Mkuu huyo Jamaa ni ' Mwanangu ' sana tena tokea Mwananyamala enzi hizo na nimeandika hayo kwa ' masikitiko ' makubwa mno huwezi amini Mtu wangu. Na hatari zaidi ' akishalanduka ' tu basi ghafla hapo hapo anageuka ' ngumi jiwe / mgomvi ' sema uzuri wake hata ' Ugomvi ' nao anaujua vile vile kutokana na kwamba ni Mtoto wa Kisela sana halafu alishafanya ' matukio ' makubwa na ya kutisha sana pande za Mwananyamala na najua wapo humu Watu wa Mwananyamala wanaomjua ' Kindakindaki ' pia.
Narudia tena kusema na kusisitiza kuwa japo ana hayo ' mapungufu ' yake yote ila ' Jamaa ' ana ' Vipaji ' vingi sana na ni ' Mbunifu ' mno kiasi kwamba kama akipata Mshauri / Kiongozi / Msimamizi mzuri sisi Wasikilizaji wa Redio tutafaidika nae sana. Ushawishi wake mbele ya Jamii hasa ya Vijana ni kubwa mno. Personally namkubali kinomanoma!