Uanaharakati katika vita vya kupata Katiba Mpya Tanzania

DaudiAiko

Senior Member
Dec 2, 2012
130
225
Wana bodi,

Mengi yamejadiliwa kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mashtaka ya ugaidi yanayo mkabili.

Je, uanaharakati tunaoushuhudia haswa kutoka kwa wapinzani unaweza kudumu kwa muda mrefu na kuleta mabadiliko ya aina yoyote?

Mchakato wa kupata katiba mpya miaka kadhaa iliyo pita hauku zaa mafanikio yoyote kwasababu wahusika walishindwa ku kubaliana kuhusu mfumo wa serikali. Ili kuwa na kampeni ambayo inaweza kuleta mabadiliko, wana CHADEMA wana takiwa kuwa na sababu za msingi au mapungufu kwenye katiba tuliyo nayo sasa hivi pamoja na tume ya uchaguzi.

Inawezekana kwamba njia pekee ya ku wasilisha mapungufu ya katiba na kuweza kusikilizwa ni kwenda mitaani lakini je wana CHADEMA wana uwezo na rasilimali watu wenye udhubutu na nidhamu ya kutosha?

Je, Tanzania ni nchi rafiki kwa mtu yeyote au kundi la watu lolote linalo pinga maamuzi ya serikali hadharani? Ukweli ni kwamba uana harakati una hitaji watu ambao wako tayari kwa lolote. Iwe kufungwa, ku chukuliwa hatua kali za sheria na kadhalika. Ninapo wa angalia wana CHADEMA nina hisi kwamba ni wepesi kugawanywa na tofauti na "generation" ya wakina Freeman Mbowe, hawana nguvu sana kuendeleza mashambulizi dhidi ya serikali.

Tafakari,
Jumanne njema.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,654
2,000
Wewe mtu suala la kudai katiba mpya sio suala la chadema pekee, ni la watanzania wote!
 
Godo

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
336
500
Hizo harakati kuna kosa la uhaini mbele yake nyie fuateni mkumbo

Tanzania ni nchi ya amani kwanza hivyo vitendo viovu havijawahi kutokea hapa kwetu.

Katiba yetu ipo wazi kama mtu yeyote hajaridhika na kipengele chochote ndani ya Katiba aende Mahakamani akafungue shauri na atasikilizwa na Mahakama itatoa maamuzi kama kipengele kipo sawa au kirekebishwe lakini huo mchezo wenu mnashinikizwa na hao wakorofi yaani hata ukiulizwa kipengele gani hakipo sawa hujui hata hiyo katiba yenyewe hujawahi hata kuiona inafananaje huna facts zozote zaidi ya kushinikizwa na CHADEMA.

Jamani hapo tu ndio tunapotofautiana na wazungu waingereza hata hiyo kopi ya katiba hawana(unwritten constitution) wanaongoza kwa tamaduni za nchi yao na makubaliano mbalimbali waliyojiwekea, lini umesikia wana hizo mambo zaidi ya kujikita kwenye kujiimarisha kwenye uchumi wao.

Mkiambiwa mambo ya Katiba mpya tuweke pembeni kwanza tujenge uchumi kwanza hamtaki.

Fanya kazi upate maendeleo na familia yako hayo masiasa ya hovyo ya kina Mdude yaani msomi na elimu yako unakaa unafuata nini Mdude anasema.
 
DaudiAiko

Senior Member
Dec 2, 2012
130
225
Wewe mtu suala la kudai katiba mpya sio suala la chadema pekee, ni la watanzania wote!
Sidhani kama wananchi wame pata hamasa kubwa kutoka kwa hotuba na "movement" zinazo endeshwa na viongozi wa CHADEMA. Vile vile kushiriki katika shughuli kama hizi kikamilifu kuna hitaji "sacrifice" kubwa ambayo
wachache sana wanaweza kujitoa.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,115
2,000
Wana bodi,

Mengi yamejadiliwa kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mashtaka ya ugaidi yanayo mkabili.

Je, uanaharakati tunaoushuhudia haswa kutoka kwa wapinzani unaweza kudumu kwa muda mrefu na kuleta mabadiliko ya aina yoyote?

Mchakato wa kupata katiba mpya miaka kadhaa iliyo pita hauku zaa mafanikio yoyote kwasababu wahusika walishindwa ku kubaliana kuhusu mfumo wa serikali. Ili kuwa na kampeni ambayo inaweza kuleta mabadiliko, wana CHADEMA wana takiwa kuwa na sababu za msingi au mapungufu kwenye katiba tuliyo nayo sasa hivi pamoja na tume ya uchaguzi.

Inawezekana kwamba njia pekee ya ku wasilisha mapungufu ya katiba na kuweza kusikilizwa ni kwenda mitaani lakini je wana CHADEMA wana uwezo na rasilimali watu wenye udhubutu na nidhamu ya kutosha?

Je, Tanzania ni nchi rafiki kwa mtu yeyote au kundi la watu lolote linalo pinga maamuzi ya serikali hadharani? Ukweli ni kwamba uana harakati una hitaji watu ambao wako tayari kwa lolote. Iwe kufungwa, ku chukuliwa hatua kali za sheria na kadhalika. Ninapo wa angalia wana CHADEMA nina hisi kwamba ni wepesi kugawanywa na tofauti na "generation" ya wakina Freeman Mbowe, hawana nguvu sana kuendeleza mashambulizi dhidi ya serikali.

Tafakari,
Jumanne njema.
kwanza kabisa, katiba mpya sio suluhisho la matatizo yote Tanzania, kunaweza kuwa na katiba mpya and still maisha yakawa ni hayahaya tu. pili, Mama kasema tujenge uchumi kwanza, sasa ninyi mnaoleta vidomodomo leteni kama ni wasafi, lakini mkileta ujinga wakati pengine mwaka jana mlikuwa mnafanya maandalizi ya ugaidi na kumwaga damu na kuchoma vituo vya mafuta na vurugu, mafaili yenu yatafufuliwa hata kama mlitakiwa kusamehewa. akili za mbayuwayu changanya na za kwako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom