Uarabuni hamna demokrasia, hamna umaskini

Hakuna mahali pasipo na demokrasia, tatizo watu wanataka kuwawekea wengine aina zao za demokrasia.
 
NI kweli hizo nchi hazina Demokrasia, Ila pia unatkaiwa utambue kuwa ndani ya hizo nchi hakuna Uonevu, Ubaguzi kwa raia zaidi ya viongozi kuwapenda na kuwajali raia wake.

Nyinyi CCM hamutaki Demokrasia wakati huo huo Munaleta Uonevu, Ubaguzi, Viburi na zaidi ya yote kuzidi kuizamisha nchi kwenye umaskini kwa kadri ya siku zinavyokwenda.
 
Nafikiri Wana utajiri mwingi sana, kiasi kwamba, hata wenye mamlaka wakiiba, bado kunabaki kiasi kingi cha kuwapa wasio na mamlaka
 
Watanzania tuna Njaa (full stop). Tutafute pesa hayo mademokrasia labda 2300 hukoo
 
Hiyo nayo ni demokrasia
Demokrasia siyo kuwa na vyama vya siasa vingi
Kama wananchi wanakubaliana jinsi viongozi wanavyopatikana, hiyo demokrasia
 
Huko wanafata sharia. Wananchi wao wanapata basic needs, Hakuna ufisadi kodi zao zipo salama.
Uislamu bado ni mfumo bora tena wa haki wa kuongozea jamii.
Mfumo huu unapotumika unafukuza umasikini.
 
Sasa mbona waliandamana dhidi ya serikali na watu wengi kuuawa sana?

Tunisia, Algeria, Libya, Misri, Yemen, Syria, Sudan n.k
 
Wabantu tusubir msaada wa ARV
 
Sasa mbona waliandamana dhidi ya serikali na watu wengi kuuawa sana?

Tunisia, Algeria, Libya, Misri, Yemen, Syria, Sudan n.k

Mkuu hizo nchi ulizozitaja sio nchi za kifalme, ni nchi zinaoongozwa kwa mfumo wa kidemokrasia zenye viongozi madikteta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…