Ubaya wa Muswada wa katiba kama ulivyo?

tatizo lililopo kwa tanzania ni kwamba atachaguliwa igp ambaye atakuwa attached to the president instead of the country, na ndio kwa mkuu wa majeshi, controller and auditor general, attorney general, etc etc, matokeo yake hata mawaziri na wabunge wanakuwa na msimamo huo. angalia mikataba ya meremeta, rada, iptl, net group, madini, nk nk kutokana na kumpa madaraka makubwa raisi ambaye kutokana na mfumo wetu tunaweza kupata kichaa, sasa mpaka wagunde wananchi au wawakilishi wao utaona wanasema katiba inayo mpa raisi madaraka makubwa haifwai

Ndio muswada huu unataka wewe upeleke hayo maoni kwenye tume then tuyapunguze madaraka ya rais kwenye katiba mpya kuna tatizo??
 
majitu ya humu jf yana matatizo ya ubongo, yaani wao hufikirishwa badala ya kufikiri, yaani wanachukua pumba za tundu ndio muongozo,
 
mleta mada hivi unajua kwanini mswada huu ulibadilishwa lugha kutoka kiingereza na sasa kiswahili..je wabunge walishindwa kusoma kizungu...issue ni kwamba ulikuwa ubadilishwe upelekwe bungeni theni kwa wananchi..je wewe kwako ni sawa
 
Unaonaje ukijadili kama ulivyo una tatizo gani? kwani hata ukipelekwa kwa wananchi halafu ukabaki kama ulivyo ni sawa?

Kama sivyo niambie kasoro za muswada huo kama ulivyo sasa???..mbona swali rahisi tu mkuu
 
Hayo unayoyasema yote ni yako wewe hujaonesha mswaada unasemaje kuhusu hayo, na pia hujatuonesha wa kwanza ni huu na wa pili ni huu. Pumba hatutaki tuwekee mchele.
Shida za kujifukiza ganja ndo hizi huwa huelewi kwa sababu ya ganja....kila kitu kwako ni kupinga hata pale pasipofaa unaudhi kwa kweli na kujifukiza ganja uache
 
Ndio muswada huu unataka wewe upeleke hayo maoni kwenye tume then tuyapunguze madaraka ya rais kwenye katiba mpya kuna tatizo??

hivi ni kweli huoni matizo ya huo mswada au unajifanya chizi tu...tutapeleka mapendekezo yetu ndiyo lakini yatachambuliwa na watu walio chaguliwa na mtu mmoja na baada ya hapo anapelekewa yeye tena.....hii itakuwa katiba ya familia yake si watanzania..halafu juzi anasema eti mbona jkn alifanya hivyo...anasahau kuwa yeye hatunaimani nae.. suti suti
 
Mkuu hivi kwa akili yako ndio umeeleza tatizo la muswada ukaeleweka??

Mfano ukapelekwa kwa wabunge (wengi ccm) wakajadili ukabaki kama ulivyo utakuwa na kasoro gani hiyo hoja yangu mbona swali rahisi tu hamuwezi kujibu au mnafuata mkumbo tu..
 
Nimesoma mkuu ukisoma ni mambo mawili tu niliyoyaona?
1. Kwamba nafasi ya Zanzibar ni kubwa mno??? unafikiri tungefanyeje?? maana ukibadilisha maana yake wazanzibar watataka kusikilizwa tena na haupiti unafirki utaratibu gani ungefaa??

2. Upelekwe kwa mara kwanza ili ujadiliwe?? lakini haonyeshi vipengele vya msingi vyenye shida zaid ya nafasi ya rais lakini anasahau hata wangepita bunge bungeni bado ccm ina nafasi kubwa zaidi?? what options do you suggest??

si tu kwamba uwakilishi wa ccm ni mkubwa lakini bado siku ya siku baada ya bunge kuafiki bado rais ndiye mwenye ku effect hiyo bill. hoja ya kwa nini bill isomwe kwa mara ya pili badala ya mara ya kwanza bungeni kama lawyer apitie vizuri. si kwa kusoma tu kanuni za vikao vya bunge asome na hiyo katiba yenyewe.

Yapo mambo ya msingi ktk mswada huo ambayo wangeweza kuishauri serikali/Kubadili kama taratibu za uwasilishaji wa taarifa na mapendekezo kwa Rais kwa kumpatia raisi muda maalum wa kupitia toka tarehe ya kupokelewa kwa report, watu kuteuliwa kwa sifa zao, kupunguza nafasi ya rais kuja na sura za kirafiki/kichama, na hata tu baada ya rais kuja na majina ya hiyo tuma basi provision iwekwe hapo kutaka majina hayo yaende kwanza bungeni kwa baraka,

Unajua inaboa sana sasa hivi tumeona wabunge kikatiba ni chombo cha kutunga sheria, lakini wameenda mabli zaidi wamegeuka watendaji, wachunguzi, wachezaji wa mpira, wanaharakati, wanataka wapigiwe saruti, kiasi ambacho wamefikia hatua ya kuwa bias, kushawishi hata baadhi ya maamuzi ya msingi yaende kwa maslahi yao, mfano utaona jinsi walivyoweza kuilazimisha serikali kuwapa mikopo ya shs 90/m wakati kilichotengwa na kupitishwa ni shs 45/m, lakini wapo kimya kwa sababu yanawahusu, umeona issue ya double payment, na jinsi CAG alivyowekewa ndita mpaka kwenye budget yake. kwa hiyo nataka kusema haina sababu ya kuchelewesha mchakato wa katiba, la msingi tutoe maoni yetu na tuone hayo mabadiliko kama mbunge asiwe waziri/ mjumbe wa board, wala mkuu wa mkoa,
 
Huyu jamaa anaonekana mshabiki, katika ishu hii nzima.Mabaharia kama vp mumpotezee.Au naye atueleze kilichompendeza katika muswada huo.Ndugu wa mama tofauti mkikua lazima mtahoji udugu wenu.Sasa wanasema tusihonji juu how katika muungano.Hata hiyo huoni Udkt OVER
 
Mkuu hujui nini kasoro ya muswada huu kama ulivyo period! unafuata bendera..lol
 
Hayo unayoyasema yote ni yako wewe hujaonesha mswaada unasemaje kuhusu hayo, na pia hujatuonesha wa kwanza ni huu na wa pili ni huu. Pumba hatutaki tuwekee mchele.

Nadhani kama sote tutachangia hoja kwa jinsi yako basi hakuna tutakachoambulia zaidi ya kuishia kurushiana matusi na kejeli zisizo na maana.
 
Unaonaje ukijadili kama ulivyo una tatizo gani? kwani hata ukipelekwa kwa wananchi halafu ukabaki kama ulivyo ni sawa?

Kama sivyo niambie kasoro za muswada huo kama ulivyo sasa???..mbona swali rahisi tu mkuu
Kasoro unazotaka ni zipi? ni za kimantiki, kiuandishi au zipi? Wenzako walijadili kuwa utaratibu ulitaka baada ya kutayarishwa ulitakiwa upate maoni ya wananchi kabla ya kusomwa mara ya pili. Maelezo yako kwamba ungepelekwa kwa wananchi na ukabaki ulivyo haimaanishi kuondoa ule uhalali wa kupelekwa kwa wananchi.
 
Ukishakuwa na jawabu kibindoni mwako, halafu ukataka watu wakupe jawabu inatia uvivu sana.
 
Shida za kujifukiza ganja ndo hizi huwa huelewi kwa sababu ya ganja....kila kitu kwako ni kupinga hata pale pasipofaa unaudhi kwa kweli na kujifukiza ganja uache

Jaribu na wewe kujifukiza uone raha yake, sasa hii mada inahusiana nini na bangi? Unanchekesha!

Sasa hapo ni kipi hujakipenda? hizo pumba alizomwaga? yeye kaulizwa muswada yeye kaleta yake, kama si pumba ni nini?
 
Mkuu hivi kwa akili yako ndio umeeleza tatizo la muswada ukaeleweka??

