Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Mkuu nzi, kitendo tuu cha kusoma hadi chuo kikuu pekee, huyo ni msomi!, kufika tuu chuo kikuu sio issue sana unaweza kwenda kosomea sanaa, soshologia, lugha, etc, hata ukitoka na DIV 4 unaingia chuo kikuu!, lakini kujiunga chuo kikuu kusomea sheria miaka hiyo kabla digrii ya sheria kubinafshishwa, kujiunga UDSM kusoma sheria lazima uwe ni DIV 1 kali!.

Kusemea digrii ya pili ya uzamili ndiko mwanzo wa kubobea kwenyewe halafu kufanya shahada ya uzamivu, ndiko kubobea kwenyewe!, ila kitu ulichonisaidia, nilidhani amebobea kwenye administrative law au constitutional law ndio maana akautafuta usipika!, kumbe ni social security law!.

Asante.

Pasco
Pasco sijui mambo ya sheria lakini nadhani kuwa mwanasheria aliyesomea sehemu fulani hakumpunguzii kuwa na weledi wa sehemu ingine ya sheria,ndio utakuta mwanasheria hajasoma mambo ya uchumi lakini anasimamia kesi/mikataba inayohusu mambo ya makampuni,Mwakyembe ni mbombezi wa mambo ya katiba lakini hakumfanyi hajui mambo ya sheria kuhusu mathalani fedha au mashirika,nadhani kwa aliyesoma sheria hata ingekuwa sio ''adminstrative'' ni tofauti na daktari wa mifugo au mhandisi.pamoja na kuwa sio mwanasheria aliyesomea mambo ya constitutional alimshinda Kibatala kwenye kesi ya mita 200 ambayo ni ya ''constitutional''
 
Dactari aliyebobea ni consultant, title unayoipata baada ya kusoma masters na Kufanya kazi miaka mitatu baada ya kumaliza masters. Sijui kwenye sheria kubobea kuna vigezo gani, lakini kwenye udactari kumaliza masters pekee yake hakukufanyi kuwa dactari uliyebobea, ni hadi ufanye na kazi kwa miaka mitatu.
 
Chifu, nikiri kwamba tafsiri kati ya maneno ya kiswahili na kiingereza, siyo nyakati zote utapata maneno kwa kila neno. Kwa mfano, hilo neno 'specialisation' linaweza pia kuwa utaalamu. Kwa hiyo naweza kusema Tulia ni mtaalamu wa sheria, nikiwa na maana ya kusema kuwa amebobea katika sheria. Unaona jinsi tafsiri zinavyokanganya?

Lakini tukiweka hizi semantiki pembeni, msingi wa hoja yangu ni kuweza kufahamu 'upekee' wa Tulia katika taaluma ya sheria, picha ambayo inatengenezwa na watu wa CCM kupitia vyombo vya habari na mijadala humu. Inavyoonyeshwa ni kwamba, akilinganishwa na wanataaluma wengine wa sheria, yeye anakuwa bora zaidi.

Kama nilivyoeleza, kwa bahati nzuri sana katika ulimwengu wa akademia (mahala ambapo Tulia inasemekana ndiko alikopata huo ubobezi) kuna vigezo ambavyo vipo katika kuweza kudadavua utaalamu/ubobezi wa mtu katika fani fulani. Hili nimelishaeleza awali, sina haja ya kulirudia.

Na hata mfano wako wa "Daktari amebobea kwenye magonjwa ya wanawake", kisemantiki na kimantiki unaonyesha kwamba kuna vigezo na sifa zinazopelekea daktari kusemwa amebobea kwenye magonjwa ya wanawake. Sifahamu sana taaluma ya udaktari, lakini naamini kuna vigezo. Pengine, idadi ya operesheni zilizofanikiwa ambazo ameshazifanya daktari husika, idadi ya machapisho juu ya magonjwa ya wanawake ambayo ameandika na kunukuliwa n.k.

Vyema. Sasa nijibu swali langu, kama nilivyouliza mwisho wa post yangu kuu.

Kwa hiyo, ningependa kuuliza tena, upo wapi huo ubobezi wa Tulia Ackson katika sheria kama inavyosemwa? Ni sifa zipi na vigezo vipi vya kitaaluma vinavyomfanya awe amebobea?

[h=2]
icon1.png
Re: Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?[/h]
Dactari aliyebobea ni consultant, title unayoipata baada ya kusoma masters na Kufanya kazi miaka mitatu baada ya kumaliza masters. Sijui kwenye sheria kubobea kuna vigezo gani, lakini kwenye udactari kumaliza masters pekee yake hakukufanyi kuwa dactari uliyebobea, ni hadi ufanye na kazi kwa miaka mitatu.​

​
 
Pasco sijui mambo ya sheria lakini nadhani kuwa mwanasheria aliyesomea sehemu fulani hakumpunguzii kuwa na weledi wa sehemu ingine ya sheria,ndio utakuta mwanasheria hajasoma mambo ya uchumi lakini anasimamia kesi/mikataba inayohusu mambo ya makampuni,Mwakyembe ni mbombezi wa mambo ya katiba lakini hakumfanyi hajui mambo ya sheria kuhusu mathalani fedha au mashirika,nadhani kwa aliyesoma sheria hata ingekuwa sio ''adminstrative'' ni tofauti na daktari wa mifugo au mhandisi.pamoja na kuwa sio mwanasheria aliyesomea mambo ya constitutional alimshinda Kibatala kwenye kesi ya mita 200 ambayo ni ya ''constitutional''

Chifu, natofuatiana na wewe. Fani ya sheria ni pana sana kuwa Jack of all trades, kwasababu tasnia ya sheria ni specialised profession. Huwezi kuwa mwanasheria wa masuala ya benki na fedha, halafu huyo huyo uwe mwanasheria wa uhifadhi wa wanyamapori. Sijui labda mwanasheria katika ngazi ya shahada ya kwanza, tena pengine mwaka wa kwanza na pili. Lakini kuanzia mwaka wa tatu, shahada ya pili, na kuendelea, hapo mwanasheria ujikita katika eneo fulani la fani ya sheria. Kama huyu dada Tulia alivyojikita kwenye social security law.

Hivyo kwa kuwa fani ya sheria ni pana sana - kama zilivyo fani nyingi za kitaaluma - siyo rahisi kwa mtu 'mbobezi' kuwa mbobezi wa kila specialisation katika tasnia ya sheria. Anaweza kuwa na uelewa wa msingi/awali, lakini hawezi kufikia uweledi wa kama mtu aliyespecialise katika eneo hilo.

Kwa upande mwingine, hiyo 'kesi ya mita 200' sielewi ni kwa misingi gani umeisema ni kesi ya kikatiba? Nifafanulie chifu..
 
Dactari aliyebobea ni consultant, title unayoipata baada ya kusoma masters na Kufanya kazi miaka mitatu baada ya kumaliza masters. Sijui kwenye sheria kubobea kuna vigezo gani, lakini kwenye udactari kumaliza masters pekee yake hakukufanyi kuwa dactari uliyebobea, ni hadi ufanye na kazi kwa miaka mitatu.

Asante chifu kwa ufafanuzi wako juu ya ubobezi katika taaluma ya udaktari wa binadamu. Kwa kweli vigezo vya ubobezi katika tasnia ya udaktari wa binadamu ni tofauti sana na tasnia nyingine. Kwani nasikia kwenye udaktari wa binadamu, haswa madaktari wanaofundisha pia kwenye vyuo vikuu vya udaktari, mtu hapaswi kuwa na shahada ya uzamivu kuweza kufikia ngazi ya uprofesa, siyo?
 
Mkuu kwanza nikupingeze kwa kuweza kutafiti na kuja na hayo yote ulioyapata katika "utafiti" wako

Lakini mi nadhani kwanza kabisa ungetengeneza msingi wa hoja yako kwamba KUBOBEA ndio kupi haswa kisha tuweze kulinganisha na utafiti wako
 
Nzi asante kwa uchambuzi wako. Hizi ni aina ya chambuzi zinazojenga JF.
 
Wewe ata usome uende hadi wapi uko huwezi kufanana na Tulia kichwani dada yuko vizur ni balaa
 
Lakini mi nadhani kwanza kabisa ungetengeneza msingi wa hoja yako kwamba KUBOBEA ndio kupi haswa kisha tuweze kulinganisha na utafiti wako

Chifu, mbona nimefanya hivyo kwenye post yangu kuu? Nimeandika hivi:

Sasa kwa minajili ya kutaka kufahamu ubobezi wake katika sheria (naomba kusema wazi kuwa mimi siyo mtaalamu wa sheria, na nilikuwa simfahamu Tulia Ackson. Ila napenda kujifunza nini watu walio wabobezi katika fani fulani wanafanya), nikaamua kufanya 'utafiti' kidogo. Lengo kuu la 'utafiti' huu usio rasmi ilikuwa ni kuangalia mchango wake kama Mhadhiri wa Sheria katika fani ya Sheria. Ninaposema mchango wake katika fani ya Sheria, ninamaanisha kuangalia machapisho yake katika majarida ya kitaifa na kimataifa katika fani ya Sheria. Katika akademia, ubobezi wa mtu utokana na nini alichochapisha, wapi alipochapisha (ikimaanisha viwango vya majarida husika katika fani), na watu wangapi wamesoma na kwa muhimu sana, kuyanukuu machapisho yake.
 
Mdau Nzi,
Shukrani nyingi kwako kwa kutoa uchambuzi wa kina, ndo maana JamiiForums inazidi kupata heshima kwa kudiriki kufanya ''background'' check kama gazeti la serikali limefanya uchambuzi wa kina au ni chombo cha kusifia maamuzi ya serikali kuwa ameteuliwa ''mbobezi'' wa sheria.
 
Mleta maada umedhirihisha kwamba wewe ni Inzi kweli.

Inzi hatofautishi pilau na kinyesi. Nina imani umenielewa. Hivi ubobezi unamlinganisha na nani?

Kwenye kambi ya Nyumbu kuna wa kumlinganisha naye?

Unaleta mambo ya ku publish academic articles hadi unaongelea impact factor ya journal. Hivi unafikiri mambo hayo ni relevant kwenye jukwaa hili.

Wewe binafsi umewahi kutoa article kwenye jarida hata kama halina hiyo impact factor?

Hivi unajua mbinu zinazotumiwa na majarida kupata impact factor kubwa?

Hata PhD thesis unadai haijawa cited. Labda ungesoma na kusema haina jipya. Labda supervisors wake na examination team waliona inafaa kuwa PhD.

Mimi nikisoma post ya mtu lazima niangalie Avatar na Signature yake. Hapo napata mengi kama ya kwako.

Kama wewe unasoma post ya mtu unaangalia Avatar na signature, basi mwache Nzi aendelee kuwa Nzi. Kwa taarifa tu, rejea post zake zote halafu urudi hapa na upembuzi.
 
Hivi machapisho yote huwa kwa net? Je uwezo wa mtu kitaalum hutokana na machapisho tu? Hao akina Lissu wamechapisha nini kwa international journals? Nadhani umexhukua muda mrefu kufanya utafiti kwa parameters zenye mapungufu.
 
Nzi

unapoteza muda wako

article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?

unafahamu journals ngapi dunia hii?

unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu

suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa

Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU

Mwakyembe ni Dr wa sheria, afanya nini kwa sasa bungeni? Ana tofauti gani na Prof Maji marefu wa Korogwe? Kati idara ya tiba Dr mzuri ni yule anayeweza kutibu mgonjwa vizuri na sio yule anafundisha wanafunzi shuleni.wakili mzuri ni yule anayeshinda kesi nyingi na sio yule wa kufundisha Wanafunzi darasani, kwani PhD ndio nini? Ukiwa na degree 2 ukafanya ya tatu ukimaliza lazima uitwe Dr hakuna jina lingine, sasa kama tatizo ni mtu kuitwa Dr ndio mwenye uwezo basi kapimwe akili.
 
Kwanza kabla ya kuanza kuelezea machapisho ya Dk. Tulia Ackson ulipaswa utueleze neno ubobezi kwako lina maana gani na kitu gani kinafanya binadamu akaitwa mbobezi katika sheria.

Jenga kwanza msingi wa hoja yako kabla ya kuanza kuelezea unachotaka kukichambua.

Mkuu umemsoma lakini mtoa mada? Hili kalieleza vyema kabisa
 
Mwakyembe ni Dr wa sheria, afanya nini kwa sasa bungeni? Ana tofauti gani na Prof Maji marefu wa Korogwe? Kati idara ya tiba Dr mzuri ni yule anayeweza kutibu mgonjwa vizuri na sio yule anafundisha wanafunzi shuleni.wakili mzuri ni yule anayeshinda kesi nyingi na sio yule wa kufundisha Wanafunzi darasani, kwani PhD ndio nini? Ukiwa na degree 2 ukafanya ya tatu ukimaliza lazima uitwe Dr hakuna jina lingine, sasa kama tatizo ni mtu kuitwa Dr ndio mwenye uwezo basi kapimwe akili.

sasa hoja ni nini?

yaani thread yake inamvua phd tulia? au ina significance gani??
 
Hizi sifa tunazopapatikia na kupenda au kuhendekeza kujikweza, ndio Giza la umaskini wetu. Leo hii Obama ana PhD yake ya sheria hapo katulia tu, lakini huwezi sikia akileweshwa sifa za namana hiyo au kuhimiza aitwe Dr. Barack Obama. Leo hii huku tunahimizwa kusema Dr. Kiwete, mara Dr. ....fulani. Ni kwanini tu watumwa wa fikra kiasi hiki?

nashangaa hata mugabe anamavyeti kibao sijasikia wakimwita hayo majina ni tanzania tu ndio unaweza kupata mazezeta ya kushoboka
 
Nakupongeza Nzi kwa utafiti na uchambuzi wako mahiri. Kwa upande mmoja tunaweza kuchukulia matumizi ya neno 'ubobezi' in the context ya Tulia kama sehemu ya tabia ya waandishi wengi hapa nchini kujikomba (flatter) kwa wakubwa hasa wanasiasa (ref. ile katuni ya gazeti la Daily Nation: Tz journalists licking JK's shoes). Lakini kwa upande mwingine hii ni propaganda machine ya CCM (gazeti la Habari Leo ni sehemu yake) iko kazini. Manazi wanaothibiti CCM wanatumia mbinu hii kumpamba mtu wanayemtaka kwenye nafasi kubwa ya uongozi kwa maslahi yao hasa pale penye utata juu ya uwezo wake. Wakati mwingine hutumia hata academic titles bandia; na hii ilianza zamani kwa akina 'Dr' Salmin Amour. (Kile kitabu cha Msemakweli kiliwataja makada wa CCM wenye vyeti na academic titles bandia).
 
Chifu, mbona nimefanya hivyo kwenye post yangu kuu? Nimeandika hivi:

Sasa kwa minajili ya kutaka kufahamu ubobezi wake katika sheria (naomba kusema wazi kuwa mimi siyo mtaalamu wa sheria, na nilikuwa simfahamu Tulia Ackson. Ila napenda kujifunza nini watu walio wabobezi katika fani fulani wanafanya), nikaamua kufanya 'utafiti' kidogo. Lengo kuu la 'utafiti' huu usio rasmi ilikuwa ni kuangalia mchango wake kama Mhadhiri wa Sheria katika fani ya Sheria. Ninaposema mchango wake katika fani ya Sheria, ninamaanisha kuangalia machapisho yake katika majarida ya kitaifa na kimataifa katika fani ya Sheria. Katika akademia, ubobezi wa mtu utokana na nini alichochapisha, wapi alipochapisha (ikimaanisha viwango vya majarida husika katika fani), na watu wangapi wamesoma na kwa muhimu sana, kuyanukuu machapisho yake.

Mkuu kwa nilivyoona mimi binafsi sikudhani kama msingi wa hoja yako ya KUBOBEA umejikita kwenye "machapisho" sababu kwanza kitendo tu chakuwa na PHd kina maana lazima utakua na machapisho, swala la kuyaweka mtandaoni au la hakufanyi mtu kuwa mbobezi
Lakini pili swala la machapisho kuwa cited bado inategemea na chanzo cha habari yako ambacho kililalia zaidi oline, kwa mazingira yetu ya kibongo

Pengine nikubaliane na wewe kwamba kupitia online Dr Tulia hajafanya vizuri sana, nakushauri jaribu kwenda mbali zaidi kwenye utafiti wako mkuu kutafuta data zingine zaidi ya online naamini utapata kitu na utakua katika kipimo kizuri cha kujua ubobezi wake
 
Kama wewe unasoma post ya mtu unaangalia Avatar na signature, basi mwache Nzi aendelee kuwa Nzi. Kwa taarifa tu, rejea post zake zote halafu urudi hapa na upembuzi.

Labda hujanielewa. Nasoma maada au posy mtu. Nikijumulisha na Avatar/Signature yake mara nyingi napata jibu kwa nini kaandika aliyooandika. The same applies to you!
 
Back
Top Bottom