Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Mipasho.
Sidhani kama Nzi anataka kumdiss Mtu, ametoa uchambuzi wake mzuri juu ya "ubobezi" wa Bi.Tulia.
Yeye hapo ndipo alipojikita. Mkuu kwa namna ulivyojibu na kama unafundisha UD basi tuna msiba mkubwa.
UD ina tutorial assistants pia. Inawezekana akawa mmojawapo maana upembuzi wake ni mdogo.Tusimlaumu
 
Last edited by a moderator:
nzi umenisaidia kitu... mimi binafsi nimemfahamu tulia tukisali nae mabibo assemblies of god namkumbuka alijitolea sana kanisani yy na mumewe ndo mana naamini mungu amembariki..kuhusu elimu so dili bunge letu mbona la kijinga mno wapumbavu no wengi...so its easy to manage
 
Hongera sana kwa uchambuzi wa kina na wa haki. Wengine hawatakubali juhudi uliyoiweka ktk kuandika uzi huu, ni kawaida yao. Wamevaa miwani ya ukada wa chama.
 
nzi umenisaidia kitu... mimi binafsi nimemfahamu tulia tukisali nae mabibo assemblies of god namkumbuka alijitolea sana kanisani yy na mumewe ndo mana naamini mungu amembariki..kuhusu elimu so dili bunge letu mbona la kijinga mno wapumbavu no wengi...so its easy to manage

Kujitolea sana kanisani ndio ubobezi ?? Kama ndio hivyo kuna wale jamaa walikesha na kukaa airport wakiamini wataenda ulaya bila passports na visa na walijitolea kwa moyo kweli , wala sidhani kama mleta mada alikua na shida na elimu ya Tulia
 

Mkuu nzi, kitendo tuu cha kusoma hadi chuo kikuu pekee, huyo ni msomi!, kufika tuu chuo kikuu sio issue sana unaweza kwenda kosomea sanaa, soshologia, lugha, etc, hata ukitoka na DIV 4 unaingia chuo kikuu!, lakini kujiunga chuo kikuu kusomea sheria miaka hiyo kabla digrii ya sheria kubinafshishwa, kujiunga UDSM kusoma sheria lazima uwe ni DIV 1 kali!.

Kusemea digrii ya pili ya uzamili ndiko mwanzo wa kubobea kwenyewe halafu kufanya shahada ya uzamivu, ndiko kubobea kwenyewe!, ila kitu ulichonisaidia, nilidhani amebobea kwenye administrative law au constitutional law ndio maana akautafuta usipika!, kumbe ni social security law!.

Asante.

Pasco

Pasco, kama ndivyo kwa mujibu wa maelezo yako, 'what is so special' kuhusu huyu dada mpaka atengenezwe na kuonyeshwa kuwa yeye ni mtu wa kipekee katika fani ya sheria? Kwa sababu kama hizo shahada za uzamili na uzamivu si kwamba ni yeye tu ndizo anazo Tanzania, siyo?

Hiyo hali ya 'kumtengeneza' na 'kumwonyesha' kama 'mbobezi' wa masuala ya sheria ndiyo ilinifanya nipende kumchunguza huyu dada. Na kweli nimebaki kuwa disappointed tu; na kushindwa kuona hiyo 'taswira' ambayo Tulia anajengewa na watu.
 
Mkuu,
Hongera sana kwa uchambuzi wa hali ya juu kuhusu Dr. Tulia. Ni wachache sana humu watakaoelewa nini ulichojaribu kuweka wazi, kwani wengi hawataki kusikia madhaifu ya mtu wao. Hongera tena kwa uchambuzi makini.
 
Wataalamu wa lugha wangetuambia kuwa neno "kubobea" lina maana gani? Baada ya hapo tusome bango la mkuu Nzi.
Kubobea kwa kiingereza lina maana ya "specialization". Dr. Tulia Akson amebobea "specialized" katika maswala ya sheria. Sioni kuna kosa. "Daktari amebobea kwenye magonjwa ya wanawake", n.k . Labda kama mnataka kuleta siasa, lakini Dr. Tulia amebobea kwenye maswala ya sheria.

Mkuu Eli79, umeelezea vyema kwa faida ya mleta mada Mkuu Nzi na wengineo. Naomba nifafanue kidogo zaidi juu ya ubobezi unaozungumziwa hapo juu.....

Ni kuwa na shahada 3 ktk fani husika na haijalishi kama umechapisha machapisho mangapi zaidi ya lile andiko kuu (PhD thesis/dissertation). Andiko kuu likishakubalika na examiners (internal&external) na candidate akawasilisha vyema andiko lake kwenye mhadhara ktk chuo husika basi mhusika uhitimu kama PhD holder (mbobezi katika fani husika).

Kwa nini nimesema kuchapisha articles ktk reputable journals inaweza ikawa sio lazima hii inategemea na nchi mhusika aliyofanya shahada yake ya uzamivu (PhD). Mathalani nchi kama Uingereza na Ujerumani vyuo vikuu vyingi havijaweka kigezo cha kuchapisha jarida ndio ukamilishe shahada yako bali wao huzingatia zaidi andiko kuu (thesis) baada ya hapo unaweza kuchapisha machapisho . Kwa upande mwingine vyuo vikuu ktk nchi kama Japani kuwa na ni lazima kuwa na machapisho mawili ambayo yamekubalika ktk majarida ya kimataifa pamoja na andiko lako kuu (thesis) kukubalika kwa watahini na pia kuwasilisha andiko lako ktk mhadhara kwenye chuo husika.

Hivyo ni vyema tukaelewa tofauti zilizopo baina ya nchi. Dr. TULIA amefanyia shahada yake ya uzamivu nchi Afrika ya Kusini ambako pia kwa vyuo vikuu vingi ni lazima uchapishe chapisho kwenye accredited journals zinazotambulikana na wizara yao ya sayansi na teknolojia kama mojawapo ya kigezo cha kuweza kuhitimu shahada ya uzamivu.

Natumaini nimesomeka kwa unahisi!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabla ya kuanza kuelezea machapisho ya Dk. Tulia Ackson ulipaswa utueleze neno ubobezi kwako lina maana gani na kitu gani kinafanya binadamu akaitwa mbobezi katika sheria.

Jenga kwanza msingi wa hoja yako kabla ya kuanza kuelezea unachotaka kukichambua.

Chifu, kama umesoma vyema nilichokiandika usingeniuliza hili swali.

Lakini, nilisema wazi kuwa nimejikita katika 'ubobezi' kwenye anga ya akademia. Na nikasema kwamba katika akademia 'ubobezi' wa mtu utokana machapisho ya mhusika katika majarida ya kitaifa na kimataifa, aina na viwango vya majarida ambayo mtu huyo uchapisha maandiko yake, na idadi ya watu waliosoma, na haswa kunukuu machapisho ya mhusika kwenye maandiko yao. Kupitia machapisho na nukuu za machapisho, hapo ndipo unaweza kuelewa mchango na ushawishi wa mtu husika katika fani na taaluma yake. Kwa uelewa na uzoefu wangu, hivi ndivyo vigezo vya ubobezi katika akademia. Nilivieleza hivi, kabla sijaongelea machapisho yake. Soma tena chifu utaona.
 
Hakuna kesi aliyowahi kushindwa sio Kushinda. Kesi ya Mita mia mbili muulize hukumu kibatala. Leo Tundu lissu alipapatika kuhusu ujio wa Dr.Shein kapigwa vifungu akaamua kukusanya Mifugo ya Fisadi akaitoa nje ya Bunge

hivi i kesi ya mita mia kama rais mwanza alisha sema kuwa ukisha piga kula nenda nyumbani hivi huyo hakimu wa kutengua kauli ya rais ni nani? acheni kumpa credit huyo dada hiyo kesi hata mm ningeshinda as long as rais alishatoa msimamo hakuna hakimu wa kupinga..
 
Hivi ubobezi unamlinganisha na nani?.

