Ubaya wa Muswada wa katiba kama ulivyo?

1. Process ya kidemokrasia ingekuwa kivipi kwa mfano? ambayo unafikiri haitakuwa ya kidikteta??

2. Zanzibar kupewa nafasi kubwa inainyima vipi Tanganyika haki zipi? kwa mfano??? lipi Tanganyika itaikosa??

3. Nimesema tukiacha malumbano ya kusomwa mara ya kwanza na ya pili maana nataka nifahamu tatizo la muswada kama ulivyo una shida gani kwa wananchi kupata katiba nzuri??

nadhani una mtindio kwa maana nyingine Topical afya ya ubongo wako ina shida.
 
Kwanza umesahau kuwa rais ni taasisi siyo mtu??

Pili hujatoa unafikiri alternatives ni ipi? maana kila alternatives ina weaknesses zake..

Kwahiyo unaona sawa taasisi moja iunde katiba ya nchi peke yake?? Kuhusu alternative sicho alichotaka kujua mtoa mada!!!
 
Ukiacha hoja za TL kwamba haukujadiliwa (i.e. mara ya kwanza na pili), naomba kwa dhati kabisa ubaya wa muswada huo kama ulivyo sasa, na pengine utaratibu gani ndio ungeleta katiba nzuri?? kwanini unafikiri kwamba kama ilivyo haitaleta katiba nzuri kwa nchi???

Mkuu, nimefuatilia kwa umakini mkubwa hoja zako kuhusu swali ulilouliza, hongera. Kabla nami sijachangia naomba nikuulize, je kwako wewe unafikiri kuna umuhimu wa kuwa na katiba mpya kwa Tanzania?
 
Mkuu shukran kwakuwa ni wewe pekee ndiye uliyeweza kunielewesha..

Moja: wananchi watapataje wajumbe wa tume (utaratibu gani) ambao utakidhi mahitaji ya kila mtanzania asilalamike? utaratibu gani utumike? besides urais ambayo itaepuka biaseness i.e. mtumwa na mtwana unayoisema??

Mbili: Hoja yako ya pili inatokana na historia ya tume kutofanya vizuri inaweza kutosha kuwa sababu maana itaonekana kama unazugumzia wakati ujao..itatokea?? kwanini tusimpe rais benefit of dought

tatu: Hilo la masharti ni kero kubwa sana, kuweka mipaka ya mijadala ni tatizo la msingi ambalo linahitaji kelele za kutosha tuko pamoja..

nne: Hilo la uteuzi linaendena na hoja ya kwanza system gani unafikiri ni bora kwa mazingara yetu, nionavyo mimi ukikubali kupeleka bungeni ni tabu tupu, ukifanya kutangaza ili watu waombe process nzima itakuwa corrupt na system nzima wanaweza kuwonga hata nape au tambwe akawa katibu ...

tano: hiyo tano sijakuelewa kwa zanziba kwenye, muungano lazima iwe na iko say kama nchi..bila kujali ukubwa wake.. (acha uwongo) sheria kama ilivyo inakataza watu kuvunja muungano lakini inaruhusu kuongelea muungano ikiwemo muundo wa serikali tatu ambao CUF na Chadema wako na proposal hiyo nafikiri ultimately tutakuwa na serikali tatu..

Mkuu TUME HURU ni very subjective term tusema at least fair representation...

Kwa hiyo Tropical umeona sasa umuhimu wa muswada hule kusomwa mara ya kwanza ili hayo maswali yako yaweze kupatiwa majibu? wewe mwenyewe sasa umejikuta automatically umeanza kujadili upungufu uliomo kwenye muswada huo ambao ulijifanya huelewi kitu ,Je kama utabaki kama ulivyo na upungufu huo ambao wenye akili tumebaini itakuwaje?Katiba hitakuwa ya kikwete na ukoo wake?
 
