Uarabuni hamna demokrasia, hamna umaskini

Tabia za kindezi za mbuni. Kutoona tatizo ndio kulitatua.
 
Demokrasia ni nini? Ni mfumo wa kiuongozi uliokubaliwa au unaokubalika na jamii husika, ukiwakilisha maslahi ya wengi, na wakiwakilishwa au kuongozwa na wachache waliowaridhia au kuwachagua.
Je hizo nchi, ni kweli hazina demokrasia au mleta uzi hujui tafsiri ya demokrasia?
Pengine hawana vyama vya siasa, au ngo, ila wana aina ya utaratibu wa kuendesha mambo yao ambayo ni wa kidemokrasia, nikimaanisha umeridhiwa na wengi.
Tofauti yao na sisi. Wana utajiri mkubwa au mwingi kiasi kwamba, hata wanaofanya ubadhirifu wameukinai, na matokeo yake inawabidi wawape na wananchi wote.
Sisi hatuna utajiri huo ndio maana ni wabadhirifu wanaotujia kwa kila aina ya ghilba, hujitajirisha wao na wengine wakibaki na upambe.
 
Wazawa wa nchi hizo wapo wachache na mapato ya mafuta ni makubwa sana hivyo per capita income ni kubwa kwa kila mtu.
UAE, Kuwait na Qatar kwa mfano wafanyakazi wa kigeni ni wengi kuliko raia.
Kama mtu unaishi vizuri NGO na demokrasia za nini, lakini sio sisi makapuku.
 
Mtoa mada ametaja kabisa Nchi anazozingumzia Qatar, Kuwait, Oman, Bahrain, Saudi Arabia na UAE wewe umeenda kuongeza Yemen an Afrika Kaskazini. Haya weka na Somalia basi ufurahi maana Wagalatia huoni raha bila kuchomeka maneno ya kero
Ameumia kusikia waarab maana alitarajibasikie Roma au Israel dah
 
Ndugu sema ngoja uchaguliwe wewe sio wachague wanaowataka.
 
Eswatini nako hakuna demokrasia, hata Tanzania maana hatukuruhusiwa kuwachagua tunao wataka. Umeona ukosefu gani wa umaskini Eswatini na Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…