Uchaguzi 2020 Twende na Bernard Membe, tuunde Serikali ya kazi na bata! Naomba kura zenu

Membe, wanadai wewe umetumwa na CCM kuja kugawa kura za upinzani. Je, kilichokuondoa CCM ni nini? Na humuwezi Lissu ki ukweli.

Kosa lako ulilofanya ni kumdharau mwenyekiti wako, ilitakiwa kukaa kimya washangae tu umechukua fomu.
Wakati mnampokea hamkujua kuwa katumwa?
 
20201024_152106.jpg
 
Yaani bora hata alivyokuwa Mhe. Lowasa, nina wasiwasi usiyo na shaka kabisa Mhe. Membe hakujiandaa kuwa Mgombea wa Urais nje ya CCM.

Nje ya CCM, Benard Membe amekuwa hasikiki kabisa bora hata ya Mgombea wa CHAUMA
Ahahahahaha.....Membe tena,Da walishamtupa lando waungwana.
 
Hii account imefunguliwa Leo,yaaani ccm wanatapatapa sana.Hakuna kugawa kura tunamchagua Lissu,na Membe kesho atakuwepo pale Kawe kukamilisha hili zoezi.
Kama imefunguliwa leo mbona uongozi wa jamiiforums wamempa heshima ya verified member
 
Unamalizia mkataba wa pesa CCM walizo kupa Dubai, umeshindwa kuzirudisha. huo mkutano chama chako kina taarifa
 
Watanzania na wapiga kura wenzangu salaam,

Mimi Bernard Kamillius Membe ni mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Tarehe 28/10/2020 ni siku ya kupiga kura ya kurejesha Uhuru uliopotea tangu awamu ya tano iingie madarakani miaka mitano iliyopita.

Ni siku ya kuchagua mtu anayefaa kuliongoza Taifa, Mtu mwenye uzoefu, Mzalendo na mwenye uchungu na maendeleo ya Nchi yetu.

Puuzeni watu wanaosema nmejiondoa kwenye kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Twendeni mkanipigie kura mimi Membe Bernard Kamillius ambaye nmekidhi vigezo vyote. Nipigieni kura tuwe na Serikali ya Kazi na Bata.

Mimi nitafunga Kampeni yangu tarehe 27/10/2020 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi.

Nawakaribisha wote.

Asanteni kwa kunisikiliza

siku zote hizi hujafanya kampeni kesho ndio ufanye mkutano wa kufunga kampeni. haki umetumwa na ccm uwagawe wapinzani kwenye kura
 
Watanzania na wapiga kura wenzangu salaam,

Mimi Bernard Kamillius Membe ni mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Tarehe 28/10/2020 ni siku ya kupiga kura ya kurejesha Uhuru uliopotea tangu awamu ya tano iingie madarakani miaka mitano iliyopita.

Ni siku ya kuchagua mtu anayefaa kuliongoza Taifa, Mtu mwenye uzoefu, Mzalendo na mwenye uchungu na maendeleo ya Nchi yetu.

Puuzeni watu wanaosema nmejiondoa kwenye kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Twendeni mkanipigie kura mimi Membe Bernard Kamillius ambaye nmekidhi vigezo vyote. Nipigieni kura tuwe na Serikali ya Kazi na Bata.

Mimi nitafunga Kampeni yangu tarehe 27/10/2020 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi.

Nawakaribisha wote.

Asanteni kwa kunisikiliza

Barua yako unasema uliwapa tume nakala na uliandikia chama chako barua sasa unagombeaje tena. Umetumwa kuigawa ACT, umefeli.
 
Huu mkutano wake wa mwisho unaweza kuunganishwa na vyombo vikuu vya habari ili asikike akifunga goli lake la ushindi katika dakika ya mwisho. Goli lenyewe huenda ni kuwataka wapiga kura angalau wa jimbo lake wampigie kura Rais atakayekuja kumuomba kama akishinda.
 
Back
Top Bottom