Baada ya kuufuatilia huu mjadala kwa ukaribu nimegundua kuwa swala linalojirudia kwa wanaoupinga mswada ni fursa aliyopewa Rais ya kufanya maamuzi juu ya process ya ukusanyaji maoni. Sijaona lalamiko lingine, labda wenzangu mnisaidie kuliona. Kwa hiyo tunaweza kusema kwa kifupi tu kuwa WANAOPINGA MSWADA HAWANA IMANI NA RAIS.
Sasa labda nilimodify swali la Topical bila kuanzisha thread nyingine.

Je, wanaopinga mswada hawana imani na Rais Kikwete au hawana imani ni taasisi ya Urais? in other words, je wanadhani Rais Kikwete hatafanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa au wanadhani Rais yeyote yule hawezi kufanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa katika swala la katiba?

Labda tukienda hivi tutafika wakati tutaelewana, hata hivyo swali la Topical la kutoa alternative method ni muhimu lijibiwe kwani siajaona aliyeattempt kulijibu.
 
Mkuu shukran kwakuwa ni wewe pekee ndiye uliyeweza kunielewesha..

Moja: wananchi watapataje wajumbe wa tume (utaratibu gani) ambao utakidhi mahitaji ya kila mtanzania asilalamike? utaratibu gani utumike? besides urais ambayo itaepuka biaseness i.e. mtumwa na mtwana unayoisema??

Mbili: Hoja yako ya pili inatokana na historia ya tume kutofanya vizuri inaweza kutosha kuwa sababu maana itaonekana kama unazugumzia wakati ujao..itatokea?? kwanini tusimpe rais benefit of dought

tatu: Hilo la masharti ni kero kubwa sana, kuweka mipaka ya mijadala ni tatizo la msingi ambalo linahitaji kelele za kutosha tuko pamoja..

nne: Hilo la uteuzi linaendena na hoja ya kwanza system gani unafikiri ni bora kwa mazingara yetu, nionavyo mimi ukikubali kupeleka bungeni ni tabu tupu, ukifanya kutangaza ili watu waombe process nzima itakuwa corrupt na system nzima wanaweza kuwonga hata nape au tambwe akawa katibu ...

tano: hiyo tano sijakuelewa kwa zanziba kwenye, muungano lazima iwe na iko say kama nchi..bila kujali ukubwa wake.. (acha uwongo) sheria kama ilivyo inakataza watu kuvunja muungano lakini inaruhusu kuongelea muungano ikiwemo muundo wa serikali tatu ambao CUF na Chadema wako na proposal hiyo nafikiri ultimately tutakuwa na serikali tatu..

Mkuu TUME HURU ni very subjective term tusema at least fair representation...
Kwanza kabisa unazungumza ukiwa ndani ya kabati la uchama, ukiondoka humo unaweza kabisa kuja na mawazo mazuri kuliko haya...

1. Wananchi watapataje Tume na ni utaratibu gani?..
Je, wewe unaujua utaratibu atakao tumia rais hadi umekubali bila kuuliza? Kuna vikao vingapi vinafanyika juu ya swala hili.. Nilichosema mimi ni jukumu la wananchi kupendekeza tume itapatikana vipi. Kama wananchi watachagua rais aichague, bunge, rais na wabunge, kamati za bunge, wajumbe toka mikoa yote, au Taasisi za ndani na nje yote haya ni majukumu ya wananchi wenyewe kama ambavyo rais atashauriwa kuichagua hiyo kamati . Hatuwezi kuikabidhi future ya nchi yetu mikononi mwa mtu mmoja as if yeye ndiye founder wa Tanzania - Huu utakuwa ni Udikteta.

2. Kwa nini tusimpe rais benefit of the doubt?
Je, na kwa nini isiwe wananchi usiwape wewe benefit of the doubt!.. Tulikotoka hatuwezi kuanza na hatua ile ile. Mchora ramani akikosea uchoraji wa hata kibanda cha kuku ataweza vipi chukua mamlaka ya ujenzi wa nyumba kubwa ili hali mwenye mali ndiye mwenye mamlaka ya kuchagua ramani itajengwa na nani?.. Wewe unataka mwajiriwa ndiye awe na mamlaka ya kuchagua mtu mwingine wa kutucholea kwa sababu yeye hawezi basi tumpe jukumu la kutuchagulia.

3. Hilo umelikubali nadhani ni tosha kurudisha muswada bungeni...

4. System nzima ni corrupt?.. then kwa nini unadiriki kuwakabidhi mamlaka hayo bila ya kinga yoyote?
Huwezi kusema system nzima ni corrupt ikiwa wapo watu nje ya system (out of the box) wanaopinga Katiba iliyopo ambayo kwa mwenye kuelewa atakwambia iliyopo ni katiba ya chama kimoja. Ni katiba ya Kijamaa ambayo athari zake ni UDIKTETA, na athari hizo hadi leo hii tunazikumbuka na zinatuburuza, sasa leo tumeingia Ubepari na athari zake ni UFISADI tumeshindwa kuweka miiko na maadili yanayoendana na mfumo huu kwa kudhania kwamba Ubepari ndio suluhisho la Ujamaa kiuchumi..Kwa hiyo katiba yetu leo imebeba Udikteta na Ufisadi kwa pamoja na ndio maana tunakwisha kijamii...

System haiwezi kuwa corrupty ikiwa tutaandaa utaratibu sisi wenyewe. Mamlaka tutayatoa sisi na tume itakuwa answerable kwa wananchi na kwa kila hatua ya majadala tena tunaweza wafungia chumbani (Bungeni) kama Jury wanapotakiwa kujadili maamuzi ya hukumu. Na rais kama Judge atasubiri kisha kuwauliza wamefikia makubaliano.. Na hayo makubaliano yatasomwa kitaifa kisha ammendment zinaweza kufuatia baadaye.

5. Nachosema mimi Zanzibar ni nchi na hakika lazima iheshimiwe lakini haiwezekani Baraza la Mapinduzi (ASP au CCM) ndio lenye mamlaka juu ya Zanzibar wakati nchi hiyo ina vyama vingi. Ebu fikiria kitu kimoja sisi tuwe tumewekewa sharti la kwamba maswala yote ya Tanganyika yatashughulikiwa na kamati kuu ya CCM.. Hii inakupa picha gani?.. Baraza la Mapinduzi livunjwe na liundwe baraza jingine ambalo halitahusisha chama kimoja kwa sababu hawa ndio waliompiga vita Salim asisimame Urais na Seif kuambiwa hataitawala Zanzibar. Maneno haya yanatakiwa kusemwa na wananchi wapiga kura...

Tunataka TUME HURU ndio neno la kupinga muswada huu... linajieleza lenyewe sidhani kama tunahitaji maelezo zaidi.
 
Mkuu, nimefuatilia kwa umakini mkubwa hoja zako kuhusu swali ulilouliza, hongera. Kabla nami sijachangia naomba nikuulize, je kwako wewe unafikiri kuna umuhimu wa kuwa na katiba mpya kwa Tanzania?

Yes naamini kuna umuhimu wa katiba mpya Tanzania, na ninatamani yafuatayo:

1. Serikali tatu (muundo wa muungano)
2. Idadi ya wizara fixed kwenye katiba na mawaziri wasiwe wabunge
3. Serikali ya majimbo (regional goverments) ambapo mkuu wa mkoa anachaguliwa na wananchi
etc
 
Kwanza kabisa unazungumza ukiwa ndani ya kabati la uchama, ukiondoka humo unaweza kabisa kuja na mawazo mazuri kuliko haya...

1. Wananchi watapataje Tume na ni utaratibu gani?..
Je, wewe unaujua utaratibu atakao tumia rais hadi umekubali bila kuuliza? Kuna vikao vingapi vinafanyika juu ya swala hili.. Nilichosema mimi ni jukumu la wananchi kupendekeza tume itapatikana vipi. Kama wananchi watachagua rais aichague, bunge, rais na wabunge, kamati za bunge, wajumbe toka mikoa yote, au Taasisi za ndani na nje yote haya ni majukumu ya wananchi wenyewe kama ambavyo rais atashauriwa kuichagua hiyo kamati . Hatuwezi kuikabidhi future ya nchi yetu mikononi mwa mtu mmoja as if yeye ndiye founder wa Tanzania - Huu utakuwa ni Udikteta.

2. Kwa nini tusimpe rais benefit of the doubt?
Je, na kwa nini isiwe wananchi usiwape wewe benefit of the doubt!.. Tulikotoka hatuwezi kuanza na hatua ile ile. Mchora ramani akikosea uchoraji wa hata kibanda cha kuku ataweza vipi chukua mamlaka ya ujenzi wa nyumba kubwa ili hali mwenye mali ndiye mwenye mamlaka ya kuchagua ramani itajengwa na nani?.. Wewe unataka mwajiriwa ndiye awe na mamlaka ya kuchagua mtu mwingine wa kutucholea kwa sababu yeye hawezi basi tumpe jukumu la kutuchagulia.

3. Hilo umelikubali nadhani ni tosha kurudisha muswada bungeni...

4. System nzima ni corrupt?.. then kwa nini unadiriki kuwakabidhi mamlaka hayo bila ya kinga yoyote?
Huwezi kusema system nzima ni corrupt ikiwa wapo watu nje ya system (out of the box) wanaopinga Katiba iliyopo ambayo kwa mwenye kuelewa atakwambia iliyopo ni katiba ya chama kimoja. Ni katiba ya Kijamaa ambayo athari zake ni UDIKTETA, na athari hizo hadi leo hii tunazikumbuka na zinatuburuza, sasa leo tumeingia Ubepari na athari zake ni UFISADI tumeshindwa kuweka miiko na maadili yanayoendana na mfumo huu kwa kudhania kwamba Ubepari ndio suluhisho la Ujamaa kiuchumi..Kwa hiyo katiba yetu leo imebeba Udikteta na Ufisadi kwa pamoja na ndio maana tunakwisha kijamii...

System haiwezi kuwa corrupty ikiwa tutaandaa utaratibu sisi wenyewe. Mamlaka tutayatoa sisi na tume itakuwa answerable kwa wananchi na kwa kila hatua ya majadala tena tunaweza wafungia chumbani (Bungeni) kama Jury wanapotakiwa kujadili maamuzi ya hukumu. Na rais kama Judge atasubiri kisha kuwauliza wamefikia makubaliano.. Na hayo makubaliano yatasomwa kitaifa kisha ammendment zinaweza kufuatia baadaye.

5. Nachosema mimi Zanzibar ni nchi na hakika lazima iheshimiwe lakini haiwezekani Baraza la Mapinduzi (ASP au CCM) ndio lenye mamlaka juu ya Zanzibar wakati nchi hiyo ina vyama vingi. Ebu fikiria kitu kimoja sisi tuwe tumewekewa sharti la kwamba maswala yote ya Tanganyika yatashughulikiwa na kamati kuu ya CCM.. Hii inakupa picha gani?.. Baraza la Mapinduzi livunjwe na liundwe baraza jingine ambalo halitahusisha chama kimoja kwa sababu hawa ndio waliompiga vita Salim asisimame Urais na Seif kuambiwa hataitawala Zanzibar. Maneno haya yanatakiwa kusemwa na wananchi wapiga kura...

Tunataka TUME HURU ndio neno la kupinga muswada huu... linajieleza lenyewe sidhani kama tunahitaji maelezo zaidi.

Umetoa maelezo mengi sana lakini umeshindwa kueleza kasoro iliyopo zaidi ya kulalamikia mamlaka ya raisa ambapo vilvile umeshindwa kueleza better well coordinataed and effective alternative..

Unatumia sana sisi wananchi na tume huru bila kusema watu milioni 40 hawawezi kukaa na kuandika katiba.. tume inateuliwa ili ipatae maoni yake kuna tatizo gani hapo? toa alternative and how it will work otherwise utakuwa sana na politicians..assume wewe uko kwenye "operation side" what are the options ambazo ni nzuri lakini si lazima ziwe zinawafurahisha wote hasa wanasias??
 
Ukiacha hoja za TL kwamba haukujadiliwa (i.e. mara ya kwanza na pili), naomba kwa dhati kabisa ubaya wa muswada huo kama ulivyo sasa, na pengine utaratibu gani ndio ungeleta katiba nzuri?? kwanini unafikiri kwamba kama ilivyo haitaleta katiba nzuri kwa nchi???

Wewe ungetueleza kwanza maruri uliyoyaona kisha na sisi tuanzie hapo kuchangia.
 
Haya sasa kesi ya kuonana na rais imeisha na taarifa imetolewa, kwa hiyo kama mnataka jadilini mapungufu ya muswada kama ulivyo ili hatimaye uende bungeni kwa marekebisho..short of that "muswada ni mzuri" lakini si kwamba hauna kasoro kwasababu ni kawaida kwa kazi wanadamu..
 
Umetoa maelezo mengi sana lakini umeshindwa kueleza kasoro iliyopo zaidi ya kulalamikia mamlaka ya raisa ambapo vilvile umeshindwa kueleza better well coordinataed and effective alternative..Unatumia sana sisi wananchi na tume huru bila kusema watu milioni 40 hawawezi kukaa na kuandika katiba.. tume inateuliwa ili ipatae maoni yake kuna tatizo gani hapo? toa alternative and how it will work otherwise utakuwa sana na politicians..assume wewe uko kwenye "operation side" what are the options ambazo ni nzuri lakini si lazima ziwe zinawafurahisha wote hasa wanasias??
Ni kwa sababu akili yako imefungwa ktk watu millioni 40 kuandika katiba. Hakuna aliyesema hivyo isipokuwa hatuwezi rudia makosa yaliyofanyika zamani yarudiwe toka mwanzo wa urasimu wa katiba na mchakato mzima..Tunachokitazama hapa ni mapendekezo ya waziri wa sheria ktk muswada huo ambao NDIYO sheria MAMA.

Sisi kama wananchi hatukubaliani na muswada huo hivyo tuna mapendekezo yetu ktk vifungu kadhaa.. Nyie hamtaki kutusikia kwa sababu akili zenu zinawatuma kwamba raisa ndiye mwenye mamlaka yote.Nilikwambia huko nyuma vizuri sana, mfano pendelezo langu la kwanza Tume ichaguliwe ktk kikao cha Bunge kitakachowahusisha Marais wote wawili, makamu wa rais, wabunge (wawakilishi wa wananchi)..

Hapa wanaweza chagua kamati ya Katiba (au kikao kizima) kuhusika na kuchagua majina ya watu kuunda tume kisha kuwakilisha ktk bunge la wazi ambalo mwenyekiti wake (rais) ndiye atayasoma majina yaliyopendekezwa ktk tume hiyo. Kura zitapigwa kuafikia ama kutoafiki mapendekezo hayo..

Pili, Hiyo tume ndiyo itakuwa na mamalaka ya juu kukusanya mawazo ya wananchi, wanasheria, wataalam, wanasiasa na kadhalika juu ya muundo wa katiba yetu na hawa watachagua viongozi wake toka mwenyekiti hadi katibu wao na hawatakuwa answerable to no one na hakuna mipaka ya kutojadili maadam wananchi wanataka kuzungumzia iwe Muungano au Urais, hadi watakapo kamilisha kazi yao. Hawa watakusanya mawazo toka kwa wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi zote za kijamii na kadhalika..

aweza kutokuwa kazi kubwa kama wataitumia katiba iliyopo na kuuliza vipengele vilivyopo vina mapungufu gani au havifai kabisa.. Ibara kwa ibara hadi wamekusanya mawazo ya kutosha na kuwakilsha report yao tena ktk kikao kamati ya Katiba...Na Huo ndio mwanzo yaani hatua ya kwanza - mapendekezo yangu! Well, nisiandike mengi ukasema bado huelewi..ni mawazo yangu na sii lazima yawe sahihi.
 
ukusoma hotuba ya tundu lisu utaona madudu yaliyomo humo..

kijana jibu swali la msingi bila kukopy na kupest ya Lisu kana kwamba unataka kutuaminisha na kutwambia huyo Lisu mawazo yake hayana madudu? kitu ambacho si sahihi hata kidogo.
 
Ni kwa sababu akili yako imefungwa ktk watu millioni 40 kuandika katiba. Hakuna aliyesema hivyo isipokuwa hatuwezi rudia makosa yaliyofanyika zamani yarudiwe toka mwanzo wa urasimu wa katiba na mchakato mzima..Tunachokitazama hapa ni mapendekezo ya waziri wa sheria ktk muswada huo ambao NDIYO sheria MAMA.

Sisi kama wananchi hatukubaliani na muswada huo hivyo tuna mapendekezo yetu ktk vifungu kadhaa.. Nyie hamtaki kutusikia kwa sababu akili zenu zinawatuma kwamba raisa ndiye mwenye mamlaka yote.Nilikwambia huko nyuma vizuri sana, mfano pendelezo langu la kwanza Tume ichaguliwe ktk kikao cha Bunge kitakachowahusisha Marais wote wawili, makamu wa rais, wabunge (wawakilishi wa wananchi)..

Hapa wanaweza chagua kamati ya Katiba (au kikao kizima) kuhusika na kuchagua majina ya watu kuunda tume kisha kuwakilisha ktk bunge la wazi ambalo mwenyekiti wake (rais) ndiye atayasoma majina yaliyopendekezwa ktk tume hiyo. Kura zitapigwa kuafikia ama kutoafiki mapendekezo hayo..

Pili, Hiyo tume ndiyo itakuwa na mamalaka ya juu kukusanya mawazo ya wananchi, wanasheria, wataalam, wanasiasa na kadhalika juu ya muundo wa katiba yetu na hawa watachagua viongozi wake toka mwenyekiti hadi katibu wao na hawatakuwa answerable to no one na hakuna mipaka ya kutojadili maadam wananchi wanataka kuzungumzia iwe Muungano au Urais, hadi watakapo kamilisha kazi yao. Hawa watakusanya mawazo toka kwa wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi zote za kijamii na kadhalika..

aweza kutokuwa kazi kubwa kama wataitumia katiba iliyopo na kuuliza vipengele vilivyopo vina mapungufu gani au havifai kabisa.. Ibara kwa ibara hadi wamekusanya mawazo ya kutosha na kuwakilsha report yao tena ktk kikao kamati ya Katiba...Na Huo ndio mwanzo yaani hatua ya kwanza - mapendekezo yangu! Well, nisiandike mengi ukasema bado huelewi..ni mawazo yangu na sii lazima yawe sahihi.

Sawa mkuu nakushukuru nimeelewa kidogo kwenye muundo unaoufikiri unafaa naamini kazi hiyo wangefanya wabunge wetu (hasa wa upinzani) kupeleka hayo mapendekezo ya tume iweje ki-muundo..

Utaoona kwenye mapendekezo yako ni Rais atakayewaita hao watu sijui sasa kuna tofauti gani ni hiki kinachofanyika sasa..

Anyway at least wewe umeleta hoja moja tu ambayo tofauti ni muswada ulivyo ni "ndogo sana" hata kuitwa ni upungufu..yale yale,
 
Baada ya kuufuatilia huu mjadala kwa ukaribu nimegundua kuwa swala linalojirudia kwa wanaoupinga mswada ni fursa aliyopewa Rais ya kufanya maamuzi juu ya process ya ukusanyaji maoni. Sijaona lalamiko lingine, labda wenzangu mnisaidie kuliona. Kwa hiyo tunaweza kusema kwa kifupi tu kuwa WANAOPINGA MSWADA HAWANA IMANI NA RAIS.
Sasa labda nilimodify swali la Topical bila kuanzisha thread nyingine.

Je, wanaopinga mswada hawana imani na Rais Kikwete au hawana imani ni taasisi ya Urais? in other words, je wanadhani Rais Kikwete hatafanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa au wanadhani Rais yeyote yule hawezi kufanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa katika swala la katiba?