Mfano ukapelekwa kwa wabunge (wengi ccm) wakajadili ukabaki kama ulivyo utakuwa na kasoro gani hiyo hoja yangu mbona swali rahisi tu hamuwezi kujibu au mnafuata mkumbo tu..

Jibu rahisi la swali lako ni kuwa kufanya kazi kwa aina hiyo unayoisema ni sawa na mwanafunzi ambaye anajitungia mtihani halafu anaufanya huo mtihani na mwishoni anausahihisha mwenyewe. Hapo kuna kitu cha maana kinachofanyika?Muswada umetoka serikalini (chini ya rais), rais anaunda tume, bunge la katiba, anapokea maoni ya tume ya katiba, atachambua maoni. Je, kuna kitu cha maana kinafanyika hapo. Kama huelewi ndugu yangu, si lazima uelewe.
 
Kwa ufupi mswada hauna matatizo ya msingi. Hakuna mswada unaoungwa mkono na kila mtu hata siku moja. Hivyo visababu alivyolalamikia Tundu Lissu, tunaviheshimu lakini havina uzito wa kuufanya mswada usipitishwe.
Kumbukeni kuwa hata leo ukiwauliza watu kama salenda bridge in umuhimu utapata mawazo tofauti tofauti na huwezi kufuata ndoto za kila mtu.
Kwa hiyo tunachoweza kusema kwa sasa ni kwamba. Tundu Lissu na kambi ya upinzani tunawashukuru kwa kushiriki kikamilifu na kuonyesha udhaifu uliopo kwenye mswada, lakini tunawapa taarifu kuwa udhaifu uliopo unasababishwa na udhaifu wa katiba tuliyo nayo sasa ambayo ni lazima tuiheshimu kama tulivyoapa. Ndio maana hata Tundu ameishia kutoa kasoro bila kuoffer any reasonably practicle solutions.
Tunamuomba Tundu Lissu na watanzania kwa ujumla wasikae kimya wanapoona mapungufu yoyote katika mchakato huu wa kuisaka katiba mpya na marekebisho yatakuwa yanafanyika kadri inavyowezekana na ndio maana mswada ulivyosomwa kwa mara ya kwanza ulirudi kwa marekebisho na vipengele tatanishi visivyokuwa na vifundo vya kikatiba vikaondolewa.
 
[/SIZE]55]Nadhani kama sote tutachangia hoja kwa jinsi yako basi hakuna tutakachoambulia zaidi ya kuishia kurushiana matusi na kejeli zisizo na maana.

Hayo matusi na kejeli niliyoyarusha yako wapi? ili ifikie "kurushiana matusi na kejeli" ni ya nini na yanakhusu nini? mleta mada kasema "naomba kwa dhati kabisa ubaya wa muswada huo kama ulivyo sasa". Hakuna mpaka sasa aliyekuja akasema huo mswaada "hapa ni panavyosema hivi ni pabaya" naona mnamwaga pumba na kile kilichoulizwa au kilichotakiwa mnakikwepa.
 
Jibu rahisi la swali lako ni kuwa kufanya kazi kwa aina hiyo unayoisema ni sawa na mwanafunzi ambaye anajitungia mtihani halafu anaufanya huo mtihani na mwishoni anausahihisha mwenyewe. Hapo kuna kitu cha maana kinachofanyika?Muswada umetoka serikalini (chini ya rais), rais anaunda tume, bunge la katiba, anapokea maoni ya tume ya katiba, atachambua maoni. Je, kuna kitu cha maana kinafanyika hapo. Kama huelewi ndugu yangu, si lazima uelewe.

Ndiyo maana nakuuliza wewe uliyeelewa kasoro za muswada na pengine ulitaka kuwekwe nini badili ya kasoro unayosema??

So far hakuna aliyesema kasoro za muswada ni a,b,c, d...

Sisi tunataka marekebisho a, b, c, d..

Kwasababu a,b,c, d...

kama hili hamuwezi yanini kupelekwapelekwa kama bendera mkuu..naomba mnieleweshe ..
 
Back
Top Bottom