Ubaguzi na dharau uko kila sehemu, unahitaji jicho la tatu kuona mambo

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,781
7,542
Wengi tunadhani ubaguzi ni wa rangi tu, hapana kuna ubaguzi wa nchi kubaguliwa bila kujali rangi zao. Mimi nataka kuongelea Tanzania tu. Nchi yetu kuna matabaka tofauti, Mswahili, mwaarabu. Indian na mpaka wasomali lakini sote ni wa Tanzania.

Kuna jambo mimi muda mrefu limekuwa linanikera sana hasa haya mashirika ya ndege yanyokua Tanzania kama Emirates, Qatar na hata Oman air. Haya mashirika ndege wanazoleta kwetu ni za zamani sana kwa maana viwango vidogo sana hizi ndege hawazipeleki nchi zingine ila Tanzania( Nasema Tanzania sababu kwingine sina uhakika) Ndege wanazotumia kuja huku ni very old. Chukua mfano mdogo kutoka Dubai kwenda Qatar ni saa moja tu lakini wanapeleka ndege mpya kabisa safi na bei ndogo, lakini kuja Tanzania karibia masaa matano na bei ziko juu ila ndege za zamani sana mpaka baadhi ya viti vimeanza kuvunjika.

Sasa swali je kosa ni letu sisi kama nchi kukubali hawa jamaa kutuletea ma Leyland huku au tuna uwezo kuweka vigezo standard fulani tu tunakubali. Ningependa kujuwa kama nchi je tunaweza kuwaambia nini kinakubalika kwetu kwa maana hii hali ni miaka sasa inafanyika. Na uhakika hakuna ndege kama hii wanayoleta kwetu ikaenda nchi zingine. Kwangu mimi huu ni ubaguzi mkubwa.
 
Hata wewe mwenyewe ni mbaguzi

Angali pale home unavyofua , nguo nyeupe hutaki kuzichanganya na nyeusi..

Kila Mbaguzi kwa asili.
 
Kama wameshindwa kusimamia ujenzi wa vyoo kwenye shule yenye wanafunzi zaidi ya 300 (inamatundu mawili "2" ya vyoo) huko wilayani Kaliua mkoani Tabora...... Kamwe serikali haina la kufanya wala kusema kwenye shirika la ndege linalo toa huduma kuja bongo mkuu, maana hata hiyo ndege chakavu ni kama wamesaidiwa.
 
Back
Top Bottom