Ubinafsishaji: Mkapa alikosea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

Discussion in 'Great Thinkers' started by BAK, Jan 25, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Mkapa ajuta​

  • Ahuzunishwa wageni kuhodhi uchumi​

  na Mwandishi Wetu | Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, amesema anajutia kitendo chake cha kuliingiza taifa katika ubinafsishaji wa rasilimali bila ya kujiandaa kikamilifu na mabadiliko hayo.

  Mkapa alitoa majuto hayo katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) uliofanyika Zanzibar wiki iliyopita katika Hoteli ya Zamani Kempinski na kuhudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.

  Mbali ya Mbeki, viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale - Mwiru.

  Mmoja ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ambaye alizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kutokutajwa jina lake, alisema Mkapa alikiri kuwa sera ya ubinafsishaji haijamsaidia kwa kiwango kilichotarajiwa Mtanzania na badala yake wamegeuka wageni katika rasilimali zao.

  Chanzo hicho kilidokeza kuwa Mkapa alibainisha kuwa kukubali kwake sera hiyo kulikuwa na lengo zuri la kuwafanya Watanzania waondokane na lindi la umaskini kupitia uwekezaji utakaofanywa katika rasilimali zao.

  "Alituambia sera ya ubinafsishaji inamuumiza mno, kwani alipoikubali hakutarajia kama ingeweza kuwafanya wageni wawe na sauti katika rasilimali za taifa kuliko wazawa kama ilivyo sasa," kilisema chanzo hicho.


  Chanzo hicho kilibainisha kuwa Mkapa alifikia hatua ya kudai kuwa kama angepata nafasi ya kuwa kiongozi tena wa taifa hili angerekebisha sera ya ubinafsishaji haraka ili walau Watanzania waanze kufaidi rasilimali za nchi yao, badala ya kuwa mashuhuda wa wageni wanaoendelea kuneemeka na rasilimali za nchi.

  Alisema tatizo kubwa lililopo katika nchi za Afrika ni kutumia baadhi ya mambo wanayotakiwa kuyafanya na wafadhili au mifuko ya fedha, bila kuyafanyia tathmini ya kina ili kujua kama hayataleta madhara katika siku za usoni.

  "Mkapa alionyesha kujutia uamuzi alioufanya kwenye uwekezaji na aliweka wazi kuwa kama angeruhusiwa kurudi katika nafasi hiyo, basi jambo la kwanza kulirekebisha ni ubinafsishaji," kilisema chanzo hicho.

  Mkapa katika utawala wake alibinafsisha mashirika mengi ya umma, ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa bei ya chini, kitendo ambacho kilizua malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, pia alibinafsisha Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na mengine mengi, kiasi cha kuzua malalamiko mbalimbali ndani na nje ya nchi.


  Aidha, katika utawala wake pia alilalamikiwa kwa kuwapendelea wawekezaji wa kigeni kuliko wazalendo, hasa katika sekta ya madini na kuingia mikataba mibovu ambayo hadi sasa imekuwa mzigo mkubwa kwa taifa, sambamba na wawekezaji hao kupata misamaha ya kodi kwa kigezo cha kuwavutia.

  Kuingia mikataba mibovu huku ndiko kulikomfanya Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini na kutoa ushauri wa namna bora ya kushughulikia sekta hiyo.


  Majuto hayo ya Mkapa yanakuja huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge na wananchi wakitaka afutiwe kinga yake ili aweze kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yake akiwa ikulu.

  Katika utawala wake, Mkapa anadaiwa kutumia madaraka yake kuanzisha miradi mbalimbali inayomhusu, ama kwa kupitia familia yake au ndugu zake, ukiwemo ule wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao hivi karibuni wamiliki wake wametajwa hadharani kwa mara ya kwanza.

