- Thread starter
- #41
Ukishakuwa na jawabu kibindoni mwako, halafu ukataka watu wakupe jawabu inatia uvivu sana.
Sina jawabu kwasababu nataka kueleweshwa ki-undani zaidi kuna ubaya hapo mkuu au?
Ukishakuwa na jawabu kibindoni mwako, halafu ukataka watu wakupe jawabu inatia uvivu sana.
Topical mimi naunga mkono msingi wa hoja yako kwa asilimia miamoja! Kimsingi watu wamebebwa na mkumbo tu kwamba mswada ni mbaya lakini ukiwataka wabainishe ubaya wake ndo kama hivi wanalete maswali ni misemo ya wahenga! Niliwahi kusema hapa kuwa hawa wanaharakati wanatupotosha watu wakabisha kwa ushabiki, kisa wameshalishwa sumu! Watanzania tuwe makini tusiweke rehani uwezo wetu wa kudadavua mambo yanayotuhusu!
Matatizo ya muswada huu kama ulivyo, samahani kaka nakujibu kwa kutumia akili zako.....
a)Unampa madaraka makubwa rais ambayo tunayapinga muda wote, hata kama kukiwa na bunge la katiba bado utampa rais mamlaka ya mwisho ya kuamua nini kifanyike katika katiba yetu......ambapo hatutaki yeye awe na mamlaka nayo kama mtu binsfsi. (means tunataka taasisi inayojitegemea)
Kumpa mtu mmoja madatraka makubwa hapa mwanzo ni kuharibu mfumo wa kutupatia katiba na katiba yenyewe kabisa.
b)Haimaanishi kwamaba hata kama muswada ni mzuri basi hauna haki ya kwenda kwa wananchi, bado watanzania walikuwa na haki ya kuujadili hata kama ni mzuri kiasi gani.
c)Mswada haujachumbua vyema nafasi ya Tanganyika kama ulivyojidadavu kuhusu Zanzibar. Zanzibar wameweza kujadili mambo yao na wakaafikiana vivyo hivyo na sisi watanganyika pia......muswada ulipaswa kuchambua nafasi ya Zanzibar na Tanganyika kwa usawa. Si kwa vile wewe ni mkubwa basi ukipigwa na mdogo usisema....atleast unamkanya.
d)Haujaainisha vyema jinsi makundi mambilibmali ya kijamiii yatakavyo husika, kwamfana Tz si Dodoma,DSM na Zanzibar.
kama bado hujaelewa dhen ntafute kwa muda wako.......napatikana Kigogo Luhanaga mkuu.
Tunachoelewa sisi ni kwamba muswada uliopo ni ule ule ulokuja mara ya kwanza kwa kiingereza sasa umerudishwa kwa kutafsiriwa tu kuja lugha ya kiswahili kwa sababu hilo lilikuwa moja ya maswala mengi yaliyokataliwa.. Sasa kinachotushanga kulikuwa na vikao kibao ambavyo vimefanyika na vinaendelea kufanyika ktk kuujadili muswada huo na kuuboresha lakini mengi yaliyojadiliwa leo hayana maana tena..Huo muswada wenyewe uko wapi? Watu wanajadili hewa tu.
Huo muswada wenyewe uko wapi? Watu wanajadili hewa tu.
Ndio maana nikasema mko hapa mnajadili hewa tu. Hujausoma? Sasa utajadilije kitu hujakisoma? Na utanambiaje mimi nikausome wakati we mwenyewe hujui unajadili kitu gani kwenye muswada? Wabongo sijui tukoje.Nakushauri uendelee kuutafuta,then uusome, mie sijausoma ila nimeusikia in kwa kifupi
Tropical, Mkuu unajua unauliza maswali kama hujui ama unauliza kwa udadisi?.. Hivi nikuulize wewe lini mtumwa asimtumikie bwana wake.... Iliona wapi..Kwa nini sisi wananchi tusitoe jukumu hilo la rais kuunda tume ama bunge ama wote ama taasisi ya katiba ama lolote lile libadilishwe ikiwa yeye rais anafahamu kwamba sisi ndio waajiri wake. Na rais ajaye atalinda kile tulichomkabidhi..
Na labda nikuulize wewe nambie Kiongozi yeyote aliyechaguliwa na rais ambaye sii mwanaCCM, toka NEC, UWT na kwingineko.. Na sababu gani zimetokana na uchaguzi huo?
Pili, nambie tume yeyote ya rais ambayo imeweza kuwakilisha taarifa safi na ikitendewa haki kama ilivyowakilishwa..Hakuna hata hiyo ya Richmond imefukiwa kukidhi maslahi yao waajiri, leo bado unataka wananchi tuwe na imani na muswada ambao tunajua fika kwamba haukidhi mahitaji yetu.
Tatu, Kwa nini ktk ibara ya tatu rais kaweka masharti ktk baadhi ya sehemu ziheshimiwe zisiguswe, yeye nani inapofikia swala la katiba mpya kama sii kutuonyesha kwamba katiba itaundwa kwa mapenzi yake (chama) na sii ya Kitaifa..
Nne, Kwa nini yeye ndiye amchague katibu na sii tume yenyewe kuchagua viongozi na makatibu wake ambao watakuwa huru.. na watawasilisha taarifa ya tume baada ya kumaliza na sio mtu alokuwa karibu naye...
Tano, katika katiba ya taifa kundi la baraza la Mapinduzi haliwezi kuwa exceptional wakati kuna vyama vingi na tumeungana. Haya maswala ya Uuwiano ktk tume hayajengi usawa wa mawazo bali kuridhisha watu. Mfumo ule ule wa kiutawala wa kuleta uuwiano wa waislaam, wakristu, Uzanzibar na Ubara ndio tunataka kuuvunja. Tunataka kuwepo serikali tatu na kaa atachagua tume atahakikisha swala hili haliguswi kama alivyoeleza..Yeye bado anafikiria mawazo ya mgawanyiko kutokana na shinikizo pengine la Baraza la Mapinduzi akini nchi hizi zimeungana na zina vyama vingi.. Baraza la Mapinduzi linaweza kujenga na wazee wa Zanzibar bila kujali wanatoka chama gani..
Kifupi tunataka TUME HURU - Je, tutaipata vipi ndio liwe swali na sii vinginevyo! Soma tena muswada halafu nambie kama hiyo itakuwa tume huru.
VICHEKESHO VINGINE HUHITAJI KWA GENIUS KUONA HUU UTUMBO.!!!!
1. Rais (kwa kushauriana na mwezake wa Znz) ndiye atakaye pendekeza tume ya kukusanya maoni.
2. Rais ndiye atakaye tengeneza hadidu za rejea za tume. (Hairuhusiwi kujadili nje ya hizi hadidu za rejea
na kwa vile tushamsikia akisema mambo kama Muungano, Madaraka ya rais yashawekewa mipaka)
3. Tume ikimaliza kukusanya maoni inarudisha kwa rais ambaye atafanya marekebisho kwa kadri ATAKAVYO ONA INAFAA.
4. Tume ya uchaguzi ndo itasimamia mchakato wa kukusanya maoni. Mwenyekiti ni mteule wa rais
5. Bunge la katiba lina wabunge zaidi ya 2/3 wa CCM ambao kama inavyofahamika wanatumikia chama hence mwenyekiti wake ambaye ni rais.
e.t.c
List unaweza itengeneza ni ndeeeefu sana. HUU NI MZAHA!!!
Mpaka hapo sijui hiyo ni KATIBA ya wananchi au ya RAIS!!!!
pls quote sentensi nzimaaaaaaaandio maana nikasema mko hapa mnajadili hewa tu. Hujausoma? Sasa utajadilije kitu hujakisoma? Na utanambiaje mimi nikausome wakati we mwenyewe hujui unajadili kitu gani kwenye muswada? Wabongo sijui tukoje.
naomba nieleweshe wewe uliyona kasoro zake say a, b, c, d...na pengine ulitaka iwekwe nini badili yake?
3. Nimesema tukiacha malumbano ya kusomwa mara ya kwanza na ya pili maana nataka nifahamu tatizo la muswada kama ulivyo una shida gani kwa wananchi kupata katiba nzuri??
Kwa vile kanuni inataka mswada usomwe mara ya kwanza na mara ya pili, kwa nini serikali ivunje kanuni hiyo? Je raia nao tukivunja shera za nchi kwa makusudi kama serikali inavyofanya itakuwaje?
Tunachoelewa sisi? Wewe na nani, jiongelee mwenyewe. Tunaenda na facts, sio "tunachoelewa sisi." Watu hawafungui muswada badala yake wanajadili makisio ya kubahatisha bahatisha tu.Tunachoelewa sisi ni kwamba muswada uliopo ni ule ule ulokuja mara ya kwanza kwa
Utanipaje lecture ya kujua kusoma na kuelewa wakati wewe mwenyewe umekiri muswada hujausoma? Kituko kikubwa sana. Na huwezi kusema nina "twist maneno ya watu," kuna rekodi ya kila maneno ya mtu hapa, uta twist vipi?...mie siko kwenye huo umbea na kutwist maneno ya watu... tafadhali kabisa tafadhali kaka/dada... kama wewe ni msomi unajua namna ya kusoma na kuelewa
Nakushauri uendelee kuutafuta,then uusome, mie sijausoma ila nimeusikia in kwa kifupi