Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

ndonger

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
875
1,544
Yaani tusijidanganye hata siku moja.

Watu weusi tunajisemaga tuko na maguvu etc..

Ila kwa jinsi hawa wenzetu ngozi nyeupe wanavyopiga kazi speed yao kama umekaa kibwegebwege utakuwa unalia kila siku

Hawa jamaa ni nuksi jamani, yaani huku kufanya kazi saa 12 + ni jambo la kawaida sana.

Halafu wako speed kama legelege lazima utapike dagaa.

Watu weusi tuko polepole sana hata kazi nchini kwetu infact ukisema u rate kwenye scale ya 10
Hawa wenzetu wako 9/10 sis tuko 1/10

Yaani hakuna kitu wakuu, nadhani hii ndio siri kubwa ya wao kutupiga gap la maana achana na kelele za ohh walikuja kuiba malighafi Afrika hizo ni kelele za kujitetea tu hawa jamaa ni watafutaji yaani wana ile spirit ya kichaga na kikinga mara 100

Ni hayo tu wadau, tupambane. sana

Na haijalishi ni me au ke hawa watu ni hatari na wanaanza michakato wadogo kabisa yaani 18yrs mtu anapiga kazi
 
Mwafrika hasa mtanzania anataka apige kazi masaa nane tena hayo bado anaona ni mengi,

Awahi kutoka kazini apitie baa amwagilie moyo na nyama choma huku akibishana simba na yanga.

Wanawake wanataka wawahi kutoka kazini wapitie saluni wakajirembe huku wakipiga soga na umbea.

Halafu jumapili wakajazane makanisani wakipayuka kama mbayuwayu kumuomba Mungu wapate mafanikio.

Hawa ndio waafrika..!!
 
Ujutume kwa bakhresa alafu unapewa 4000 a u Silas kule mkwanja mrefu ndo maana wakimbizana na muda kila lisaa ni pesa kwao ila huku umbuzi mwingi......ukija na mada kama hii unatakiwa uweke na scale za misharaaa bosa
Kila eneo lina value for money yake .unakuta huko unalipwa buk4 ila unaweza kula milo mi4...huku pia mishahara mikubwa ila expensive life ingawa huko kumezidi..mnanyonywa sana
 
Mwafrika hasa mtanzania anataka apige kazi masaa nane tena hayo bado anaona ni mengi,

Awahi kutoka kazini apitie baa amwagilie moyo na nyama choma huku akibishana simba na yanga.

Wanawake wanataka wawahi kutoka kazini wapitie saluni wakajirembe huku wakipiga soga na umbea.

Halafu jumapili wakajazane makanisani wakipayuka kama mbayuwayu kumuomba Mungu wapate mafanikio.

Hawa ndio waafrika..!!
Na ndani ya hayo ayo masaa nane ya kazini humo ndani ndio kuna lisaa la chai, lisaa la lunch, lisaa la kupiga umbra kwenye simu na muda wa kubishana Simba na Yanga pia.
 
Nadhan wenzetu nafasi za kazi zipo nyingi sana kutokana na viwanda ni vingi, ndio maana mtu anaweza kufanya kazi hata tatu kwa siku na analipwa kwa masaa

Kwahiyo wana kila sababu ya kupiga kazi sana
Na hawachagui sana..huku kukuta mtoto maisha mazur home..anapiga kaz ya kibarua supermaket ni kawaida .yaan level ya kuona noma hawana hawa watu..kila mtu na maisha yake
 
Back
Top Bottom