Ubaguzi wa rangi au jinsia sio mzuri

Mishenyi

JF-Expert Member
Oct 6, 2019
464
748
Ubaguzi ni kitu kibaya pale ambapo jamii moja uamini ni bora kuliko jamii nyingine kama ilivyo kwa mzungu kuamini anastahili kuongoza kila kitu duniani kwani ngozi nyeusi ina laana"wana amini hivyo"

Akili hizo zipo pia kwenye jinsia mwanamme anaamini yeye ni bora anayestahili kutawala kila kitu duniani huku wakimlazimisha mwanamke kubaki jikoni akipika, waafrika tungejifunza kitu hapa hii tabia ya jamii moja kuibagua jamii nyingine ni siasa inayotengenezwa kwa kipindi kirefu ili kuua vipaji na maono ya jamii nyingine.

Mwafrika anaweza kuongoza shirika lolote duniani na likafanikiwa!! Hivyo wazungu si kila kitu

Hivyo hivyo kwenye jinsia wanawake wanaweza kuongoza taasisi yoyote na ikafanikiwa hivyo mwanamme kuamini yeye ndo kila kitu haina mashiko
 
Umemwingiza mzungu by default tu,hoja yako ilikuwa kuhusu kina mama. Mimi binafsi naamini kina mama ni wa kuchunga sana. Mf Samia na Tulia hawana uwezo kwenye hizo nafasi. Kuna nafasi ni nyeti hatuwezi kupeana kama sadaka.

Tayari Samia kasharudisha uchifu na wizi wa kula kwa urefu wa kamba. Tulia kashasema rais hakoselewi. Kuna nini hapo
 
Tuwape mda tutatoa tathimini kwa walichofanya 2025

Sent from my T702 using JamiiForums mobile app
 
Mwafrika anaweza akiwa nje ya afrika case study hao walioweza wakirudi afrika nao hawawezi kama Waafrika.Rejea wengi waliokabidhiwa nafasi
 
Mwafrika anapenda rushwa na ufisadi

Hapaswi kuaminiwa kupewa nafasi yenye mamlaka kipesa.

Ona hapa Bongo tunavyowaibia waajiri wetu, na waajiri wanavyotuibia waajiriwa
 
Umemwingiza mzungu by default tu,hoja yako ilikuwa kuhusu kina mama. Mimi binafsi naamini kina mama ni wa kuchunga sana. Mf Samia na Tulia hawana uwezo kwenye hizo nafasi. Kuna nafasi ni nyeti hatuwezi kupeana kama sadaka.

Tayari Samia kasharudisha uchifu na wizi wa kula kwa urefu wa kamba. Tulia kashasema rais hakoselewi. Kuna nini hapo
Kwenye uongozi wanawake huwa wanatafuta Ili kulipiza visasi vya kumkomoa mwanaume na sio kuleta ukombozi,rejea ishu ya Mbowe sijui walikwaruzana wapi.
Mwanamke bosi ofisini ukitaka kumfitinisha na mbaya wako hasa mwanaume mwambie huyu mwanaume anakudharau kisa wewe ni mwanamke atashughulikiwa hadi ofisi aione chungu.
Wanaamini Sana umbea wa kuambiwa Ili waufanyie kazi.
Don't mess up with a woman.
Mbowe sio gaidi.
 
Mwafrika anapenda rushwa na ufisadi
Hapaswi kuaminiwa kupewa nafasi yenye mamlaka kipesa.
Ona hapa Bongo tunavyowaibia waajiri wetu, na waajiri wanavyotuibia waajiriwa
Na huu ni ukweli ulio mchungu mno,kuna yeyote anaweza kunitajia nchi ingalau 5 zinazoongozwa na watu weusi na nchi hizo zinafanya vema kiuchumi,demokrasia etc etc
 
Kwenye uongozi wanawake huwa wanatafuta Ili kulipiza visasi vya kumkomoa mwanaume na sio kuleta ukombozi,rejea ishu ya Mbowe sijui walikwaruzana wapi.
Mwanamke bosi ofisini ukitaka kumfitinisha na mbaya wako hasa mwanaume mwambie huyu mwanaume anakudharau kisa wewe ni mwanamke atashughulikiwa hadi ofisi aione chungu.
Wanaamini Sana umbea wa kuambiwa Ili waufanyie kazi
umegusa penye mshono kabisaaaaaa. Hata issue ya Ndugai ni hilo tu. Tunao maofisini wengi tu.
 
Ubaguzi ni kitu kibaya pale ambapo jamii moja uamini ni bora kuliko jamii nyingine kama ilivyo kwa mzungu kuamini anastahili kuongoza kila kitu duniani kwani ngozi nyeusi ina laana"wana amini hivyo"

Akili hizo zipo pia kwenye jinsia mwanamme anaamini yeye ni bora anayeatahili kutawala kila kitu duniani huku wakimlazimisha mwanamke kubaki jikoni akipika,,,waafrika tungejifunza kitu hapa hii tabia ya jamii moja kuibagua jamii nyingine ni siasa inayotengenezwa kwa kipindi kirefu ili kuua vipaji na maono ya jamii nyingine.

Mwafrika anaweza kuongoza shirika lolote duniani na likafanikiwa!! Hivyo wazungu si kila kitu

Hivyo hivyo kwenye jinsia wanawake wanaweza kuongoza taasisi yoyote na ikafanikiwa hivyo mwanamme kuamini yeye ndo kila kitu haina mashiko
Wewe kama hutaki huo ubaguzi, basi pambana kwanza na yule aliyetubagua tangu awali kwa misingi ya jinsia zetu! Yaani kwa nini tusiitwe kwa jina moja tu? Mfano Binadamu! Kinyume na hapo, basi ujue umeleta mada ya kutafuta huruma pasipo na sababu ya msingi.

Kitendo cha kuwepo tu na huo utofauti, tayari ni ubaguzi! Sasa huo usawa unao utaka unatoka wapi? Au kama vipi kama unaona sisi wanaume ni wabaguzi kwa wanawake, basi badili jinsia ili na wewe uwe mwanamke! Kama njia sahihi ya kuukataa huo ubaguzi.
 
Ubaguzi ni asili ya binadamu Jamii yeyeto isiyofanana kwa namna yeyeto haiwezi kaa pamoja.Elimu na dini ushinda ubaguzi
 
Naunga mkono hoja ubaguzi ni kitu kibaya sana .. tena sana .. MWALIMU alipinga sana ubaguzi wote.. kuanzia udini,ukabila,rangi mpaka jinsia na mabaguzi mengine cha ajabu sasahivi unakuta mpaka kwenye familia baba/mama mmoja lakini wanabaguana sijui Nani? Katupa ujinga huu .. huu ni ujinga kabsa leo anapondwa mama SAMIA na Jopo lake watu wamesahau kama mama ELIZABETH kama yupo na yeye ni kiongozi huko kwao na kunaendelea vizuri tu.. sisi tumelongwangwa kitambo tu
 
Badala tujikite kuchapa kazi!! Tunalalamika eti mwanamke kaongoza!! Mwafrika anadhihirisha ni dhaifu
 
Umemwingiza mzungu by default tu,hoja yako ilikuwa kuhusu kina mama. Mimi binafsi naamini kina mama ni wa kuchunga sana. Mf Samia na Tulia hawana uwezo kwenye hizo nafasi. Kuna nafasi ni nyeti hatuwezi kupeana kama sadaka.

Tayari Samia kasharudisha uchifu na wizi wa kula kwa urefu wa kamba. Tulia kashasema rais hakoselewi. Kuna nini hapo
Facts tupu umeongea
 
Wanaume tulizoea pamoja na kuongoza miaka 60 bado tunasumbuliwa na uhaba wa vyoo mashuleni achana na makubwa makubwa ,,,,acha wanawake waongoze,tulifika wakati tunaitana wanyonge!!! Aisee!
 
Back
Top Bottom