi wa CCM pale Kiteto kwamba ilikuwa wingi wa kura ilizopata ama ununuzi wa shahada za wapiga kura, ama matumizi makubwa ya nguvu za dola (nitawawekea picha za vipgo walivyofanyiwa CHADEMA baadaye),
Kwa taarifa ya discussants hapa jukwaani CHADEMA Kiteto waliandikiana barua 24 kwa muda usiozidi mwezi mmoja na Msimamizi wa Uchaguzi kulalamikia faulu mbali mbali bila hatua yoyote kuchukuliwa (Nakala za barua hizo zikihitajika zitawekwa hapa wazi wazi)

Tuendelee kuadili ili tufikie ukweli kule Kiteto CCM walishindaje? Na je watashindaje huko Tarime?
 
...Maana wote tunajuwa watu wa Tarime ni wajanja sana tu na wanajuwa utajiri wao..Kutokuwasikiliza ni sawa na kukaribisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.

When was the last time you had psychiatric evaluation, jmush1? And who told you that kutowasikiliza watu wa Tarime ni sawa na kukaribisha vita ya wenyewe kwa wenyewe? C'mon man! The fact of matter is, citizens of Tarime are too smart than you think! Kwahiyo usitake ku-generalize mambo hapa kwa kuwa-paint watu wa Tarime kama watu wasioweza ku-resolve issues kwa njia nyingine isipokuwa kwa fujo tu. And by the way, ni watu gani Tanzania kama sio watu wa Tarime ambao walikuwa wa kwanza kifunidisha nchi kuhusu nini maana ya mageuzi ya kweli?
 
When was the last time you had psychiatric evaluation, jmush1? And who told you that kutowasikiliza watu wa Tarime ni sawa na kukaribisha vita ya wenyewe kwa wenyewe? C'mon man! The fact of matter is, citizens of Tarime are too smart than you think! Kwahiyo usitake ku-generalize mambo hapa kwa kuwa-paint watu wa Tarime kama watu wasioweza ku-resolve issues kwa njia nyingine isipokuwa kwa fujo tu. And by the way, ni watu gani Tanzania kama sio watu wa Tarime ambao walikuwa wa kwanza kifunidisha nchi kuhusu nini maana ya mageuzi ya kweli?

MAGEUZI YA KWELI HAPA TANZANIA YATATOKA MARA, SIKU ZAJA WAKATI WASOGEA, SIKU UTAONA AKINA NIMROD MKONO, BUTIKU, MAKONGORO NA WENGINE WENGI, WAMEHAMIA CHADEMA MJUE UKOMBOZI UMEKARIBIA, HAPA TARIME BADO CHADEMA ITASHINDA TU, SIKU YAJA CCM WATABAKI SITOFAHAMU, MUNGU IBARIKI MARA, MKOA WA WALE WANAOJITOA KAFARA(SADAKA) ILI TAIFA HILI LIPONE, ALIANZA MWALIMU, NA SISI TUTAFUATA.................................., HAIJALISHI.

Wana Mara hatuna ukabila, watu tunaolipenda taifa letu, jamani..............!!!!!

Tunajulikana kama matahira (MACHIZI)tusiyo na akili, laiti mwalimu angefufuka akayaona haya,basi yale aliyoyasema yangetimia.

Mwalimu alikwisha kiona chama chenye mwelekeo ni CHADEMA na ndiyo maana tutaendeleza fikra zake.

Vita dhidi ya mafisadi itaendelea tu, ninyi ni mashahidi ni wapi raia wameweza kupigania haki zao bila kuhofu serikali iliyomadarakani? tutaendelea kujitetea hadi tone letu la mwisho.

Tuungeni mkono basi watanzania wenzetu, vita hii isiwe yetu tu,Leo CHACHA KATANGULIA SISI TUKO NYUMA YAKE TU.

Ilikuwaje Makongoro akakisariti CCM siku zile? Hivyo hivyo ndinyo watakavyokisariti mara tena.
 
Safi sana wanatarime.Hawa mafisadi mpaka wakome.AFADHALI NINYI MNATAMBUA UHURU WENU
 
Mimi nashangazwa sana na tabia hii ya kurithiana vyeo hasa vya kisiasa.
Watanzania itabidi tujiulize kuwa huko Tarime kuna watanzania wangapi? Au kuna ukoo tu wa kina Wangwe ambao ndio wao tu amabao wanawajibu wa kugombea cheo cha Ubunge wa Tarime.
Raul Castro huko Cuba aliporithi cheo ya ndugu yake Fidel Castro sisi wengi tulivurupuka na kusema kitendo hicho si cha kidemkrasai. Sasa kwa nini CCM inamtongoza Prof.Wangwe ili angombee ubunge wa Tarime kwa maana cheo kile hapo awali kilikuwa ni cha ndugu yake?
Kama ni hivyo kwa nini CCM ile ile ilitowa jina la J.Kikwete kugombea urais wa Tanzania badala ya mtoto wa mzee Nyerere hususan Makongoro Nyerere kama wao wanaamini vyeo vya kisiasa vinarithiwa?
Tanganyika toka 1961 {Baada ya Uhuru) na Tanzania toka1964 (baada ya muungano) tuliuondoa Uchifu,Umangi na Usultani kwa vile vyeo hivi vyote vilihitaji urithi.Sasa ninyi CCM mnataka kurudisha Uchifu huko Tarime ili kina Wangwe warithiwe cheo cha Ubunge?

Ndio maana hata wabunge wengi wanalalamika kuwa serikali ya CCM sio ya kidemokrasia. Wacheni uppuzi huu.
Tanzania ina mambo mengi muhimu ya kuyafualiza, umasikini,umeme,uchumi na kadhalika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom