U.S.A, China, Singapore wanatufundisha mambo gani na vipi kuhusu nchi nyingine?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,353
Meza ya siasa na uongozi
Somo lililopo mezani je, ni mambo gani Singapore, U.S.A na China wanatufundisha sisi nchi iliyo poteza dira ?

Kwangu mimi kama tukitaka kujifunza Vyama bora vya siasa, Mifumo/taasisi imara na Bunge bora Basi yatupasa kuzama hizi nchi.

Kwa Bunge bora
Hapa tutazame na tujifunze mwenendo na utendaji wa bunge la Singapore kuna vitu tutajifunza na kuepukana na huu uozo tulionao Dodoma.

Kwa Vyama bora vya siasa
Hapa tutazame muundo na utendaji kazi wa chama kikomunisti cha wachina kinafanya vizuri na imara kama chama cha siasa ni mfano wa kuigwa na kuepukana na huu utitiri wa magenge ya wapiga kelele yaitwayo vyama vya siasa yaliyopo hapa nchini.

Kwa mifumo/taasisi imara
Hapa tujifunze kwa hawa manguli wa amerika ni bora sana kwa umri wa taifa lao mpaka sasa wameweza kuwa na taasisi independent na bora kabisa kwa mfano wa kuigwa utakao tuepusha na changamoto mbalimbali za taasisi zetu mbovu hapa nchini.

Haya nawe ongeza wapi tujifunze katika
  • Mahakama
  • Serikali za mitaa
  • Serikali kuu
  • Majeshi
  • n.k
 
Back
Top Bottom