Namlinganisha na wabobezi halisi wengine katika sheria Tanzania na kwingineko duniani.

Unaleta mambo ya ku publish academic articles hadi unaongelea impact factor ya journal. Hivi unafikiri mambo hayo ni relevant kwenye jukwaa hili..

Ni relevant kwa sababu ndiyo vigezo vilivyopo sasa katika ulimwengu wa akademia, ambako Tulia inasemekana alikuwa 'mbobezi' wa sheria. Na katika mada hii, mjadala ni juu ya ubobezi wa Tulia katika sheria. Hivyo basi, ni jambo ambalo haliepukiki kujadili 'impact factor' za journals.

Wewe binafsi umewahi kutoa article kwenye jarida hata kama halina hiyo impact factor?.

Hili suala binafsi, ambalo si mahala pake kulijibu wala kulijadili.

Hivi unajua mbinu zinazotumiwa na majarida kupata impact factor kubwa?.

Nafahamu, naelewa na pia najua.

Hata PhD thesis unadai haijawa cited. Labda ungesoma na kusema haina jipya. Labda supervisors wake na examination team waliona inafaa kuwa PhD..

Hapa unachanganya mambo mawili tofauti. Sijasema kuwa PhD thesis yake haifaa, la hasha. Ni sawa na kuchapisha andiko kwenye journal kama Cell, ambalo halijawahi kunukuliwa, halafu nisema halifai. Lakini kwa utaratibu wa kwenye akademia kunukuliwa kwa chapisho lako ni sifa moja kubwa kwamba kuna mtu kasoma na kuweza kuona mchango wa andiko lako katika fikra zake na uandishi wake. Hivyo, ni sifa ya mwana-akademia yeyote kuwa na machapisho ambayo yananukuliwa; na inaonyesha kwamba mchango wako (kupitia uandishi wako) unakubalika au hata kupingwa na wana-akademia wengine. Hii ndiyo fahari ya kuwa mwana-akademia.

Mimi nikisoma post ya mtu lazima niangalie Avatar na Signature yake. Hapo napata mengi kama ya kwako.

Nashukuru kwa kusoma signature yangu, na kupata mengi kama ya kwangu.
 
Nzi

unapoteza muda wako

article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?

unafahamu journals ngapi dunia hii?

unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu

suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa

Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU

Kwan Ugomvi mkuu
Mto hoja katoa hoja ya kisomi tena yenye uchambuzi yakinifu..
Kaonyesha uwezo mkubwa wa kujenga hoja ,, kutafiti na kuitetea sasa hapo Nzi kawaje.
Yakupasa kumjibu kwa Hoja.
Kazi ya NZI Unaifahamu?
 
Kwa Tanzania ukiwa na PhD tu wewe ni mbobezi.

Nimesikia kuna mtu anaitwa Rehema Nchimbi
hiyo PHD yake ni only in Tanzania
labda mkuu Nzi atufanyie uchunguzi wa huyu pia
 
Last edited by a moderator:
Wataalamu wa lugha wangetuambia kuwa neno "kubobea" lina maana gani? Baada ya hapo tusome bango la mkuu Nzi.
Kubobea kwa kiingereza lina maana ya "specialization". Dr. Tulia Akson amebobea "specialized" katika maswala ya sheria. Sioni kuna kosa. "Daktari amebobea kwenye magonjwa ya wanawake", n.k .

Chifu, nikiri kwamba tafsiri kati ya maneno ya kiswahili na kiingereza, siyo nyakati zote utapata maneno kwa kila neno. Kwa mfano, hilo neno 'specialisation' linaweza pia kuwa utaalamu. Kwa hiyo naweza kusema Tulia ni mtaalamu wa sheria, nikiwa na maana ya kusema kuwa amebobea katika sheria. Unaona jinsi tafsiri zinavyokanganya?

Lakini tukiweka hizi semantiki pembeni, msingi wa hoja yangu ni kuweza kufahamu 'upekee' wa Tulia katika taaluma ya sheria, picha ambayo inatengenezwa na watu wa CCM kupitia vyombo vya habari na mijadala humu. Inavyoonyeshwa ni kwamba, akilinganishwa na wanataaluma wengine wa sheria, yeye anakuwa bora zaidi.

Kama nilivyoeleza, kwa bahati nzuri sana katika ulimwengu wa akademia (mahala ambapo Tulia inasemekana ndiko alikopata huo ubobezi) kuna vigezo ambavyo vipo katika kuweza kudadavua utaalamu/ubobezi wa mtu katika fani fulani. Hili nimelishaeleza awali, sina haja ya kulirudia.

Na hata mfano wako wa "Daktari amebobea kwenye magonjwa ya wanawake", kisemantiki na kimantiki unaonyesha kwamba kuna vigezo na sifa zinazopelekea daktari kusemwa amebobea kwenye magonjwa ya wanawake. Sifahamu sana taaluma ya udaktari, lakini naamini kuna vigezo. Pengine, idadi ya operesheni zilizofanikiwa ambazo ameshazifanya daktari husika, idadi ya machapisho juu ya magonjwa ya wanawake ambayo ameandika na kunukuliwa n.k.

Labda kama mnataka kuleta siasa, lakini Dr. Tulia amebobea kwenye maswala ya sheria.

Vyema. Sasa nijibu swali langu, kama nilivyouliza mwisho wa post yangu kuu.

Kwa hiyo, ningependa kuuliza tena, upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa? Ni sifa zipi na vigezo vipi vya kitaaluma vinavyomfanya awe amebobea?
 
Nimesikia kuna mtu anaitwa Rehema Nchimbi
hiyo PHD yake ni only in Tanzania
labda mkuu Nzi atufanyie uchunguzi wa huyu pia

Hiyo PhD ya yeye peke yake anaitumiaje sasa hapa nchini?

Manake kama ni yeye tu aliyenayo....hahahahaa....duuh.

Huwa anajiongelesha mwenyewe na kujiandikia mambo yeye mwenyewe au?
 
Nimesikia kuna mtu anaitwa Rehema Nchimbi
hiyo PHD yake ni only in Tanzania
labda mkuu Nzi atufanyie uchunguzi wa huyu pia

Chifu, Rehema Nchimbi ndiye yule aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma, siyo?
Sitaki kuonekana mfukunyuku. Kwa vile sijasikia huyo Nchimbi akiitwa na kuonyeshwa kuwa ni mbobezi katika taaluma fulani, huyo sina 'ugomvi' naye.
 
Nzi Uzi wako uko vizuri nilikua nafikiri ka wewe huo ufafanuzi ndo umenifanya nijue yukoje hasa hizo articles zake. Kama zimesomwa na mtu mmoja nilijua anazo journal nyingi alizoziandika

Ndiyo hapo sasa. Mbobezi wa taaluma ya sheria, aliyepata shahada yake ya uzamivu mwaka 2007, lakini kwa miaka hii 8, kanukuliwa mara 1 tu, tena na mtanzania.

Kuna msemo kwamba uwongo ukizungumzwa sana bila kupingwa uonekana ukweli. Sasa nimeamua 'kupinga' taswira ya ubobezi wa sheria ambayo Tulia anavikwa na watu wa CCM, katika kumwonyesha ni wa kipekee sana hapa nchini katika fani ya sheria.
 
Chifu, Rehema Nchimbi ndiye yule aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma, siyo?
Sitaki kuonekana mfukunyuku. Kwa vile sijasikia huyo Nchimbi akiitwa na kuonyeshwa kuwa ni mbobezi katika taaluma fulani, huyo sina 'ugomvi' naye.

Ndo huyo huyo mkuu.....
 
Hiyo PhD ya yeye peke yake anaitumiaje sasa hapa nchini?

Manake kama ni yeye tu aliyenayo....hahahahaa....duuh.

Huwa anajiongelesha mwenyewe na kujiandikia mambo yeye mwenyewe au?


Nilivyosikia ni aibu tupu
but 'nimesikia tu'
ndo maana nilikuwa namuomba Nzi atusaidie...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom