Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 54,530
- 43,913
FaizaFoxy,Ni mfupi wa kumbukumbu, tutakukumbusha.
Ritz tafadhali mkumbushe huyu kijana Nasari alisema nini.
Mpe hii....
MAJUMA kadhaa yaliyopita Tanzania na Dunia kwa ujumla imeduwazwa na ujasiri wa Mbunge kijana wa Jimbo la Arumeru Mashariki Nassari Joshua (Chadema) pale alipotamka kuwa yeye na chama chake wana mipango ya kujitenga na kuunda Taifa lao.
Taarifa hii licha ya kuwaudhi watanzania wengi wakiwemo viongozi wa chama hicho cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hasa Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, lakini vijana wenzake ambao ambao wanajiita Makamanda walinyosha vidole juu na kushangilia kana kwamba ni jambo jema sana kwa mustakabali wao na vizazi vyao.
Kutokana na matamshi ya Mbunge huyo maarufu kwa jina la Mheshimiwa, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa aliinuka na kukanusha vikali matamshi hayo huku akisema kuwa huo si msimamo wa chama hicho jambo ambalo kwa wazalendo walimsifu Mbowe kwa ujasiri wa kusimamia misimamo ya chama chake.
Miongoni mwa matamshi anayotuhumiwa kuyasema Nassari ni kumpiga marufuku Mkuu wa Nchi kukanyaga Arumeru na Kanda ya Ziwa, eti kwa kuwa maeneo hayo ni ya Chadema na wakati wowote watatangaza Rais wao kama ilivyokuwa Sudani Kusini.
Last edited by a moderator: