Ubaguzi wazidi kuiangamiza CHADEMA

Ubaguzi wazidi kuiangamiza CHADEMA

FaizaFoxy unakosea sana.
Amani ya nchi inatoweka kwa sababu ya kutotenda haki na udhaifu wa serikali, kama hutoi haki watu wataidai KWA NGUVU.
Serikali itoe haki ya kila mtu bila kumbagua kwa itikadi yake,dini yake,kabila lake au anakotoka alafu serikali iwe madhubuti kukamata mkorofi basi amani ingekuwepo.
Mbona hao watu wa Kaskazini walikuwepo tangia enzi na enzi na pailkuwa na amani?? iweje leo???
Alafu kama unasema CHADEMA mbona ipo nchi nzima siku hizi??? je unamaanisha nini kwa WaCHADEMA wanaotoka maeneo mengine ya Tanzania ??? watu wa Kaskazini amabao ni CCM wao sio wabaguzi??

Usichukie watu kwa ajili ya asili yao usije nawe ukachukiwa kwa ajili ya asili yako

Ni haki ipi uliyonyimwa wewe? ukiongea mambo mazito kama ya haki inabidi uweke na vielelezo la sivyo unakuwa huaminiki. Si umeona post #1 , haipingiki.
 
Soma post #1 usikurupuke.

.......Mie sisomi vichwa vya habari.......kwahiyo ulikuwa unamaanisha watu wote wa Kilimanjaro ni wanachama wa CHADEMA?????? Tunaokuelewa twajua...... you are against people from Kilimanjaro.....swala la udini..no comment..... kwani unaeleweka vilivyo
 
.......Mie sisomi vichwa vya habari.......kwahiyo ulikuwa unamaanisha watu wote wa Kilimanjaro ni wanachama wa CHADEMA?????? Tunaokuelewa twajua...... you are against people from Kilimanjaro.....swala la udini..no comment..... kwani unaeleweka vilivyo

Soma nani anaongelewa wacha kuremba-remba, unani weyee?
 
tutakupiga ban tena, Bibie.

humu haturuhusu hoja zenye ukabila na udini

Soma post namba 1, halafu niambie hiyo hoja yangu udini wake uko wapi na ukabila wake uko wapi?

Usintishe kwa ban, mie ndio JF Ban 1, kama ulikuwa hujui.
 
Ndio, Rais Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete ndiye alikabidhiwa ardhi yote ya Tanzania.
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Nikweli hujakosea ndo maana inagawiwa kama pipi kwakila anayetaka, nasikia putin naye mda simrefu atatinga bongo.
 
MziziMKAVU umetumia nguvu nyingi kutengeneza hoja yako, lakini ukweli ni kwamba wapinzani hawakataa waungane; kwanza kila chama kina mlengo wake.

CCM= Chama Tawala
CUF = Chama cha upinzani chenye nguvu Zanzibar na Bara kinasuasua
NCCR Mageuzi = Chama chenye wabunge 6, hakina nguvu kote bara na visiwani
CDM = Chama chenye nguvu kubwa sana Tanzania bara, Visiwani kinasuasua

Muungano ya vyama uliyopo hai:
CCM na CUF walishaungana zanzibar; so CUF ni part ya chama tawala Tanzania visiwani

Miungano rafiki isiyo rasmi.

CCM na NCCR Mageuzi wameungana, muungano usio rasmi, kitendo cha Mwenyekiti wa CCM kumteua Mwenyekiti wa NCCR kuwa mbunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni ushuhuda tosha kwamba vyama hivi ni vimoja.

Nani aungane na CDM?
CDM chama kinachopigania haki za watanzania hakijawahi kuunganisha nguvu na chama chochote kwa kuogopa yafuatayo:
a) Kuungana na CUF tayari CDM itakuwa sehemu ya chama tawala maana kuna ndoa kati ya CUF na CCM; wana CDM pingeni hili kwa nguvu zote
b) Kuungana na NCCR ambao tayari wana urafiki wa karibu na CCM ni kuwasaliti wananchi wanaowaamini sababu kufanya hivyo mtakuwa na nyie CDM mmeingia urafiki na CCM ( Mntakuwa subset member)

Jibu:

CDM kuweni makini sana na vyama vinavyowafuata kuunganisha nguvu kwani hulete migogoro na hatmaye chama chenu kukosa nguvu.
 
Good analysis. Ila najua kuna watu watakutukana na kukupa majina kibao ya ajabu

Wewe ni Mjinga, TLP ina Viti sita Arusha, ina Diwani mmoja tu hata wakimchukua CCM, who cares? Unalishwa sumu na wewe unakubali tu.. Chadema tukiamua kuchukua Halimashauri ya jiji la Arusha tunachukua anytime, Tuna madiwani wa kata 9, viti maalum 3, wabunge 4, jumla 16, keshokutwa tunashinda Sombetini tutakuwa 17. CCM na TLP hawatuwezi kabisa ndo maana wanaweweseka!
 

UBAGUZI baina ya vyama vya upinzani uliopata nguvu bungeni wakati wa kuanzisha Kambi Rasmi ya Upinzani chini ya CHADEMA, umeanza kutafuna chama hicho chenye ushawishi mkubwa kuliko vyama vingine vya upinzani Tanzania Bara.


Uundwaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, ulitokana na msimamo wa CHADEMA yenye wabunge wengi bungeni, kukataa kushirikisha vyama vingine vya upinzani, ikiwamo CUF ambayo ilikuwa na idadi ya wabunge wanaotosheleza kuunda Kambi ya Upinzani, lakini imezidiwa kiidadi na CHADEMA.

CHADEMA pia ilikataa kushirikiana na NCCR- Mageuzi, TLP, UDP na kuamua kuunda kambi ya wabunge wa CHADEMA pekee, ambapo kwa busara kwa kuwa CUF pia ingeweza kuunda Kambi ya Upinzani, kambi hiyo ya CHADEMA ikapewa jina la Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.

Athari za ubaguzi huo zilijitokeza Arusha hivi karibuni, ambapo chama hicho kilionekana kutaka kuongoza halmashauri ya jiji hilo, lakini kikashindwa baada ya kukosa kura mbili tu za TLP, na jana imejidhihirisha wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Katika siasa za Arusha, baada ya CHADEMA kutetea viti vyake vinne vya udiwani katika uchaguzi mdogo na uliokuwa muhimu kwa siasa za CHADEMA, ilifikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha, huku CCM ikibakiwa na viti 12 na TLP viti sita.

Pia CHADEMA mbali na kuwa na viti hivyo 15, inayo nafasi ya kuongeza kiti zaidi, kwani kuna nafasi moja ya viti maalumu iliyokuwa ikishikiliwa na Rehema Mohamed, aliyetimuliwa mwaka 2011.

Hata hivyo, pamoja na CHADEMA kuongoza kwa kuwa na viti vingi vya udiwani Arusha, haikuwa na uwezo wa kumweka Meya, kwa kuwa idadi ya madiwani wake ni 16 na kingehitaji zaidi ya kura 17 katika baraza, ili kupata nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo.

Hivyo CHADEMA ilihitaji kushirikiana na TLP, ili kupata zaidi ya nusu ya kura inayohitajika kikanuni kumuweka Meya madarakani.

Uvinza Baada ya CHADEMA kusema haina uroho wa madaraka katika umeya wa jiji la Arusha, chama hicho kimejikuta katika mazingira kama ya Arusha, mkoani Kigoma.

Mkoa wa Kigoma, katika halmashauri mpya ya Uvinza, CHADEMA ikishindwa kuishawishi NCCR-Mageuzi kuwaunga mkono, itakuwa katika mazingira ya kukosa nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo mpya.


Katika halmashauri hiyo, CCM ina madiwani wanane, CHADEMA madiwani saba na NCCR-Mageuzi inayo madiwani watano na Mbunge mmoja, ambaye anaingia katika Baraza la Madiwani na anaruhusiwa kupiga kura na hivyo chama hicho kuwa madiwani sita.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA) alinukuliwa akiwataka madiwani wa CHADEMA na NCCR- Mageuzi, kuunganisha nguvu ili CCM iunde Kambi ya Upinzani katika halmashauri hiyo.


"CHADEMA na NCCR-Mageuzi tuna madiwani 13 katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza…CCM ina madiwani wanane tu, hivyo tuna kura nyingi upinzani. CHADEMA ina madiwani saba, NCCR-Mageuzi watano na Mbunge mmoja," alinukuliwa Zitto akishawishi huku akisema wakishindwa kuungana, CCM itapita katikati.

Umoja wavunjika Tofauti na matazamio ya Zitto, kwamba vyama hivyo vingeweka mgombea mmoja dhidi ya mgombea wa CCM, Hamisi Mkwafi, NCCRMageuzi pamoja na kuwa na madiwani sita tu, ilisimamisha mgombea wake, Fidelis Kumbo, na CHADEMA ikaamua kuweka mgombea wake, Cassiano Mabondo.

Katika mazingira yaliyoonesha kuwa vyama hivyo vya upinzani, ikiwemo CHADEMA vilikuwa na uroho wa nafasi ya Mwenyekiti, havikusimamisha mgombea katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ambayo CCM ilijikuta ikiwa haina mpinzani baada ya kumsimamisha Diwani wa Kalya, Lucas Kanoni.

Awamu ya kwanza ya uchaguzi huo uliokuwa ukisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Nicolous Kombe na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ulishindwa kupata mshindi baada ya kila chama kupata kura saba.

Matokeo hayo yaliamsha mjadala wa muda mrefu na mwishowe walikubaliana uchaguzi huo urudiwe, ambapo matokeo yake yalionesha kuwa wajumbe walipigia kura wagombea wa vyama vyao kwani mgombea wa CCM, aliongoza kwa kupata kura nane na kufuatiwa na mgombea wa CHADEMA aliyepata kura saba na wa NCCR -Mageuzi aliambulia kura sita.

Utata Baada ya matokeo ya uchaguzi wa raundi ya pili, mjadala uliibuka tena kuhusu matakwa ya kikanuni, kwamba mshindi anapaswa kupata zaidi ya nusu ya kura za wajumbe waliopiga kura, ambazo ni 11, jambo ambalo hakuna mgombea hata mmoja aliyefikisha.

Msimamizi wa Uchaguzi, Kombe alilazimika kusitisha mjadala huo kwa muda, ili wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wapate ufafanuzi wa kisheria, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Baada ya zaidi ya saa moja ya kusubiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Miriam Mbaga, alisema majibu waliyopata yanaeleza kuwa aliyeshinda kwa kura nyingi, mgombea wa CCM Mkwafi, anapaswa kutangazwa mshindi.

Majibu hayo ya Mkurugenzi yalizua tafrani ambapo baadhi ya madiwani walimtaka Mkurugenzi huyo kufuta kauli hiyo, kwa madai kwamba si kauli rasmi.


Mkurugenzi huyo alilazimika kufuta kauli hiyo, na baadaye Msimamizi wa Uchaguzi, Kombe aliahirisha uchaguzi huo hadi utakapoitishwa upya.

Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Mwenyekiti, wajumbe walikataa kupiga kura kumchagua Makamu Mwenyekiti, ambayo ilikuwa na mgombea mmoja, Kanoni (CCM).

UBAGUZI WAZIDI KUIANGAMIZA CHADEMA - MPEKUZI HURU

Huna Jipya wewe, chadema hatuhitaji ushirika na Giza, Nuru na Giza havina Ushirika hata siku moja... Pia umedanganya kuhusu Arusha, Cgadema tuna Majority Arusha kwa sasa CCM-TLP combine hawafikii idadi ya wajumbe wa Halimashauri wa Chadema, tunasubiri uchaguzi wa kata ya Sombetini uishe, mtasikia mambo yetu, hatutaki ushirika wa kinafiki, NCCR ni CCM 'C'..
 
Ubaguzi mbaya kuliko wote ni wa Kidini, rangi na kabila. Huo unaongelea ni ubaguzi wa nini (kati ya aina hizo tatu nilizotaja)? Kila Chama kinapoanzishwa lengo lake kuu ni kuongoza (huwa kunakua hakuna fikra za kushirikiana na yoyote katika kukamata dola/madaraka). Hii ndio lengo la msingi. Maana yake ni kuwa, chama kinatakiwa awali ya yote kijisimamie chenyewe kutwaa madaraka. Sasa kama inaonekana kuna uwezo wa kufikia malengo hayo mwenyewe, tatizo ni nini?
 
Hatutaki siasa zenu za kidini , ubaguzi (soma post #1 ), upiganaji (kauli mbiu yenu) na sasa mmekuja na ugaidi "red brigades".

Ataewapa uongozi ana matatizo ya kufikiri.

"Chama kilichofilisika kisera husungumzia udini na ukabila; ukiona chama kinazungumzia udini au ukabila..... Ujue kwisha kazi!" - JK Nyerere
Faiza unataka tuamini hapo ndipo mlipofika wenzetu CCM? Poleni!
 
Halafu hao mnataka watu wawape kuongoza nchi?

Wataihamisha nchi yote waipeleke Kilimanjaro.

Data ni za kupika zaidi na unashabikia upumbavu kila siku hakuna post inayoponda cdm ukakosa humu kushadidia mjinga mkubwa wewe.
 
[JFMP3][/JFMP3]

Nikweli hujakosea ndo maana inagawiwa kama pipi kwakila anayetaka, nasikia putin naye mda simrefu atatinga bongo.

Wacha waje wenye ujuzi wao, kama na wewe unaweza nenda kachimbe uranium, dhahabu, almasi, tanzanite, gas, oil na sasa kuna rare earth. Ulikatazwa?

Kumbuka kuna Watanzania kibao walienda nje ya Tanzania maskini wamerudi matajiri na wengine bado wamewekeza hukohuko nje. Na pia kuna matajiri wa Kitanzania wengi wanawekeza nje ya Tanzania. Unalijuwa hilo au hulijuwi?
 
Back
Top Bottom