Ubabe wa Clouds FM uangaliwe

DissDotCom

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
395
268
Habari wakuu,

kiukweli nimekua mdau wa media kwa muda sana na kujua mazuri na mabaya ya baadhi ya media.

Leo acha niongelee hii redio clouds fm juu ya mambo wanayoyafanya ambayo ni kama vitendo vya kikatili.

Mwanzoni wasanii wengi walikua wanailalamikia redio hiyo kuwa ndio wanaowadhurumu kazi zao na mapato yao kwa kuwapa masharti magumu ambayo mwisho wa siku yanawakandamiza wasanii na hatimaye kujikuta kuishia masikini na kutonufaika na kazi zao za kisanii.

Kikubwa zaidi ni hiki cha kuingilia tasnia ya utangazaji, ambapo mwanzoni wakati huo kuna mtangazaji anafahamika kwa jina la paul james "p.j" ambaye ni moja kati ya watangazaji mahili na wenye weledi katika tasnia ya habari, lakini wakati fulani alihama redio hiyo na kuhamia e f.m redio ambapo aliambatana na mtangazaji mwenzake "gerald hando" ambapo walifanya kazi nzuri sana na kufanya kipindi walichotangaza kuwa moja kati ya vipindi pendwa vya asubuhi.

Lakini hawa clouds fm wakafanya ya kufanya wakamrudisha clouds fm p.j lakini hakupewa hadhi kama ile aliyokuwa nayo awali kabla hajahama na hii kumfanya mtangazaji huyo kushuka thamani kwa sasa.

Vilevile e f.m ilikua na mtangazaji wake mahili sana hasa katika kipindi cha genge ambacho alivuma sana na aina ya mziki wa singeri ambapo mtangazaji huyo alijulikana kwa jina la kicheko, kama haitoshi clouds fm wakafanya ya kufanya na hatimaye kumnyakua kicheko na uhamisho wake ulivunja record ambayo haijawahi kutokea kwani alisindikizwa na bodaboda takribani 150, pamoja na kuwa na thamani kubwa alipokua e f.m lakini alipotua clouds fm hakupewa thamani ile ambayo alistahili kwni akawa anapewa segment ndogo sana na kuna wakati huwa hasikiki kabisa..

Sasa hii imejidhihirisha kuwa hawa clouds fm wapo kwaajili ya kuua vipaji na sio kuendeleza....
 
Back
Top Bottom