  Chagizo la kutaka kutolewa kinga limezidi kupata kasi baada ya waliokuwa mawaziri wake, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, kufikishwa mahakamani kwa kosa la kulisababishia taifa hasara ya sh bilioni 11 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya M/S Stewart.

  Kinga ya Mkapa inaweza kuondolewa kama Bunge litapiga kura ya kutaka kutengua kinga hiyo, lakini ni lazima hoja hiyo iungwe mkono na theluthi mbili ya wabunge wote.
   
  Last edited by a moderator: Jan 25, 2009
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Majuto ni mjukuu. Ananikumbusha mwalimu alivyosema angerudi madarakani angekataa mikopo yote yenye masharti! ...Politics!!!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Mwalimu aliona mbali alipohakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa mikononi mwa Watanzania badala ya wageni. Pia mara nyingi alikataa masharti mbali mbali ya IMF na WB ili tupatiwe misaada toka mashirika hayo yakiwemo kubinafsisha makampuni mbali mbali na kushusha thamani ya shilingi yetu.

  Wewe ulipoingia tu basi ukajifanya mjuaji na kuwakumbatia IMF na WB na chochote walichokwambia ufanye ukakifanya mara moja bila kujali athari yake kwa Taifa letu. Pamoja na Watanzania kukupigia kelele katika sera zako lakini hukusikia la jini wala la shetani. Ukawaleta makaburu wa Net Group bila kujali pingamizi la Watanzania dhidi ya makuburu wale na kuwalipa mishahara na marupurupu ya hali ya juu. Ukasaini mikataba isiyo na maslahi kwa Watanzania ya kuchimba madini yetu na kuifanya siri kubwa hata wabunge hukutaka waione. Ukanunua Rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi pamoja na Watanzania wengi kupinga manunuzi hayo. Ukatuona Watanzania hatustahili kumiliki chochote ndani ya nchi yetu, kila ulichobinafsisha uliwapa wageni.

  Ukajiuzia Kiwira katika mazingira ya kifisadi na kutuficha Watanzania. Ukauza nyumba za serikali kwa bei ya bure pamoja na kuwa Watanzania wengi tulipinga kuuzwa kwa nyumba hizo

  Ukatutukana Watanzania kwamba tuna wivu wa kike na kila aliye tajiri tunadhani ni mwizi. Ukawatukana waandishi wa habari wetu kwamba hawajui kuuliza maswali ni bora uuliwe maswali na wanahabari toka CNN, BBC na wengine wa nje.

  Sasa leo unaona sauti za kutaka kuondolewa kinga ili upandishwe kizimbani kujibu tuhuma za kifisadi dhidi yako zinazidi kuongezeka unatafuta sympathy kwa kujifanya unasikitika sera zako jinsi zilivyowamilikisha wageni uchumi wetu. Hupati sympathy yoyote toka kwa Watanzania wenye mapenzi ya kweli na nchi yao, labda mafisadi wenzio ndiyo watakaokupa sympathy.

  Mwisho turudishie Kiwira yetu pia utufahamishe Ikulu ulikuwa unafanya biashara na nani na ilikuwa biashara gani!? Na ujiandae kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma mbali mbali dhidi yako.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  zamani tulikuwa tunasema "gia ya kuingilia".. naamini hii ni mojawapo.., ya pili itakuwa ni kusikitikia wafanyakazi wa umma kujinufaisha kutokana na nafasi zao na atasikitika sana hawakuweza kusimamia maadili kwani waliamini kila mmoja ni mzalendo..
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jan 25, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mkapa angekuwa mkweli, angeshasimamama hadharani na kukemea maovu yaliyotokana na sera zake wazi wazi kama ambavyo Nyerere alikuwa akifanya. Badala yake yeye amenyamza kimya kimya na kuendelea kula faida ya sera zake.

  Kama kweli yeye ni kiongozi, basi akubali kuchukua adhabu itokanayo na makosa yake kama mfano kwa wengine; kuongoza maana yake ni kuonyesha njia.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Kama kweli anajutia maamuzi yake atwambie Watanzania nini kifanyike haraka sana ili kubadili hali iliyokuwepo badala ya kukaa kimya huku hali ikiendelea kuwa mbaya.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mgonja, Mramba, Yona wote wana kesi ya kujibu ya kutumia madaraka vibaya, wananchi tulilalamika sana kuhusu hii sera ya ubinafsishaji na matumizi yasio na lazima lakini majibu yalikuwa kama kula nyasi na tule.

  Mimi sioni kwa nini mkapa asiwe kwenye fungu moja na hao nilowataja hapo juu, kwa sababu hata Mwalimu aliyeanzisha hivyo viwanda na mabemki aliikemea sana hii sera ya ubinafsishaji hasa katika taasisi ambazo zilikuwa zinafanya vizuri (TBL, SIGARA, NBC NK). MZEE ILIMUUMA SANA NA KAMA TUNAKUMBUKA JINSI ALIVYOKIOKOA KIWANDA CHA URAFIKI PALE UBUNGO KISIENDE KWA WATU WALIOKUA TAYARI WASHAWEKA FEDHA ZAO KUKICHUKUA.

  KWA KWELI HAPA KWA MKAPA HAKUNA MSAMAA HUYU BWANA ANASTAHILI KUKILI MAMBO YAKE MBELE YA JAJI SIKU YA HUKUMU YAKE
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Anamimina chumvi kwenye majeraha aliyotuachia!
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Yote tisa, kumi hii habari ni hearsay. Kwa principle za journalism, huyo mwandishi kapata tip toka kwa mmoja wa wajumbe. Alitakiwa kufanya homework yake vizuri to seek attribution from competant authority, hata kama wasinge ongea. Other wise angetafuta collaboration toka kwa angalau wajumbe wengine wawili.

  Hizi news za single source has always leave a room for doubt maana zina hatari kubwa ya exegaration na Tanzania tuna bahati ya kuwa na wanasheria wachache, otherwise magazeti mengi yangeshafilisiwa long ago.

  Naombeni wana JF msinishambulie my comments has nothing to do na utetezi wa Mkapa, bali Journalism Professionalism and Ethics.
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Badala ya kusema anajutia wizi wake wa mali za umma, sasa eti anajutia uamuzi wake wa ubinfsishaji as if wabongo tumelala usingizi, unaona viongozi wetu wanavyotuona kwenye macho yao na mawazo yao finyu!

  - Huyu ni Kisutu's candidate sasa anajaribu ku-buy time na hizi nonesense za kujutia, buruza Kisutu tu akasemee yote kule sio vikao vya usiri usiri huko Kempisk, halafu anyamaze asubiri mbele ya sheria haya maneno yake yataishia kuvuruga ushaidi.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Pasco ni kweli ni hearsay, lakini tunaweza kufuatilia ili kuhakikisha je, kulikuwa na kikao kilichofanyika Z'bar kilichoandaliwa na UVCCM. Je, Thabo Mbeki hivi karibuni alikuwa Z'bar? kwa shughuli ipi? na je alihudhuria kikao cha UVCCM kilichofanyika Z'bar hivi karibuni? Je, Mkapa alikuwa Z'bar hivi karibuni? kwa shughuli ipi? Tukipata majibu ya maswali hayo ama tunaweza kuukaribia ukweli au kuzidi kuwa mbali nao.

  Inasikitisha (kama ni kweli) kumuona aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa wa nchi anaona nchi inadidimia kutokana na sera zake alipozipitisha alipokuwa madarakani, lakini hayuko tayari kuwaambia Watanzania sera zake zinaipeleka nchi pabaya na labda yafanywe mabadiliko makubwa kuhusu sera hizo ili kuwanusu Watanzania. Yuko radhi kuongea pembeni na wale aliowambia masikitiko hayo nao kuwa mabubu au kuzungumza kwa masharti kwamba majina yao yasitajwe. Huu ni uwendazimu wa hali ya juu!!!! Nchi inaangamia lakini bado viongozi wanaogopa kusema waliyoambiwa na Mkapa!! Kwa maana nyingine ni bora wakae kimya kuliko kusema hadharani na kuwanusuru Watanzania!!!!

  Pasco, si unakumbuka Dr Slaa alipotoa list ya mafisadi mbali mbali ndani ya chama na serikali. Wengi wakatoa vitisho kwa Dr kwamba watamfungulia mashataka kwa kuwachafulia majina yao kwa tuhuma nzito, lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kumfikisha Dr kizimbani.

  Sasa majina ya baadhi ya waliohudhuria kikao hicho yamewekwa hadharani. Basi ni wajibu wao kukanusha habari hii kama Mkapa hakutamka maneno hayo. Kukaa kwao kimya kuhusiana na habari hii ni ufisadi wa aina yake.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,
  Kusema kweli mimi Mh. mstaafu Mkapa kanishtua na kunifurahisha sana kwa hotuba hiyo... Hakika kwa mara ya kwanza naweza kumpa hongera kwa kitendohicho pamoja na kwamba amefanya mengi mabaya ambayo naamini kuwa ilikuwa makusudi kabisa...

  Ni mwanzo mpya, tuwe wepesi kusoma makosa na kuweza kuyarekebisha kwani maneno ya Mkapa yanarudia usemi wangu toka mwaka 2000 kuhusiana na Ubinafsishaji.. Niliwahi kusema kwamba Mkapa anajua vizuri sana akiwa balozi hapa Canada na US jinsi wenzetu walivyofanya transition ya Ubinafsishaji kwa hatua.. Kuna sekta za nguzo za uchumi wa nchi ambazo hadi leo miaka zaidi ya 200 bado zipo mikononi mwa serikali zikitoa cotracts kwa watu binafsi tena wazawa..

  Kulikuwepo na vijana kina MgonjwaUkimwi, mwalimu Augustine Moshi na Tito Mwiula na wengine tulipishana sana kimawazo ktk hoja zinazohusiana na Ubinafsishaji, bahati mbaya hawakuweza kuona mbali kutofautisha mazingira yetu na nchi ambazo tayari ni Mabepari.
  Niliyasema mabaya yote yanayotokana na kutojiandaa na kuuza mali hizi hata kutunga tungo za sisi kuwa wapangaji ktk nchi yetu wenyewe..
  Hoja za uzawa na kadhalika zote hizi zilitazamwa kwa jicho la ubaguzi zaidi ya reality yenyewe. Nikatoa hata mifano ya ndoa mabyo watu huchagua mchumba na pengine kupendelea mchumba wa kabila au dini yake kutotazamwa kama ni ubaguzi isipokuwa ndoa ni hatua moja zaidi ya mapenzi..
  Leo hii tunajutia, na Mkapa kama kiongozi mstaafu nampa hongera KUKUBALI MAKOSA kama mwalimu aliyekubali kushindwa Ujamaa..na hakika kwa maneno yake ya kuungama ningependa kufahamu kama yupo tayari wananchi kumhukumu kwa makosa yake!..Ni mwanzo mzuri sana kwetu sisi kujirekebisha, and this time kiburi cha viongozi kutawala kipatiwe sheria inayoshirikisha wataalam na bunge maalum la Uchumi ktk kupitisha sera zenye maamuzi mazito na costly kama haya..
  Hongera sana Mh. Mkapa sii kwamba nakuchukia au nafanya wivu ktk hoja zangu isipokuwa huwa nahoji uzalendo wako kwa taifa letu..Leo umekubali makosa na hakika imenifurahisha sana!
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Pasco , pamoja na kuwa inawezekana kuwa ni hearsay laikini habari imeandikwa na haijakanushwa. Lets wait and see.

  Hata hivyo inaelekea the sentiments are geunine hata kama hazikuwa for public consumption.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pasco,

  Hiki ki-habari cha TanzaniaDaima ni udaku mtupu. Mkapa ana soo la kubinafsisha mgodi na partner in crime wake Daniel Yona ana kesi mahakamani kuhusiana na haya haya ma hanky-panky ya dealings za serikali na wawekezaji, hawezi kujitia kitanzi kukiri makosa saa hizi.

  Sio principle za journalism tu, hata za stori za mtaani haziendi hivyo. Hivi tukiwa tunamtafuta Juma atujibu kuhusu mali zetu halafu tunakuja kuambiwa kuna fulani kasema Juma kakiri kosa, hatutataka kujua huyo fulani anaesema Juma katubu ni nani, na nani mwingine alisikia wakati anatubu? Halafu alipokubali makosa alisema nini kuhusu mali zetu going forward? You know?

  Halafu ki-habari kina misrepresent ukweli kwa kusema pressure ya kumshitaki Mkapa imeongezeka. Kila kukicha tunasikia padri so and so mbunge huyu na yule wanasema let this Mkapa character alone, sasa hiyo pressure iko wapi? Na Pinda keshapayuka kwamba it's a complicated process.

  Kinga yenyewe walivyoiongelea ni misrepresentation tupu. Hakuna sehemu kwenye Katiba paliposema Wabunge wanaweza kuondoa kinga. Itabidili Wabunge waandike kipengele hicho cha Katiba upya, na hiyo ndio itahitaji theluthi mbili za wabunge, tena inabidi ipatikane kote Zanzibar na Bara separately.

  Halafu Pasco, notice kwamba kwenye misingi journalism, ilibidi pale kwenye paragraph ya kwanza, au ya pili at the latest, waseme kwamba wanaripoti based on stori ya kuambiwa na anonymous source. Walivyoiweka ni kama wao Tanzania Daima ndio wanaripoti wakati hawana uhakika. Wakishitakiwa watasema sisi tumeambiwa na mtu, lakini hapa wameitengeneza kuwa-fool unwary readers kama wana uhakika vile. Wadaku.

  Halafu, notice vi-taarifa ambavyo hawana uhakika hawatoi jina la mwandishi, wanavunja cardinal rule of journalism, inayotakiwa kuleta credibility na accontability.

  Eti gazeti linaripoti kwa kuambiwa na mjumbe mmoja, udaku, uzushi, vilaza wakutupwa nje ya press room.
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkapa hakuwahi kuwa a serious politician, na kila aliposhauriwa ushauri mwingi wa kisiasa alikubali mbele ya waliompa ushauri, lakini alipotoka tu usoni mwao akafanya anayotaka ambayo sasa yanamgeuka,

  - Sasa kama unajua vizuri siasa ukiaiingalia hii habari utaona imetengenezwa na washauri wake wapya wa siasa, yaani kufanya kikao cha siri na kuvujisha habari za kikao kwa ajili ya kumsafisha Mkapa, kwamba uporaji wake wa mali za wananchi sio crime by the law ila ilikuwa ni makosa ya yeye kukubali ubinafsishaji bila kuuelewa vizuri, which is pure nonesense!

  - Sasa the catch ni kwamba wananchi tukilia sana kua hii habari ni foolish, basi baadaye wavujishaji watajitokeza na kusema hii habari sio ya kweli, lakini kukiwa na sympathy nyingi kwa Mkapa, kama ambavyo mwenzetu mmoja hapa alivyoanza tayari basi tutaletewa habari zaidi za kikao hicho za kumsafisha zaidi Mkapa,

  Tunawaambia wavujishaji kwamba tu waste of time, huwezi safisha fisadi mpaka mbele ya sheria tu! Hivi mmeungundua kuwa mafisadi wote huwa ni waoga sana wa sheria, maneno mengi pembeni lakini hakuna wa kutangulia wkenye sheria!
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mimi sio mwanasiasa, lakini naamini;

  moja ya sifa za kiongozi makini aliyepewa dhamana ya kuongoza, ni kutumia uzoefu, busara na elimu yake kufanya maamuzi anayoamini ni sahihi, kwa wakati muafaka na kwa matarajio mema.

