Uchaguzi 2020 Twende na Bernard Membe, tuunde Serikali ya kazi na bata! Naomba kura zenu

Bernard Membe

Verified Member
Oct 19, 2020
1
75
1603716193507.png

Watanzania na wapiga kura wenzangu salaam,

Mimi Bernard Kamillius Membe ni mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Tarehe 28/10/2020 ni siku ya kupiga kura ya kurejesha Uhuru uliopotea tangu awamu ya tano iingie madarakani miaka mitano iliyopita.

Ni siku ya kuchagua mtu anayefaa kuliongoza Taifa, Mtu mwenye uzoefu, Mzalendo na mwenye uchungu na maendeleo ya Nchi yetu.

Puuzeni watu wanaosema nmejiondoa kwenye kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Twendeni mkanipigie kura mimi Membe Bernard Kamillius ambaye nmekidhi vigezo vyote. Nipigieni kura tuwe na Serikali ya Kazi na Bata.

Mimi nitafunga Kampeni yangu tarehe 27/10/2020 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi.

Nawakaribisha wote.

Asanteni kwa kunisikiliza


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom