Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Ubobezi katika sheria wa Tulia Ackson ni upi?

Mleta maada umedhirihisha kwamba wewe ni Inzi kweli.

Inzi hatofautishi pilau na kinyesi. Nina imani umenielewa. Hivi ubobezi unamlinganisha na nani?

Kwenye kambi ya Nyumbu kuna wa kumlinganisha naye?

Unaleta mambo ya ku publish academic articles hadi unaongelea impact factor ya journal. Hivi unafikiri mambo hayo ni relevant kwenye jukwaa hili.

Wewe binafsi umewahi kutoa article kwenye jarida hata kama halina hiyo impact factor?

Hivi unajua mbinu zinazotumiwa na majarida kupata impact factor kubwa?

Hata PhD thesis unadai haijawa cited. Labda ungesoma na kusema haina jipya. Labda supervisors wake na examination team waliona inafaa kuwa PhD.

Mimi nikisoma post ya mtu lazima niangalie Avatar na Signature yake. Hapo napata mengi kama ya kwako.

Watanzani wengi hufeli mitihani katika masomo yao kutokana na namna wanavyotafsiri Maswali. Umemwelewa mtoa mada? Naona unatoka nje ya reli taratiiibu huku ukidhani bado upo.
Mleta mada hajamlinganisha Dr.Tulia na mtu yeyote,wewe umeanza kwa kulinganisha, swali ni Dr. Tulia Ubobezi wake ni upi kwa Criteria alizoziweka, ungejibu kwa kutuambia Aidha Upi ni Ubobezi wake, ama, mtoa Hoja ametumia Criteria ambazo hazifai au hazipo.
Otherwise umepaniki ndugu!
 

Mkuu nzi, kitendo tuu cha kusoma hadi chuo kikuu pekee, huyo ni msomi!, kufika tuu chuo kikuu sio issue sana unaweza kwenda kosomea sanaa, soshologia, lugha, etc, hata ukitoka na DIV 4 unaingia chuo kikuu!, lakini kujiunga chuo kikuu kusomea sheria miaka hiyo kabla digrii ya sheria kubinafshishwa, kujiunga UDSM kusoma sheria lazima uwe ni DIV 1 kali!.

Kusemea digrii ya pili ya uzamili ndiko mwanzo wa kubobea kwenyewe halafu kufanya shahada ya uzamivu, ndiko kubobea kwenyewe!, ila kitu ulichonisaidia, nilidhani amebobea kwenye administrative law au constitutional law ndio maana akautafuta usipika!, kumbe ni social security law!.

Asante.

Pasco

Hizo zinaitwa degree za kuvuliwa chupi/bikini ndio ya Huyo naibu wenu.
 
Nzi

unapoteza muda wako

article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?

unafahamu journals ngapi dunia hii?

unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu

suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa

Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU

Sasa ulichoandika hapo ndo Ubobezi wake? Mbona unakuwa kama nguruwe aliyepigwa shoka la utosi alafu akatoroka?
 
Nzi

unapoteza muda wako

article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?

unafahamu journals ngapi dunia hii?

unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu


suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa

Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU

hapo red:hivi benson bana ni mwalimu pale udsm?
 
Watanzani wengi hufeli mitihani katika masomo yao kutokana na namna wanavyotafsiri Maswali. Umemwelewa mtoa mada? Naona unatoka nje ya reli taratiiibu huku ukidhani bado upo.
Mleta mada hajamlinganisha Dr.Tulia na mtu yeyote,wewe umeanza kwa kulinganisha, swali ni Dr. Tulia Ubobezi wake ni upi kwa Criteria alizoziweka, ungejibu kwa kutuambia Aidha Upi ni Ubobezi wake, ama, mtoa Hoja ametumia Criteria ambazo hazifai au hazipo.
Otherwise umepaniki ndugu!

Upende usipende, ubobezi lazima uwe kwa kulinganisha. Ukisema fulani ni mwema, tayari unafanya comparison bila kujijua. Maana yake kuna wengine si wema.
 
Sii tu social security law, bali probate and administation of estates....aiseeee angelikua ni palamagamba kabudi kweli angekua ni mbobezi...

mkuu kama kubobea kwenyewe ndio hapo kwenye red,mbona mi mwenyewe nilikuwa mkali wa executorship kipindi kile nafanya CPA(T)!!!!!!!...
 
Hizo zinaitwa degree za kuvuliwa chupi/bikini ndio ya Huyo naibu wenu.
Mkuu with due respect, huyu bidada namfahamu ni kichwa cha ukweli!. Sijapenda jinsi ulivyotumia hilo neno la kuvuliwa... ni tusi!. Wanawake ni mama zetu, bibi zetu, sangazi zetu, dada zetu, wadogo zetu, wake zetu na watoto wetu, wanastahili kuheshimiwa!.

Kwenye makosa yote ya defamation, yanahitaji ushahidi mbele ya mahakama, lakini shitaka la kumtusi mwanamke, linaitwa 'chastity of women', halihitaji ushahidi, mwanamke akikufungulia kesi ya kwa kumtukana matusi ya nguoni, hahitajiki ushahidi wa any third party, unahukumiwa!.

Kabla hujamtukana mwanamke yoyote tusi lolote, mfikirie kwanza mama yako, alifanya nini ndipo wewe ukazaliwa!.

Heshima kitu cha bure!.

Pasco
 
Hays ndio madhara ya kutokuwa na fair play ground. Nafasi za juu namna hiyo ya spika n naibu wake rasimu ile mliyoitupa ilipendekeza wenye sifa waombe na wafanyiwe interview hadharani. Ona vituko tunavyoletewa kuongoza wenye weledi kuliko wao kisha wanarundikiwa sifa wasizonazo. Eti ubobezi! UPI? Kipi amekifanya chenye maslahi na dunia ?
 
Nzi

unapoteza muda wako

article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?

unafahamu journals ngapi dunia hii?

unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu

suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa

Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU

wewe hujasoma hili andiko ndiyo sababu ya wewe kujibu kama ulivyojibu
 
Hivi machapisho yote huwa kwa net?

Ndiyo. Kwa sababu kwa dunia ya leo (hapa naongelea dunia ya akademia) yenye maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, kutokuweka machapisho yako mtandao ili watu wote duniani (wenye kupata mtandao) ni sawa na kupigana na ukuta. Vilevile, kazi mojawapo ya mwana-akademia ni kufanya tafiti ili kuboresha uelewa au kuleta uelewa mpya kwenye fani husika. Sasa usipoweka machapisho yako kwenye mtandano, watu wa fani husika walio nchi zingine watawezaje kusoma na kuelewa mchango wa muandishi kwenye hiyo fani?

Je uwezo wa mtu kitaalum hutokana na machapisho tu?

Ndiyo. Hicho ndicho kigezo kikuu chifu. ndiyo maana katika akademia machapisho utumika katika upandaji wa madaraja. Kwa hiyo uwezo unapimwa kwa kile ulichokiandika na mchango wa ulichokiandika katika fani husika. Na ndiyo maana kwenye akademia kuna msemo usemwao publish or perish.

Hao akina Lissu wamechapisha nini kwa international journals?

Kwa ufahamu wangu siyo mwana-akademia, nikimaanisha hafanyi kwenye taasisi za ki-akademiki. Yeye ni mwanasheria na wakili tu. Sana sana nakumbuka alishiwahi kuwa mtafiti kupitia mtandao wa wanasheria wa mazingira. Kwa hiyo kama Lissu hayupo kwenye akademia halazimiki kuchapisha kwenye majarida ya kimataifa ili kudhiirisha ubobezi wake, kama ilivyokuwa kwa Tulia Ackson.

Nadhani umexhukua muda mrefu kufanya utafiti kwa parameters zenye mapungufu.

Hapa inategemeana na maana ya 'muda mrefu' kwako. Kwa kuwa neno 'muda mrefu' ni relative sana, inategemeana na mazingira na tukio husika. Lakini ili kunisaidia katika swali langu, leta hizo parameters zisizo na mapungufu ili tujadili 'ubobezi' wa Tulia Ackson katika fani ya sheria.
 
Nakupongeza Nzi kwa utafiti na uchambuzi wako mahiri. Kwa upande mmoja tunaweza kuchukulia matumizi ya neno 'ubobezi' in the context ya Tulia kama sehemu ya tabia ya waandishi wengi hapa nchini kujikomba (flatter) kwa wakubwa hasa wanasiasa (ref. ile katuni ya gazeti la Daily Nation: Tz journalists licking JK's shoes). Lakini kwa upande mwingine hii ni propaganda machine ya CCM (gazeti la Habari Leo ni sehemu yake) iko kazini. Manazi wanaothibiti CCM wanatumia mbinu hii kumpamba mtu wanayemtaka kwenye nafasi kubwa ya uongozi kwa maslahi yao hasa pale penye utata juu ya uwezo wake. Wakati mwingine hutumia hata academic titles bandia; na hii ilianza zamani kwa akina 'Dr' Salmin Amour. (Kile kitabu cha Msemakweli kiliwataja makada wa CCM wenye vyeti na academic titles bandia).

Nimekuelewa mkuu. Watu wa CCM wamemjengea Tulia taswira ya kumwonyesha ni wa kipekee sana. Kumbe ni wa kawaida tu. Ndiyo maana nikapata hamasa ya kumchunguza, na kugundua kuwa hajafanya jambo lolote over-the-top katika fani yake ya sheria.
 
Mkuu kwa nilivyoona mimi binafsi sikudhani kama msingi wa hoja yako ya KUBOBEA umejikita kwenye "machapisho"

Hili nimelieleza kwa wazi kabisa katika post yangu kuu. Pengine hukusoma kwa makini.

sababu kwanza kitendo tu chakuwa na PHd kina maana lazima utakua na machapisho,

Siyo kweli. Kama mdau mmoja alivyoelezea humu awali, hili utegemeana na taratibu za vyuo kwenye nchi husika. Kwa mfano, nchi za Uingereza, Ujerumani na Marekani (kwa vyuo ninavyovifahamu kwenye nchi hizi), utaratibu sana sana wa kutunukiwa shahada ya uzamivu ni kuwa na Ph.D. thesis au dissertation. Unaweza kuchapisha makala kwenye majarida ya kimataifa, lakini haulazimiki sana kufanya hivyo. Kwa hiyo mtu aliyesoma shahada ya uzamivu katika nchi hizo anaweza kumaliza shahada akiwa na chapisho moja tu, ambalo ni hiyo thesis au dissertation yake.

Kwa vyuo kwenye nchi za Skandinavia utaratibu ni kwamba ili uweze kutunukiwa shahada yako ya uzamivu basi ni lazima uchapishe makala kadhaa kwenye majarida ya kimataifa yenye viwango ambavyo vimewekwa na vyuo husika. Kwa hiyo, mwanafunzi aliyemaliza masomo yake Skandinavia akimaliza lazima awe na machapisho kwenye majarida.

Kwa upande mwingine, sidhani kama hoja yangu ni kusema Tulia hana machapisho. Naamini umeona nimeorodhesha machapisho yake niliyoyapata. Lakini, kwa vigezo ambavyo nimeshavieleza, kupitia hayo machapisho yake, bado sijaona wa hype ambayo wana CCM wanaitengeneza juu yake kwenye ubobezi wa fani ya sheria.

swala la kuyaweka mtandaoni au la hakufanyi mtu kuwa mbobezi

Kama nilivyomweleza mdau mmoja hapo awali, kwa ulimwengu wa sasa kuwa na mawazo kama haya ni sawa na kupingana na ukuta. Na kumbuka kwenye ulimwengu wa akademia knowledge dissemination and sharing ni jambo lisiloepukika. Na kuwa mobile ni jambo la msingi katika kuongeza maarifa na ujuzi kwenye akademia. Sasa usipoweka machapisho kwenye mtandao mambo haya yatafanikiwa vipi? Na kama nilivyosema awali, ili watu wa nchi zingine waweze kusoma na kunukuu machapisho yako, yasipokuwa kwenye mtandao watafanikiwa vipi?

Lakini pili swala la machapisho kuwa cited bado inategemea na chanzo cha habari yako ambacho kililalia zaidi oline, kwa mazingira yetu ya kibongo

Hili nalo nimelieleza wazi kwenye post yangu kuu. Nimesema kwa kutumia Google Scholar na Researchgate, ndiyo nimefikia hitimisho langu. Sasa mkuu, ebu niambie njia ambazo ni effective na efficient (kwa kuzingatia muda na fedha) katika kufahamu ni kwa kiwango gani machapisho ya mtu yamenukuliwa na waandishi wengine kwenye majarida, vitabu na hata thesis au dissertation.

Lakini kama mtu ni mbobezi kweli, hata kwa hayo machapisho 8 yaliyopo kwenye mtandao ingejionyesha. Lakini kwa muda wa miaka 8, 'mbobezi' kanukuliwa mara 1!!

Mazingira yetu ya kibongo yepi bwana?!? Mbona kuna watanzania wabobezi kwelikweli ukiangalia Google Scholar, watu wamenukuliwa zaidi ya mara elfu 1. Hiki hakiwezi kuwa kisingizio chifu kwa bidada Tulia.