  ...Kusema "...samahani!" inamaana hakutumia elimu yake, busara au uzoefu aliokuwa nao?

  Mwl Nyerere mpaka anakwenda Kaburini hakupata kujutia Azimio la Arusha wala Alhaj Ali Hassan Mwinyi hajajutia azimio la Zanzibar.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FMES,

  Mimi nachukulia kama kweli habari hii imenukuliwa toka mkutano huo... habari za IF au haiwezekani huwa sina muda zaidi wa kujadili kwani kinachotakiwa hapa ni kutazama mbele.

  Kama kweli Mkapoa amekubali makosa namshukuru sana, for the first time amekubali kutupelka pabaya na ushahidi tosha kwetu kumshtaki na pengine kumhukumu. Wale wote waliokuwa nyuma yake watatafuta njia nyingine ya kutokea lakini mbele ya haki huwezi kuomba sympathy za watu isipokuwa mahakama ndiye mwamuzi wa haki iliyovunjwa.

  To me sio lazima Mkapa afungwe jela isipokuwa kurekebisha mikataba, kurudisha mali zote ambazo zimetolewa kiholela ni mwanzo mzuri sana. Tusipoteze sana muda kudai Kisutu tukasahau kwamba nchi hii inatakiwa kwenda mbele na sio kusuasua tukitegemea matokeo ya Kisutu kuwa ndio suluhisho la uchumi wetu.

  Ya Kisutu yatakwenda na sheria, wakati huo huo uchumi wetu unapatiwa marekebisho muhimu sana kwa maendeleo yetu..
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mbu,

  Azimio la Arusha halikuwa na makosa isipokuwa baadhi ya vipengele na utekelezaji wake sawa na hilo la Zanzibar au Ubinafsishaji.

  Hakuna mtu anayemlaumu Mkapa kwa sera ya Ubinafsishaji isipokuwa ni vipengele ambavyo vilivunja maadili na miiko ya Uongozi, pia hatua zilizochukuliwa ndani ya sera hiyo..vile vile kwa Mwinyi na Nyerere.

  Acha huyo Mkapa, hata mimi naweza kwenda kaburini nikiunga mkono sera ya Ubinafsishaji lakini sio kama tulivyofanya sisi!..
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wooow! Mkuu Bob, slow down bro, kiongozi anayejutia makosa yake alipokuwa kwenye uongozi wa wananchi hujitokeza hadharani mbele ya wale wananchi aliowakosea na maamuzi yake anayoyajutia na kuwaambia wazi mbele yao,

  - Sio kujificha kwa siri huko Kempisk na anaofanana nao, yaani kina Msekwa
  na Kingunge, halafu kuvujisha this nonesense kwetu wananchi aliotukosea sidhani kwamba that is what Mwalimu did, na by the way ni wapi hapo hasa ambapo Mwalimu alikubali makosa yake ya Ujamaa jamaa?
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280

  Ahsante sana Mkandara. Nakubaliana na wewe. Na nitakuwa mstari wa mbele kumpigia makofi Mkapa kama akiamua kuja hadharani na kutamka kwamba sera zake zimeuweka uchumi wa Tanzania mikononi mwa wageni kitu ambacho ni kasoro kubwa sana kwa usalama na maendeleo ya nchi yetu.

  Pia awe mstari wa mbele kusema hadharani nini kifanywe ili kurekebisha hali hiyo na kuurudisha tena uchumi wa Tanzania mikononi mwa Watanzania badala ya kukaa kimya au kuongea pembeni wakati anaona nchi inaelekea pabaya kutokana na uchumi kushikiliwa na wageni.
   
Loading...