Dhana isiyosemwa; Hofu ya ushirikina imedumaza maendeleo ya kijamii ya Maeneo mengi yenye historia ya kukaliwa na waarabu hapa nchini

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,883
5,191
Ukitembelea au Kuishi maeneo kama ya Tabora town, Lindi town, Kigoma town Na yanayofanana na hayo, kuna ufanano mkubwa wa hali ya Maendeleo ya kijamii duni i.e Makazi, huduma za afya, Elimu na Miundombinu kama barabara za hovyo. Kijamii miji hii imekua na sifa kubwa sana ya wazee wakongwe wa Ushirikina.

Ni katika miji hii mabwana afya, MEOs & WEOs huogopa kusimamia utaratibu wa mipango makazi kwa hofu ya kulogwa kama mwenzao fulani aliyerogwa. Huku ni kawaida kukuta sehemu chafu na kahawa/ chakula kinauzwa pembeni na jirani kuna ofisi ya afisa afya.

Huku ndio watumishi wa umma aggresive wamekumbwa na kadhia za kulazwa nje.

Hofu ya kurogwa kwa watumishi wa umma, viongozi pale wanaposimamia maamuzi ya kimaendeleo imejenga fikra na tamaduni hasi zilizokwamisha Maendeleo ya maeneo hayo kwa miaka mingi.
 
Sijakuelewa umetumia neno dhana,hofu je wewe hauamini uchawi upo maeneo hayo?
 
Back
Top Bottom