Pengine nikubaliane na wewe kwamba kupitia online Dr Tulia hajafanya vizuri sana, nakushauri jaribu kwenda mbali zaidi kwenye utafiti wako mkuu kutafuta data zingine zaidi ya online naamini utapata kitu na utakua katika kipimo kizuri cha kujua ubobezi wake

Mimi nimekamilisha nilichopenda kukifanya. Na kwa mazingira niliyonayo, njia ya online ndiyo bora zaidi. Sasa, kwa kuwa jibu la swali langu bado sijapata, basi wewe nenda mbele zaidi ya nilipoishia kwa kutafuta hizo data zingine, ili uje ujibu juu ya 'ubobezi' wa Tulia Ackson katika sheria.
 
mkuu mimi nadhani ( na kwa kweli ndiyo ukweli wenyewe) mwandishi wa gazeti hilo ametumia kigezo cha ubobezi tofauti na chako.Kwa mtizamo wa mwandishi Dr Tulia ni mbobezi wa sheria kwa sababu ya kuwa na PhD katika sheria na si vinginevyo.We we umetumia kigezo cha Machapisho (Kwa academia hiki ndicho kigezo kikubwa cha ubobezi wa mwanataaluma kwani ndicho hutumika kumpandisha daraja kutoka Lecturer- senior recturer-Associate professor-Professor).
 
Huyo Daktari kabobea kuliko Mh.Asha Rose Migiro.Tuanze kuangalia sheria zikiletwa kwa marekebisho......itaoendeza aaana siku hizo akae kitini
 
mkuu mimi nadhani ( na kwa kweli ndiyo ukweli wenyewe) mwandishi wa gazeti hilo ametumia kigezo cha ubobezi tofauti na chako.Kwa mtizamo wa mwandishi Dr Tulia ni mbobezi wa sheria kwa sababu ya kuwa na PhD katika sheria na si vinginevyo.We we umetumia kigezo cha Machapisho (Kwa academia hiki ndicho kigezo kikubwa cha ubobezi wa mwanataaluma kwani ndicho hutumika kumpandisha daraja kutoka Lecturer- senior recturer-Associate professor-Professor).

Kwanza, ni jambo gani limekufanya kudhani kwako kuwa ndiyo ukweli wenyewe? Pili, kama kuwa na PhD katika sheria ndiko kunamfanya Tulia kuwa mbobezi, hype yote juu ya ubobezi wake ya nini sasa? Kwani yeye ndiye wa kwanza kuwa na PhD katika sheria? Kama mdau ulivyosema humu, what is so exceptional kuhusu Tulia mpaka watu wa CCM wamjengee taswira ya kuwa 'mbobezi' wa kipekee katika sheria? Na tatu, kama nilivyosema, kwa kuwa Tulia alikuwa kwenye akademia, na ndiyo msingi wa yeye kuonwa 'mbobezi' na watu wa CCM, hilo la machapisho haliwezi kuepukika, kwani ndiyo kipimo cha ubobezi kwenye ulimwengu huo.

Na kumbuka, hilo la kwenye gazeti ni eneo moja tu. Nimesema, 'ubobezi' na 'upekee' wa Tulia Ackson unasemwa sana humu JF na kwenye socia media outlets zingine.
 
Mkuu kwa nilivyoona mimi binafsi sikudhani kama msingi wa hoja yako ya KUBOBEA umejikita kwenye "machapisho" sababu kwanza kitendo tu chakuwa na PHd kina maana lazima utakua na machapisho, swala la kuyaweka mtandaoni au la hakufanyi mtu kuwa mbobezi
Lakini pili swala la machapisho kuwa cited bado inategemea na chanzo cha habari yako ambacho kililalia zaidi oline, kwa mazingira yetu ya kibongo

Pengine nikubaliane na wewe kwamba kupitia online Dr Tulia hajafanya vizuri sana, nakushauri jaribu kwenda mbali zaidi kwenye utafiti wako mkuu kutafuta data zingine zaidi ya online naamini utapata kitu na utakua katika kipimo kizuri cha kujua ubobezi wake

Kwa hiyo hajabobea Online .............
 
nmekuelewa mkuu Nzi umetoa elimu tosha juu ya ubobezi hasa katika sheria,pia umedhihirisha jinsi gani elimu ya bongo ilivyokumbatiwa kisiasa,binafsi nilidhani ana phd ya utawala/adminstration law kumbe ni social law. kuna haja ya kufumua mfumo wa elimu ya Tanzania ili kumuwezesha mhitimu kujithamini
 
Kwanza kabla ya kuanza kuelezea machapisho ya Dk. Tulia Ackson ulipaswa utueleze neno ubobezi kwako lina maana gani na kitu gani kinafanya binadamu akaitwa mbobezi katika sheria.

Jenga kwanza msingi wa hoja yako kabla ya kuanza kuelezea unachotaka kukichambua.

mkuu tafuta kamusi ya kiswahili
 
Mnamfagilia tu kwa maslahi yenu, sasa tusubiri bunge lianze
 
Back
Top Bottom