Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,797
- 12,239
Sijui viongozi wetu wanawaza nini lakini kwa kifupi ama wamepotoka au wanapotoshwa. Filamu ya aina ya Royal Tour si ya kwanza kuandaliwa duniani, ndugu zetu wa Rwanda walikwisha iandaa na imekwisha tazamwa sana. Sasa sijui kama viongozi wetu walikwisha fanya research ndogo tu kuona imeinufaishaje Rwanda. Manufaa ambayo kama Rwanda imepata basi yasingeweza kuwa siri ya ndani ya Rwanda bali pia spill over tungezipata hapa Tanzania au nchi nyingine za jirani.
Kitu cha kuzingatia ni kuwa wazo la kuandaa filamu hizi si la kwetu bali la hao wenye kumiliki uchumi lakini gharama ni za kwetu. Siyo siri katika kujenga uchumi wa nchi hakuna rafiki bali mwenye nguvu ndiye hushinda na kufaidi. Akili mu kichwa! Walio andaa wamefanikisha malengo yao bila jasho na kwa gharama nafuu.
Uzinduzi wa Royal Tour umekuwa balaa zaidi kwa hazina ya nchi! Rais wa nchi akiwa na wapambe wapatao 50 wamekaa zaidi ya wiki mbili nchini Marekani kufanya uzinduzi wa filamu hii kwa gharama za Watanzania walipa kodi. Wamarekani wamenufaika kwa kutembelewa na watalii kutoka Tanzania. Big brain amenufaika!
Kama hiyo haitoshi sasa uzinduzi utafanyika tena Tanzania kwa kodi zetu. Uzinduzi utafanyika Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam. Tena washiriki watakuwa wengi zaidi! Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma! Tumepigwa!
Tujisahihishe!