Labda tukienda hivi tutafika wakati tutaelewana, hata hivyo swali la Topical la kutoa alternative method ni muhimu lijibiwe kwani siajaona aliyeattempt kulijibu.

Ukiangalia mabadiliko ya katiba kwa kumfikiria rais wa sasa (ambaye kwa sasa ni Mhe Dkt JK) utakuwa ni mtu wa kuangalia puani. Hakuna mwenye tatizo la Mhe JK. Tatizo la katiba ya sasa (hii iliyotupitisha katika miaka 50 inayoishia Dec 9, 2011) ni kwamba ilitengeneza urais kuwa umungu-mtu. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa jamii hususan ikitokea tukapata mtu mwenye nati zilizolegea kichwani (kwa bahati nzuri hatujapatwa na masahibu hayo. Lakini hatutaki kuishi kwa kutegemea kudra ya Mungu wakati tumepata fursa ya kufanya mabadiliko). Sasa kama mchakato unampa rais madaraka ya umungu-mtu unatarajia matokeo yake yatakuwa ni nini - si ni kurejea pale pale tulipotaka kujitoa? Kumbuka tunalilia katiba itakayotuongoza kwa miaka hamsini au mia ijayo. Tutakuwa hatujitendei haki wala hatuwatendei haki wajukuu na vitukuu vyetu kwa kukubali kuburuzwa na akili finyu za wabunge wa ccm na vibaraka wao.
 
Wewe kama kichwa kibovu kitaendelea kuwa kibovu tu! Mchakato mzima unaonesha kuwa Katiba itakayoundwa ni "Katiba ya Rais" na si ya wananchi!
1. Wajumbe wa Tume ya Kukusanya maoni ni wateuliwa wa Rais,
2. Hadidu za rejea wanapewa na Rais,
3. Maoni yakishakusanywa anapelekewa Rais ambaye kwa mujibu wa Katiba iliyopo "halazimiki" kufuata ushauri wa mtu yeyote,
4. Tume isiyo huru ya Taifa ya uchaguzi ambaye Mwenyekiti wake ndiye mteule wa Rais, itasimamia zoezi zima la kura za maoni,
5. Baadhi ya masuala kutojadiliwa ni matakwa ya wananchi au matakwa ya Rais?
Kwa ujumla JK anataka kututungia Katiba na sio kuturuhusu wananchi kutunga Katiba iliyo na ridhaa ya kweli ya wananchi! Ndio maana wananchi wanapotaka kuandamana kupinga Muswada wanaambulia moshi wa mabomu ya machozi! Sasa kama huko si kulazimishana ni nini?

Je sheria hii ya sasa imezingatia haya mahitaji yako mkuu?
 
Ukiangalia mabadiliko ya katiba kwa kumfikiria rais wa sasa (ambaye kwa sasa ni Mhe Dkt JK) utakuwa ni mtu wa kuangalia puani. Hakuna mwenye tatizo la Mhe JK. Tatizo la katiba ya sasa (hii iliyotupitisha katika miaka 50 inayoishia Dec 9, 2011) ni kwamba ilitengeneza urais kuwa umungu-mtu. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa jamii hususan ikitokea tukapata mtu mwenye nati zilizolegea kichwani (kwa bahati nzuri hatujapatwa na masahibu hayo. Lakini hatutaki kuishi kwa kutegemea kudra ya Mungu wakati tumepata fursa ya kufanya mabadiliko). Sasa kama mchakato unampa rais madaraka ya umungu-mtu unatarajia matokeo yake yatakuwa ni nini - si ni kurejea pale pale tulipotaka kujitoa? Kumbuka tunalilia katiba itakayotuongoza kwa miaka hamsini au mia ijayo. Tutakuwa hatujitendei haki wala hatuwatendei haki wajukuu na vitukuu vyetu kwa kukubali kuburuzwa na akili finyu za wabunge wa ccm na vibaraka wao.

je sheria iliyopo imewatenda haki wajukuu zako? au umeridhika tu kwakuwa chadema wameridhika?
 
Back
Top Bottom